SABABU MUHIMU ILIYOPELEKEA WAISLAMU KUMILIKI WATUMWA BAADA YA KUWATEKA VITANI.
Hii ni kutokana na kurudisha kisasi na itasaidia kwa waislamu kuwa na nguvu juu ya maadui zao. Pia itawapa uhuru mateka badala ya kuuawa wataachwa huru lakini wakiwa mateka na watumwa.
Lakini suala la mateka na utumwa litaangaliwa kama ifuatavyo:-
Endapo hao watu walioingia vitani kati yao na waislamu kama huwa wana tabia ya kuteka nao watatekwa bila ya kuachwa huru.
Kama huwa hawana tabia ya kuteka nao hawatatekwa.
Kama huwa wana tabia ya kuwafanya mateka watumwa nao watafanywa watumwa.
Na kama wakiwakamata mateka wanawauwa nao wakikamatwa mateka watauwawa.
Hebu jiulize?! : Mmarekani alipo mvamia Mjapan na akawapiga Wajapani kwa Kombora zito mwaka 1945 katika Mji wa Hiroshima. Je unadhani kama Wajapani nao wangekuwa na Kombora zito kama hilo waliliopigwa na Wamarekani unadhani Wajapani wasingerusha na wao Kombora hilo kuwapiga Wamarekani kwa kulipiza kisasi?. Jibu ni kwamba wangelipa kisasai tu.
Hapa ndio tunasema kwamba pale uislamu ulipo bakisha njia ya vita ndio njia pekee ya kupatia utumwa hii haimaanishi kuwa Uislamu unaendeleza utumwa na una upa nguvu bali Uislamu umeacha njia hii kwa ajili ya kulipiza kisasi.
Tena ukichukulia kipindi Uislamu unatangazwa hapo mwanzo kulikuwa na vita Vingi kati ya Waislamu na wasio kuwa Waislamu. Hivyo basi haingii akilini unapigana vita na watu wanaoteka wanajeshi wako na familia zako na watoto pia. Halafu wewe ukawa hauwateki wao hata kidogo.
Hivyo basi kwa hali kama hii tuliyoieleza ndio imefanya Uislamu ubakishe njia moja ya kuingia katika utumwa ambayo ni mateka wa kivita. Japokuwa ukiangalia utaratibu uliopo katika dini ya kiislamu katika kuwamiliki hao mateka utaelewa kwamba mateka waliotekwa na waislamu wanapewa haki zao za misingi zote za kibinadamu na kijamii, sio kama mateka waislamu wanapotekwa na maadui zao.
Soma katika aya hii Mwenyezi Mungu anaelezea Sifa za Waumini mingoni mwasifa hizo ni kuwalisha Mateka wakitaraji malipo kwa Allah.
وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا} الأنسان:8-9}
[Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.] [Al Insaan:8-9]
Maadui wa Waislamu wanapo wateka wanawake huwafanyia vitendo vya unyama kwa kuwabaka na kuwadhalilisha kijinsia.
Lakini kwa waislam endapo watatekwa wanawake watakaa chini ya utawala wakiwa ni wake za watu maalumu.
Endapo waislamu watakuwa hawachukui mateka kwa maadui zao, lakini maadui zao wakawa wanateka waislamu, basi jambo hilo litatia unyonge katika nyoyo za wapiganaji wa kiislamu na litapelekeka jeshi kushindwa nguvu na kufeli kabisa, ndipo Uislamu kwa kuchunga hayo yote ukaweka sheria ya kuwepo mateka na watumwa katika njia ya vitani tu.
Mtume ﷺ alipopigana vita na kabila la Banii-Mustaliq, na akateka wanawake zao. hii ni kwa sababu kabila hilo lilikuwa na tabia ya kuteka watu pale wanapopigana nao vita.
Lakini kuna vita nyingine Mtume alipigana na Maqurayish na hakuwateka hata kidogo, hii ni kwa sababu wao walikuwa hawana tabia ya kuchukua mateka wanapo pigana na maadui zao.
Hata hivyo ukitizama vyema aya hii tukufu ndipo utaelewa kuwa Uislam haukuamrisha watu wawe na watumwa, pia hakuna hadithi iliyo amrisha moja kwa moja kumiliki watumwa, hata wakati wa vita hauja amrisha moja kwa moja kwa kusema (Wafanyeni adui zenu watumwa).
Anasema allah mtukufu:
فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّى إِذَا أَثْخَنْتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّى تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا} محمد:4}
[Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe mpaka vita vitulie…”.] [Muhammad:4]
Ukitazama aya hii tukufu haija amrisha kuwepo watumwa hata kidogo japokuwa imeeleza kukaa na mateka kwa muda kisha kiongozi akitaka awachie huru au wajikomboe baada ya kumalizika vita, na wala aya haisemi mkiwateka basi moja kwa moja hao ni watumwa wenu.
Hapo ndipo utakapojua vyema kuwa Uislamu haukuunga mkono mwendelezo wa utumwa, bali umesapoti njia za watu kutokuwa watumwa, ingawa tabia ya utumwa ilikuwepo tangu na tangu kabla ya kuja Uislam alioueneza Mtume wetu Mohammad ﷺ.
Ukizingatia kuwa utumwa ilikuwa ni tatizo kuu la kijamii ambalo lilihitaji kulitatuliwa na kuondolewa katika jamii hadi liishe kabisa. Kwa kuwa tatizo hili liliota mizizi sana katika jamii mbalimbali lilihitaji ustaarabu wa hali ya juu katika kuliondosha kwa watu, na wala sio kukurupuka na kulikemea mara moja kwa nguvu moja tu, bali lilihitaji hatua kwa hatua.
Kwa mfano : Mwaka 1861 Rais wa Marekani Bwana ABRAHAM LINKULIN ambaye alikuwa Rais wa Nchi hiyo kuanzia mwaka 1861 hadi 1865. Mara tu baada ya kuwa Rais aliamuru kuwa watu wote nchi nzima wanao miliki watumwa wanatakiwa wawaachie huru, baada ya Rais ABRAHAM kutoa amri hiyo watu wote walitii na kuwaacha huru watumwa wote. Lakini cha kushangaza baada ya watumwa hao kuwa waendelee na mambo yao wamekuwa huru, walirudi kwa mabosi wao walokuwa watumwa kwao!
Sasa tujiulize ni kwanini warudi na wakati tayari walishaachwa huru??.
Jawabu:
Jambo la kwanza: lililo wafanya wao wenyewe waamue kurudi kwa mabosi wao na kutaka waendelee kuwa watumwa, ni kutokana na jamii ilikuwa ina wanyanyapaa. Kwa sababu jamii ilishazoea kuwaona wao wakiwa utumwani nabado haijapewa elimu ya kuwa ona wao nao ni watu wanaostahiki kuwa huru na kuishi na jamii.
Mfano: Hii ikumbukwe kuwa mwaka 1992 ulipoanza ugonjwa wa Ukimwi mkoani Kagera watu walikuwa wana wanyanyapaa wagonjwa hao wa UKIMWI hadi serikali ilipoanza kutoa eliku kwa jamii kuwa hawa ni watu kama sisi na wala ukiwa nao sio kwamba atakuambukiza ndipo jamii ikawakubali na ikaondoa unayanyapaa baada ya taaluma kutolewa.
Hivyo basi Rais wa Marekeni IBRAHAM yeye alitoa amri ya kuachwa huru watumwa wote mara moja kabla ya kuifundisha jamii iwaozee kuwa nao ni watu wanaostahiki uhuru kama wenzao.
Jambo la pili: lililo wafanya watumwa kurudi kwa mabosi wao baada ya Amri ya Rais ABRAHAM. Ni jambo la kisaikolojia na hali ya mazoea ya mazingira. Yaani watumwa wenyewe akili zao zilikuwa sio akili huru tena, ni akili ambazo zimekwisha athirika kuamrishwa kila siku, akili ambazo hazijazoea kupanga na kuamua mambo kutoka kwenye vichwa vyao.
Hivyo amri ilipotolewa na Rais IBRAHAM kuwa watumwa waachwe huru kipindi hicho ilikuwa akili zao hazikuandaliwa kitaaluma kwamba wajijue kuwa wao ni watu huru ambao wanaweza kufanya kazi kwa kuamua na kupanga wenyewe vichwani mwao.
Kwa hiyo hali halisi ikaonesha walipata uhuru wa mwili kabla ya uhuru wa akili na ndio maana walirudi tena kwa mabosi wao kuomba waendelee kuwa ni watumwa.
Hivyo basi ndio maana Uislamu kwa kutambua athari kama hizo hauku kurupuka tu kutoa katazo mara moja la kutomiliki watumwa, bali uliweka njia ambazo zitawatoa watu katika utumwa kidogo kidogo mpaka waishe kabisa.
Kama ulivyo fanya Uislamu katika kuikataza pombe kidogo kidogo hadi mwishowe kuiharamisha kabisa, na hii ni kwa sababu unywaji pombe ulikuwa ni kama kitu cha kawaida sana katika jamii ya waarabu, ilikuwa ni vigumu kuiharamisha mara moja kwa kauli moja tu ya (acheni kunywa pombe) bali hekima ikapelekea kukatazwa hatua kwa hatua.
Utumwa na haukukatazwa mara moja tu kwa kauli moja kwa sababu utumwa ulikuwa unatumika katika nchi nyingi kipindi hicho kama sehemu ya pato la nchi. Na pia ilikuwa ni biashara kuu ya mataifa ya Marekani ya sasa na Uingereza ya sasa na baadhi ya nchi zingine.
Hivyo ilikuwa ni muhali kwa dini ya kiislamu kutoa kauli moja ya kuacha utumwa jambo ambalo lisingewezekana kwa uharaka wa namna hiyo na ndio maana ukatoa njia za utaratibu zinazolimaliza tatizo hilo.
Kwa sababu ingetolewa kauli moja ingesababisha mporomoko mkubwa sana katika uchumi wa mataifa kwa kipindi hicho jambo ambalo madhara yake yange wagusa hadi wananchi wa hali ya chini kabisa kwa kipindi hicho na watu wengi wangepata hasara kwa siku moja tu. Na sio lengo la Uislam kuwapatisha watu hasara duniani.
Kwa sababau hizo tulizo zitaja hapo zinatufahamisha kwamba Uislam uliangalia mbali sana katika jambo zima la kuharamisha utumwa , badala yake zikawekwa kanuni mbalimbali zitakazoteketeza utumwa.
Uislamu pekee ndio umeweka njia na namna nzuri ya kutatua au kutibu tatizo sugu la utumwa. Na njia hizo ni
Njia za Kikanuni
Njia ya hatua kwa hatua
Njia ya Utu (Ubinadamu)
Na lengo kuu la kuwekwa njia hizi ni kupatikana binadamu huru kikamilifu kiakili, kimwili na kijamii.
Kiakili: Yaani akili yake ijitambue kuwe yeye ni mtu huru na ana uhuru wa kutoa maamuzi sahihi na kufanya kwa mujibu wa kile anachokiamua.
Kimwili: Yaani mwili wake pia uwe sehemu huru isije ikawa akili yake iko huru na mwili wake bado unatumikia utumwa.
Kijamii: Yaani jamii nayo ielewe kuwa maana ya mtu kuwa huru, ni kujikomboa utumwani na kuwa na maamuzi yake sahihi ya kiakili na kivitendo, na anahaki ya kushirikiana na jamii kama binadamu wengine. hivyo inakubali kwamba ni mtu huru katika mujitamaa.
MAKALA YAENDELEA
IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL
TAFSIRI:
BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.
NJIA ZA KUONDOA WATU UTUMWANI ZILIZOLETWA NA UISLAMU
Njia zilizoasisiwa na uislamu na kuziweka kuwa ni sheria za kuwatoa watu utumwani ni hizi zifuatazo ambazo ni:-
Mtu akila kiapo kwamba atafanya kitu fulani cha ibada kisha akawa ameacha kutekeleza kiapo chake hicho, basi sheria inamtaka atoe kafara, yaani kifutio cha dhambi yake ya kutotekeleza kiapo chake na kifutio hicho au (Kafara) hiyo ni : kumwacha huru mtumwa, ima awe ana mmiliki au akamnunue kwa mtu kisha amwacha huru.
لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ المائدة:8
Allah amtukufu anasema:
[Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru] [Al Maaida:89]
Mtu akimfanyia dhwihari, mkewe kwa kumwambia kuwa wewe ni kama mama yangu tu au dada yangu au shangazi yangu basi sheria inamtaka kwa kosa alilo lifanya ajitakase mbele ya Allah kwa kuacha huru mtumwa.
وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ} المجادلة:3}
Allah mtukufu anasema:
[Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda.] [Al Mujaadalah:3]
Mtu ambaye alikuwa amefunga faradhi ya Ramadhani akimwingilia mkewe mchana wa Ramadhani sheria inamtaka kwa kosa alilofanya ajitakase mbele ya Allah kwa kuacha huru mtumwa.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : هَلَكْتُ ، قَالَ : وَمَا أَهْلَكَك ؟ قَالَ : وَقَعْتُ عَلَى امْرَأَتِي فِي رَمَضَانَ ، قَالَ : أَعْتِقْ رَقَبَةً رواه مسلم
Kutoka kwa abuu hurayrah allah amridhie anasema: mtu mmoja alikuja kwa Mtume ﷺ akasema: ewe Mtume nimeangamia! Mtume akamuuliza : ni kipi kilichokuangamiza? Yule mtu akasema : mimemuingilia mke wangu mchana wa ramadhani!. Mtume akasema : “ acha huru mtumwa….” [Imepokewa na Muslim]
Mtu akimuwa mwislamu mwenzake kwa kukosea anatakiwa na sheria kujitakasa mbele ya Allah kwa kuacha huru mtumwa.
وَمَنْ قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ} النساء :92}
Allah mtukufu anasema:
[Na mwenye kuuwa muislamu kwa bahati mbaya , anatakiwa aache huru mtumwa muumini]. [Al Nnisaa:92]
Mtu ambae anataka kuokoka moto wa Allah na misuko suko ya siku ya mwisho sheria ina mwambia aache huru mtumwa.
عن أبي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ, قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : [ أَيُّمَا رَجُلٍ أَعْتَقَ امْرَأً مُسْلِمًا اسْتَنْقَذَ اللَّهُ بِكُلِّ عُضْوٍ مِنْهُ عُضْوًا مِنْهُ مِنْ النَّارِ.] متفق عليه
Kutoka kwa abii hurairah allah amridhie anasema: Amesema Mtume Muhammad ﷺ:[Mtu yeyote akiacha huru mtumwa muislamu, allah atamuokoa mtu huyo kutokana na moto kwa kila kiungo cha mtumwa Yule] [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
Mtu akipenda moyoni mwake kumwacha huru mtumwa akifanya hivyo pia ina kubalika na njia hii tu ndio iliyokuwa ikitumika kabla ya uislamu na baada ya kuja uislamu nao umekubali na njia hii.
Mtu anae miliki mtumwa akimpiga na kumumiza sheria ya kiislamu inamlazimisha mtu huyo kumwacha huru mtumwa huyo. Hizi njia zote ndizo zinazotumika kupoteza utumwa duniani na kuuteketeza kabisa.
Na njia ya nane ni mtu aliye miliki mtumwa wa kike sheria ina mruhusu kumwingilia ili akipatikana mtoto atakuwa ni mtoto huru na ataweza baadae kumwokoa mama yake katika utumwa.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه – قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ – صلى الله عليه وسلم – – ” لَا يَجْزِي وَلَدٌ وَالِدَهُ, إِلَّا أَنْ يَجِدَهُ مَمْلُوكًا فَيُعْتِقَهُ” – رَوَاهُ مُسْلِم ٌ
Kutoka kwa abuu hurayrah allah amridhie anasema: amesema Mtume Muhammad ﷺ : [Mtoto hawezi mlipa fadhila mzazi wake ispokuwa atakapomkuta kuwa ni mtumwa na akamkomboa kutokana na utumwa] [Imepokewa na Muslim].
JE UISLAMU UNAUNGA MKONO UTUMWA AMA UNAPINGA UTUMWA?
Jibu ni kwamba uislam pekee inayopinga vikali jambo la utumwa na watumwa kwa sababu nyingi tulizoziona ukilinganisha na tabia zilizokuwapo kabla ya uislamu, watu walikuwa na njia nyingi za kuingia utumwani na walikuwa hawana namna mbadala ya kutoka utumwani isipokuwa moja tu. Nayo ni kuridhia yule mtu anae miliki mtumwa na akaamua kumwacha huru mtumwa wake.
Lakini Uislam kwa kuunga kwake mkono suala la kuachwa huru watumwa ukatoa njia nane za kutoka utumwani na kuwa huru, na ukabakisha njia moja ya dharura ya kuingia watu utumwani kwa maslahi ya wapiganaji wa kiislamu, pia kwa maslahi ya mateka.
Na njia hiyo ni: watumwa wanaotokana na mateka wa kivita kati ya waislamu na wasiokuwa waislamu, vita ambayo itatangazwa na Kiongozi Mkuu wa Waislamu (Amiri Utawala) na ndie Amiri Jeshi Mkuu wa Waislamu.
Endapo akaona kulingana na hali halisi ilivyo wakati huo kwamba kuna umuhimu wa vita kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu kupigana, basi watu watakao tekwa katika vita hivyo watakuwa ni watumwa ni sawa mateka hao wawe wanawake au wanaume.
MAKALA YAENDELEA
IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL
TAFSIRI:
BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.
UONGOZI DHALIMU
KUZALIWA KWA MUSA (Alayhi salaam)
kuzaa au kuzaliwa nijambo lakawaida kwa binadamu wanyama na hata miti. Issa (Alayhi salaam) utukufu wake ulianza kwa jinsi mamake alivyopata mimba soma Qur'ani:
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا مريم:16-21
[Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki.Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.(Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.] [Maryam:16-21]
na haya ndio yamewachanganya wenzetu wanaoona yesu ( ISSA Alayhi salaam) ni Mungu kwa kuwa hakuzawa kawaida.
Ama kwa Musa (Alayhi Salaam) utukufu wa mazazi yake yalianza kwa wahyi alopewa mamake musa wa kuwa na plan (A) myonyeshe soma Qur'ani suratul Qaswas Aya 7
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ } قصص:7}
[Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe.]
plan (B) mrushe kwa bahari ukiogopa soma Qur'ani:
{فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ}
Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.]
hapa kwa plan (B) mrushe au muweke kwa bahari ndio ushindi na utukufu wa musa juu ya udhalimu waanza.
Mazazi ya musa yafungamana na bahari na yaashiria uongozi Dhalimu utaangamizwa na bahari ,kama inavyoashiria kuwa musa alipofikiwa kuangamizwa akiwa na miezi mitatu Allah alitumia bahari kumnusuru na alipokuwa akimbia ataka angamizwa akiwa mtu mzima Allah pia alitumia bahari kumnusuru, na kwa utawala wake alitumia bahari kuangamiza upotofu wa Firaauni.Kwa maana kama kwamba plan (B) ambao ilikuwa bahari inaashiria makubwa kwa Musa Alayhi salaam kuanza kuzaliwa.
Musa bin imraan yashikana nasaba yake na yaakub (Alayhi salaam) , na asli ya musa kuzaliwa misri ni natija ya maonevu na uhasidi walofanya nduguze Yussuf Alayhi salaam. kwa Yusuf walipomtupa kwa kisimani kisha kusingizia kuliwa na mbwa mwitu soma Qur'ani suratu Yusuf aya ya 17
قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ
[Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli.]
alafu kuokotwa na msafara kutoka misri na kuuzwa kama mtumwa kwa mtukufu wa misri (wengine waona ni mfalme) kama kinavyo julikana kisa cha Yusuf Alayhi salaam.
MAFUNGAMANO YA YUSSUF NA MUSA (A.S)
1) Yussuf alitupwa kwa kisima alipokuwa kijibarobaro kwa malengo yakuangamizwa na nduguze wawe bora na kupendeza kwa baba yao, Musa alitupwa kwa bahari kwa malengo ya kumkimbiza kuchinjwa na jeshi la firaaun
2) mke wa firauun matarajio yake yalikuwa huenda Musa Alayhi Salaam atawafaa au wamfanye mtoto wamlee, Ama kwa Yussuf mtukufu wa misri ndie alimnumua yussuf na kumpelekea mkewe kwa malengo yale yale ya mke wa firaaun.
MAFUNZO KATIKA KISA CHA KUZALIWA MUSA ALAYHI SALAAM
1)Musa ambae alizaliwa huku uoga na hadhari umetanda nyumba na familia yake kwa kuwa akijulikana atachinjwa Allah alimpangia aishi kwa Qasri ya ufalme ili apate malezi yakutoogopa na kujuana na wengi ambao wako kwa utawala wa misri pamoja na kujua siri ya serekali dhalimu.
2)Musa kuwa kwa Qasri ya utawala kuanzia udogoni mwake ilimpatia nguvu na uwezo wa kupambana na dhulma kwa sababu malezi ya banii israeel yalikuwa yaunyonge na kunyanyaswa na uongozi wahitaji malezi yakujiamini zaidi , haya hayangepatikana nyumbani kwao.
3) maskini na wanyonge hawafai kujidharau Musa aliandawa kukomboa banuu israeel wakati watu wake wamekata tamaa hata ya uhai wake , hivyo ndivyo alivyokuwa Yussuf A.S utukufu ulikuja baada ya dhiki na mitihani mikubwa na hata kufungwa jela .
Dr.Majid Hobeni
College of islamic studies mombasa
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA UTUMWA.
MAANA YA UTUMWA NA UHURU
Kwanza tujifunze ufafanuzi kuhusu neno utumwa na uhuru, nini tofauti yake.
Maana halisi ya neno “UTUMWA” ni: “Kumilikiwa na mtu jumla na kutokuwa na uhuru wa kujiendesha kwa maamuzi yako, yaani kuwa chini ya miliki ya mtu jumla jumla”.
Na neno “UHURU” ni : “ Kuwa huru katika maamuzi na kutokumilikiwa na mtu”.
Ama neno “UHURU” kwa mujibu wa uislamu ni : “Kitendo cha mtu kuitakasa shingo yake na kuitoa katika utumwa na kuwa mtu huru anaejimiliki mwenyewe”.
Na suala zima la mtu kuwa huru au kuachwa huru ni jambo ambalo limetolewa maelekezo katika Kitabu na Sunna na makubaliano ya Wanachuoni
Ama katika Kitabu cha Allah amesema:
فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ } النساء 92}
[Ni kuacha huru shingo ya mtu Muumini] 4/92.
Na hadithi zinazo elezea umuhimu wa kuacha huru mtu ni nyingi sana miongoni mwa hadithi hizo ni :
عن أبي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ, قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : [ أَيُّمَا رَجُلٍ أَعْتَقَ امْرَأً مُسْلِمًا اسْتَنْقَذَ اللَّهُ بِكُلِّ عُضْوٍ مِنْهُ عُضْوًا مِنْهُ مِنْ النَّارِ] رواه البخاري
Kutoka kwa abii hurairah allah amridhie anasema: amesema mtume Muhammad rehema na amani zimfikie: [Mtu yeyote akiacha huru mtumwa muislamu, allah atamuokoa mtu huyo kutokana na moto kwa kila kiungo cha mtumwa Yule]. [Imepokewa na Bukhari].
pia wanachuoni wa kiislamu wamekubaliana kuwa mtu akilimiliki mtumwa anatakiwa amuache huru.
Na miongoni mwa wanachuoni wa kiislamu walioandika katika vitabu vyao umuhimu wa jambo hili ni mwanachuoni aitwaye Ibn Hajar. Ambae ameandika katika kitabu chake bubughul-marami somo maalumu linaloelezea umuhimu wa mtu kuwa huru tena somo hili ameliweka mwishoni mwa kitabu chake kwa matarajio ya kutaka Allah amwache huru kutokana na moto.
Kama ambavyo kuna baadhi ya wanachuoni wengine wa kiislamu wanafanya hivyo katika vitabu vyao na waka taja somo hili baada tu ya kuelezea mambo ya mirathi kwa sababu mtu akimwacha huru Mtumwa sheria inampa cheo cha uwalii wa kumrithi huyo aliye mwacha huru kama atakuwa hana watu wa kurithi mali zake katika wanae au jamaa zake wanaostahiki kisheria kumrithi.
Hivyo kila mwanachuoni huandika kitabu chake na kuweka somo moja baada ya jingine kwa kuchunga vitu maalumu anavyoviona katika taaluma yake.
Tunamwomba Allah atuache huru sisi pamoja na wao kutokana na moto wa Jahanam.
SABABU ZINAZOPELEKEA KUMILIKI MTUMWA KATIKA DINI YA KIISLAMU
Sababu za kumiliki Mtumwa katika Dini ya Kiislamu ni mbili tu:
Sababu ya kwanza: Ni mtu kuwa kafiri au (Ukafiri), Yaani endapo pata tokea vita kati ya waislamu na wasiokuwa waislamu na wakafanikiwa waislamu kuwashinda maadui zao na waka wateka wapiganaji na familia zao na wake zao, basi hizi familia na hawa wanawake wote wanakuwa ni watumwa papo hapo kwa kitendo cha kutekwa kwao.
Hivyo mwanzo walikuwa ni watu huru ila baada tu ya kutekwa kwa sababu ya vita ya kisheria ya jihadi wakawa ni watumwa wenye kumilikiwa na waislamu.
Sababu ya pili ya utumwa: Ni matokeo ya kupitia chimbuko la utumwa, yaani endapo kijakazi atakuwa na mmiliki halisi kisha akaja mwanamume mwingine akamuoa mwanamke huyo mtumwa basi inakuwa kila mtoto anaezaliwa na mwanamke huyu anakuwa nae ni mtumwa.
Lakini kama mwanamke huyo mtumwa atazaa na mmiliki wake halisi aliye mnunua au aliyepewa na kiongozi wa kiislamu baada ya kupatikana mateka hao, basi mtoto atakaye zaliwa anakuwa ni mtu huru na sio mtumwa na kwa sababu hii Allah mtukufu amewakataza wanaume wa kiislamu kuwaowa wanawake watumwa ili kutozidisha jamii nyingi ya utumwa, ila tu ameruhusiwa kwa dharura maalumu mtu kuowa mtumwa kama ataogopea kuingia katika uzinifu na pia hana mahari ya kuweza kuowa mwanamke huru.
25 :ذَلِكَ لِمَنْ خَشِيَ الْعَنَتَ مِنْكُمْ} النساء }
[hilo (la kuowa mwanamke mtumwa) ni kwa yule tu anae hofia kuingia katika uzinifu] [Al Nnisaa:25]
JE UISLAMU NDIYO ULIOTESHA MIZIZI YA UTUMWA NA WATUMWA NA HAUJAKATA AU LAA?
Wanasema baadhi ya watu wa nchi za magharibi kutokana na chuki zao juu ya uislamu kwamba uislamu ndio dini inayo endeleza utumwa na imeruhusu kuendelea kuwepo utumwa na umeamrisha kueneza utumwa ulimwenguni.
Tena umehalalisha kwa waislamu kuwafanya wanawake kuwa ni watumwa. Na umelikubali hilo bila ya kuogopa, na umewadhalilisha mateka wa kivita wanawake. Kwa kitendo cha kuruhusu kwamba anaweza mtu mwanaume mmoja kukaa na wanawake hao zaidi ya wanne bila ya ukomo maalumu tena bila ya idadi maalumu kinyume na wanawake huru uislamu umemruhusu mwanamme wa kiislamu kutozidisha zaidi ya wanawake wanne.
Kabla ya kujibu tujiulize kwanza swali hili muhimu sana. Je uislamu ndio chanzo cha utumwa au laa, Yaani je uislamu ndio umeanzisha utumwa au utumwa ulikuwapo hata kabla ya mtume Muhammad kutangaza uislamu?
Jawabu ni kwamba: Utumwa ulikuwepo kablaya uislamu huu alioshushiwa mtume wetu Mohammadi rahma na amani za allah zimfikie , yaani mtume amepewa utume amekuta utumwa upo tayari duniani.
Hivyo basi uislamu sio chanzo cha utumwa, bali uislamu umekuja umekuta tayari utumwa upo. Pia uislamu hauja anzisha njia za utumwa bali uislamu
umeanzisha njia nyingi za kuachwa huru mtumwa.
Kama tulivyosema kwamba uislamu umekuja hali ya kuwa tayari utumwa upo na vyanzo vya utumwa ni vingi yaani njia za watu kuwa watumwa zilikuwa nyingi na rahisi sana. Na njia za mtu kutoka kwenye utumwa na kuwa huru ni chache yaani havizidi moja nayo ni Yule mmiliki mtumwa akubali tu kwa ridhaa yake kumwacha huru mtumwa wake.
Lakini uislamu ulipo fika ukaziba njia zote za kuzalisha watumwa na ukafungua njia nyingi sana za kuwaacha huru watumwa, hali ambayo kipindi cha nyuma kabla ya uislamu kulikuwa na njia moja tu ya kumtoa mtu katika utumwa kama tutakavyoona katika somo letu hili .
VYANZO VYA UTUMWA KABLA YA UISLAMU:
Vyanzo vya kuwaingiza watu katika utumwa kabla ya kuja uislamu ni hivi vifuatavyo:-
1. Mtu kuwa mateka katika vita anakuwa tayari ni mtumwa.
2. Kabila moja likivamiwa na jingine likashindwa nguvu tayari linakuwa kabila lote ni watumwa wa kabila lililowashinda, utumwa huo utaendelea vizazi na vizazi vyao
3. Mtu akifanya dhambi na akataka kutubia anakwenda kwa kiongozi wa jamii hiyo, ima awe kiongozi wa kimila au kiongozi wa kidini, ili atubie dhambi zake na anajitakasa kwa kuwa mtumwa wa kiongozi huyo.
4. Mzazi akisumbuliwa na mwanae na akakasirika anampa mtu mwingine mtoto huyo kwa njia ya utumwa.
5. Mtu akiwa anadaiwa na akashindwa kulipa deni, mwenye kudai anammiliki na kuwa mtumwa wake baada kushindwa kulipa deni.
6. Mtu kutekwa akiwa katika safari zake, akizidiwa nguvu anakuwa mtumwa wa huyo alomteka, kama ilivowahi kutokea kwa swahaba mtukufu zaidu bun haarithah radhi za allah ziwe juu yake.
7. Utumwa wa kurithi kutoka kwa wazazi.
8. Mtu kufanya kosa kwa mtu na kuambiwa ili ni kusamehe lazima uwe mtumwa wangu ndio nakusamehe akubali anakuwa mtumwa.
9. Mtu kuiuza nafsi yake kwa sababu ya uamsikini (ufakiri) au hali ngumu ya maisha wake kwa kusema nipe chakula nile na unifanya mtumwa wako.
10. Mtu kumuuza mwanae kwa sababu ya hali ngumu ya maisha ili akidhi mahitaji yake ya lazima.
Hivyo basi hizi zote tulizo zitaja hapo nyuma ndizo sababu na njia za kumiliki watumwa kabla ya kuja uislamu.
Na ili mtu atoke kwenye utumwa ni hadi yule anae mmiliki amwache huru tu. Na wala hakukuwa na njia zingine za kumtoa mtu katika utumwa hivyo kila siku hadi siku watu walikuwa wanazidi kuwa wengi utumwani.
Hivyo basi baada tu ya kuja uislamu ukaasisi njia nyingi za kutoa watu utumwani na ukawa umebakisha njia moja tu ya utumwa ambayo inatokana na vita kati ya waislamu na wasio kuwa waislamu. Hivyo wale waliotekwa wanakuwa ni mateka na pia ni watumwa.
MAKALA YAENDELEA
IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL
TAFSIRI:
BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.
UONGOZI
Nidhamira ya uandishi huu kuangazia suala la uongozi ambalo ni sehemu muhimu katika maisha ya binadamu na hata viumbe vengine.
Uongozi dufu au mbaya ni chanzo cha upotofu wa dini,Dunia na Akhera pia.
Tutachukua kiegezo kwa MUSA (Alayhi salam) kwa sababu ni mmoja katika mitume walotumwa kupambana na udhalimu, unyanyasaji, maonevu na ubaguzi.
MUSA
Musa ibnu Imran mjukuu wa mtume Yaakub (Alayhi salam) alizaliwa Misri wakati wa Firaaun dhalimu ambaye alijulikana kwa maonevu dhulma mauaji, ubaguzi na dhulma nyingi nyingine. Soma Quran Qaswas Aya (4).Mwenyezi Mungu anasema:
{إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ}
[Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.]
Musa alijulikana kwa nguvu zake za kimwili na ukaribu wake kwa Allah kwa kuzungumza na Allah mpaka kuomba kutaka kumuona Allah. Soma Quran. Suratul A'raaf Aya (143)
{وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَن تَرَانِي وَلَٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي}
[Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona].
Tutaangazia kwa Mada hii ya Musa na uongozi dhalimu vipengee vifuatavyo.
(1) kuzaliwa kwa Musa (A.S)
(2) Bahari
(3) kunyonyesha
(4) kahama kwa musa
(5) kuowa kwa musa
(6) Musa akiwa Madyan
(7) Kuajiriwa kwa musa
(8) Musa kurudi Misri
(9) Musa Kupewa Risala (UTUME ) njiani
Kufikia hapa tutakuwa tumejaribu kueleza maisha ya mwanzo ya Musa (A.S) na mafunzo alopata kupambana na udhalimu na uongozi mbaya.
Kifungu cha pili tutaangazia
(10) Musa kukumbushwa alivyofadhiliwa au kulelewa na Firaaun
(11) Banuu Israel Misri
(12) Uchoyo /au kujipenda zaidi
(13) Kutafuta mustaqbal mzuri
(14) Kujifunza kwa khidri
(15) Musa /wachawi
(16) Siku ya idd
(17) Musa kuomba apewe nduguye amsaidie.
(18) Vishawishi au visaidizi alokuwa nazo musa
(19) Utawala / utajiri
(20) Hasira ya Firaaun
(21) Kukimbia kwa Musa
(22) Bahari mara ya pili
(23) Kuangamizwa udhalimu
Kufikia hapa tutakuwa tumejaribu kuangazia mapambano ya musa na Utawala mbaya au uongozi dhalimu, tutaanza kuangazia Utawala wa Musa (A.S)
(24) Watu wa musa na mazowea ya upotofu
(25) Tabia yakupenda mali (Qaruun)
(26) Musa kuenda kuonana na Allah ( kuzungumza )
(27) Samiriyu - Upotofu kwa Utawala wa Musa
(28) Haroun kuogopa Fitna
(29) Kijigombe - Mungu mpya kwa Utawala wa musa (upotofu)
(30) Musa kupewa sheria ya serekali yake
(31) Hasira Takatifu
(32) Kujitetea
(34) Vita juu ya upotofu wa samiriyu
(35) Vita juu ya utukufu wa Utajiri (Qaruun)
(36) Musa na Ardhi takatifu
(37) kufa kwa Haroun
(38) kufa kwa Musa
(39) Mafunzo (1)
(40) Mazingatio/ Mwisho
Imeandikwa na Dr.Majid Hobeni
Deputy principal College of Islamic studies mombasa
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.