MASHARTI YA KUPUNGUZA SWALA
Suali: Ni yapi Masharti ya kupunguza Swala ? Na kupunguza Swala inaisha mda gani ?
Jawabu: Ama baada ya kumshukuru na kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake :
Ni sharti kwa mtu anaetaka kupunguza Swala: awe mtu huyo ni msafiri ambae safari yake ya kwenda inafika kiwango cha kupunguza Swala nayo ni Burd nne ambayo ni sawa na kilo mita Themanini na tatu (83) takriban. Na iwe safari yake ni kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu au jambo la halali.
Na kupunguza Swala kunaisha kwa mtu kufika katika Nchi yake au Mji wake , au katika sehemu ambayo kuna mke wake ambae ameshamuingilia, au kwa nia ya kukaa siku Nne na zaidi. Na Swala zinazopunguzwa ni Swala zenye rakaa Nnne peke yake, ambazo ni Adhuhuri, Al Asiri, na Ishaa.
Na ALLAH ndie mjuzi zaidi
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.