Menu

NI NINI UISLAMU?


WHAT


Uislamu ni dini ya mwisho ambayo amekuja nayo bwana Mtume Muhammad S.A.W na Uislamu umekuja kukamilisha sheria zote zilizopita. Na uislamu ni dini ya Mitume wote kwanzia Adam mpaka Mtume Muhammad .
Uislamu ni kunyenyekea na kujisalimisha kwa mungu na kumuabudu Mungu mmoja mwenye Nguvu alie Mbinguni.

MWENYEZI MUNGU NI NANI ?

Mungu au ALLAH ndie Mungu mmoja alieumba kila kitu na ndie anaeendesha kila kitu katika ulimwengu ni mungu mmoja anaejitegemea mwenye nguvu hakuzaa wala hakuzaliwa wala hafanani na kitu chochote wala haonekani kwa utukufu wake.

Mwenyzi Mungu anasema katika Qur'ani Tukufu Sura 112 Aya 1-4

[Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.Mwenyezi Mungu MkusudiwaHakuzaa wala hakuzaliwaWala hana anaye fanana naye hata mmoja.]


UISLAMU UNAFUNDISHA NINI?

Uislamu unafundisha kumuabudu mungu mmoja na kuacha kuabudu Masanamu na vitu vingine , Uislamu unafundisha Tabia njema, kuishi na Majirani vizuri, kuwatendea wema  wawili, na kuwafanyia wema watu wote hata wasiokua Waislamu imekuja katika Qur'ani Mwenyezi anasema:

[Hawakatazi Mwenyezi Mungu kwa wale wasiowapiga vita katika dini yenu na hawajawatoa katika majumba yenu kuwafanyia wema na kuwafanyia uadilifu hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kufanya uadilifu].   [60:8]

YESU NI NANI KWA WAISLAMU?

Yesu ama Nabii (Issa) ni binadamu kama binadamu wengine na ni Mtume katika Mitume wa Mwenyezi Mungu wala sio mungu wala mwana wa mungu na kuzaliwa kwake bila ya baba ilikua ni Miujiza katika miujiza ya mungu kwani yesu ni kama Nabii (Adam) ambae aliumbwa bila ya Baba wala Mama.

[Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa]     [3:59]

Na Nabii Issa au yesu kama Manabii wengine alipewa Miujiza ya kufufua maiti na kuwaponya wagonjwa sio kwa uwezo wake bali ni kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho atawakana wanaomuabudu na sisi Waislamu tunaamini yakwamba yesu hakuuwawa wala hakusulubiwa bali alipaishwa Mbinguni kwa mwenyezi Mungu,na atashuka mwisho wa Dunia na kufariki.

[Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.]  [4:157-158]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6785496
TodayToday497
Highest 07-17-2025 : 4917
US
Guests 33

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_68a98c24b0cf42966647381755941924
title_68a98c24b0de01300998931755941924
title_68a98c24b0ec4228282541755941924

NISHATI ZA OFISI

title_68a98c24b24f94856172211755941924
title_68a98c24b25ec20744091491755941924
title_68a98c24b26b89955552381755941924 Add content here

HUDUMA MPYA

: 14 + 7 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com