NJIA ZA KUONDOA WATU UTUMWANI ZILIZOLETWA NA UISLAMU
Njia zilizoasisiwa na uislamu na kuziweka kuwa ni sheria za kuwatoa watu utumwani ni hizi zifuatazo ambazo ni:-
Mtu akila kiapo kwamba atafanya kitu fulani cha ibada kisha akawa ameacha kutekeleza kiapo chake hicho, basi sheria inamtaka atoe kafara, yaani kifutio cha dhambi yake ya kutotekeleza kiapo chake na kifutio hicho au (Kafara) hiyo ni : kumwacha huru mtumwa, ima awe ana mmiliki au akamnunue kwa mtu kisha amwacha huru.
لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ المائدة:8
Allah amtukufu anasema:
[Mwenyezi Mungu hatakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakushikeni kwa mnavyo apa kweli kweli kwa makusudio. Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu. Hii ndiyo kafara ya viapo vyenu mnapo apa. Na hifadhini yamini zenu. Namna hivyo Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake ili mpate kushukuru] [Al Maaida:89]
Mtu akimfanyia dhwihari, mkewe kwa kumwambia kuwa wewe ni kama mama yangu tu au dada yangu au shangazi yangu basi sheria inamtaka kwa kosa alilo lifanya ajitakase mbele ya Allah kwa kuacha huru mtumwa.
وَالَّذِينَ يُظَاهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ۚ ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ ۚ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ} المجادلة:3}
Allah mtukufu anasema:
[Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda.] [Al Mujaadalah:3]
Mtu ambaye alikuwa amefunga faradhi ya Ramadhani akimwingilia mkewe mchana wa Ramadhani sheria inamtaka kwa kosa alilofanya ajitakase mbele ya Allah kwa kuacha huru mtumwa.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : هَلَكْتُ ، قَالَ : وَمَا أَهْلَكَك ؟ قَالَ : وَقَعْتُ عَلَى امْرَأَتِي فِي رَمَضَانَ ، قَالَ : أَعْتِقْ رَقَبَةً رواه مسلم
Kutoka kwa abuu hurayrah allah amridhie anasema: mtu mmoja alikuja kwa Mtume ﷺ akasema: ewe Mtume nimeangamia! Mtume akamuuliza : ni kipi kilichokuangamiza? Yule mtu akasema : mimemuingilia mke wangu mchana wa ramadhani!. Mtume akasema : “ acha huru mtumwa….” [Imepokewa na Muslim]
Mtu akimuwa mwislamu mwenzake kwa kukosea anatakiwa na sheria kujitakasa mbele ya Allah kwa kuacha huru mtumwa.
وَمَنْ قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ} النساء :92}
Allah mtukufu anasema:
[Na mwenye kuuwa muislamu kwa bahati mbaya , anatakiwa aache huru mtumwa muumini]. [Al Nnisaa:92]
Mtu ambae anataka kuokoka moto wa Allah na misuko suko ya siku ya mwisho sheria ina mwambia aache huru mtumwa.
عن أبي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ, قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : [ أَيُّمَا رَجُلٍ أَعْتَقَ امْرَأً مُسْلِمًا اسْتَنْقَذَ اللَّهُ بِكُلِّ عُضْوٍ مِنْهُ عُضْوًا مِنْهُ مِنْ النَّارِ.] متفق عليه
Kutoka kwa abii hurairah allah amridhie anasema: Amesema Mtume Muhammad ﷺ:[Mtu yeyote akiacha huru mtumwa muislamu, allah atamuokoa mtu huyo kutokana na moto kwa kila kiungo cha mtumwa Yule] [Imepokewa na Bukhari na Muslim].
Mtu akipenda moyoni mwake kumwacha huru mtumwa akifanya hivyo pia ina kubalika na njia hii tu ndio iliyokuwa ikitumika kabla ya uislamu na baada ya kuja uislamu nao umekubali na njia hii.
Mtu anae miliki mtumwa akimpiga na kumumiza sheria ya kiislamu inamlazimisha mtu huyo kumwacha huru mtumwa huyo. Hizi njia zote ndizo zinazotumika kupoteza utumwa duniani na kuuteketeza kabisa.
Na njia ya nane ni mtu aliye miliki mtumwa wa kike sheria ina mruhusu kumwingilia ili akipatikana mtoto atakuwa ni mtoto huru na ataweza baadae kumwokoa mama yake katika utumwa.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه – قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ – صلى الله عليه وسلم – – ” لَا يَجْزِي وَلَدٌ وَالِدَهُ, إِلَّا أَنْ يَجِدَهُ مَمْلُوكًا فَيُعْتِقَهُ” – رَوَاهُ مُسْلِم ٌ
Kutoka kwa abuu hurayrah allah amridhie anasema: amesema Mtume Muhammad ﷺ : [Mtoto hawezi mlipa fadhila mzazi wake ispokuwa atakapomkuta kuwa ni mtumwa na akamkomboa kutokana na utumwa] [Imepokewa na Muslim].
JE UISLAMU UNAUNGA MKONO UTUMWA AMA UNAPINGA UTUMWA?
Jibu ni kwamba uislam pekee inayopinga vikali jambo la utumwa na watumwa kwa sababu nyingi tulizoziona ukilinganisha na tabia zilizokuwapo kabla ya uislamu, watu walikuwa na njia nyingi za kuingia utumwani na walikuwa hawana namna mbadala ya kutoka utumwani isipokuwa moja tu. Nayo ni kuridhia yule mtu anae miliki mtumwa na akaamua kumwacha huru mtumwa wake.
Lakini Uislam kwa kuunga kwake mkono suala la kuachwa huru watumwa ukatoa njia nane za kutoka utumwani na kuwa huru, na ukabakisha njia moja ya dharura ya kuingia watu utumwani kwa maslahi ya wapiganaji wa kiislamu, pia kwa maslahi ya mateka.
Na njia hiyo ni: watumwa wanaotokana na mateka wa kivita kati ya waislamu na wasiokuwa waislamu, vita ambayo itatangazwa na Kiongozi Mkuu wa Waislamu (Amiri Utawala) na ndie Amiri Jeshi Mkuu wa Waislamu.
Endapo akaona kulingana na hali halisi ilivyo wakati huo kwamba kuna umuhimu wa vita kati ya Waislamu na wasiokuwa Waislamu kupigana, basi watu watakao tekwa katika vita hivyo watakuwa ni watumwa ni sawa mateka hao wawe wanawake au wanaume.
MAKALA YAENDELEA
IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL
TAFSIRI:
BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.