Menu

Sehemu ya Yautangazaji


SASA NIMEFAHAMU!!


  maxresdefault 1


Wengi huniuliza (SASA NIMEFAHAMU!!) umefahamu nini ?? Na wamanisha nini? na wapo walio tafsiri wanavyo taka wao walivyo dhania bila kuniuliza nilicho kikusudia.
Kwa wanao taka kujua nilicho kikusudia katika msamiati huu (SASA NIMEFAHAMU) nawambia hivi:
Nimefahamu mengi nilio kua siyajui na ata niliokua nayajua, tena SASA wala sio leo kumanisha ni jambo ninalo endelea nalo paka mwisho wa maisha yangu, sababu inawezekana nilio wambia kua nimefahamu ikawa bado sijafahamu lakini sina khofu kwakua nasoma nafanya utafiti nafikiria nauliza na mwanadamu heshi kusoma hivyo basi daima anatakiwa kufahamu kila anacho kisoma, na hapo nitakapo fahamu lolote lile wakati huo pia nitawambia yakua SASA NIMEFAHAMU, kufahamu ndilo lengo kuu kwa tunayo soma na kujifunza, na ndipo nikaufanya msemo hu SASA NIMEFAHAMU kua ni project yangu katika kuleta mabadiliko ya kifikra katika jamii na kusahihisha baadhi ya mambo yanao hitajia kusahihishwa na kufahamika katika imani, ibada, akhlaq, matangamano, Dunia na mengineo. Na nimeandaa programmes tofauti chini ya msamiati huu, 
Kufahamu ndilo lengo kuu la yoyote anae taka kujua, na mjuzi alie fahamu, Hawi sawa na asie fahamu, japo wote wamesoma sababu wa kwanza kafikia lengo, na wapili hakufikia.

Mwenyezi Mungu s.w  ameiteremsha hii Qur'ani ili watu waizingatie Aya zake na wapate kuwaidhika wenye akili kama alivyo sema:

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ}    ص:29}

[Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.]       [Swaad:29]

Na Mwenyezi Mungu ameashira katika aya nyingi kuhusu jambo hili lakufiri na kutafakari Aya za Qur'ani, ama Visa vilivyo simuliwa ndani ya Qur'ani, mfano wa aya hizi:

فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ}  الأعراف:176}

[Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.]     [Al-A'araaf:176]

كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ}    يونس:24}

[Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.]    [Yunus:24]

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ}  الرعد:3}

[Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.]    [Ar raa'd:3]

وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ}  النحل:44}

[Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.]     [An Nah'l:44]

Hizi ni baadhi za aya zilizo kuja katika kutuhimiza kufikiri,na Aya zilizokuja kinamna hii ni Aya nyingi.

Inatakiwa mwenye kuisoma Qur'ani awe ni mwenye kuzingatia na kutafakari aya zake wala sio kusoma tu bila ya kuzigatia japo kuwa ni mwenye kupata thawabu.

Hii Qur'ani yataka izingatiwe na wenye akili busara na wenye kufikiria, kumanisha wasio tumia akili zao hawataeza kufahamu, hatimae hawezi kua na uwamuzi wowote zaidi ya kufwata yalio fahamika na wengine bila kujali hali au zama au mazingira ya hao walio fahamu wakati huo,kwa namna nyengine twaeza sema wasio fahamu hawaezi jitahidi wakapata hukumu inayo endana na zama wanazo ishi, sababu wamezoea kuiga kusema yalio Semwa na kufwata yalio fwatwa bila kuzingatia zama wanazo ishi. Huo ni upeo wa kufungika Akili na watu aina hiyo mara nyingi hudhuru jamii kuliko kunufaisha ata iwapo wanashiriwa kua wamesoma lakini hawakufahamu.

Asema Mtume :

مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ]   رواه البخاري ومسلم]

[Mwenyezi Mungu s.w anapo mtakia mja kheri humpa ufahamu wa dini.]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Tuna haja sana leo kueza kufahamu Uislamu wetu kama mfumo kamili wa Maisha yetu katika nyaja zote ndipo tue mfano duniani kama watu wenye Katiba ilio kamilika Mzuri inayo muitikia Mwanadamu juu ya mahitajio yote bila yakua ni yenye kumnyima baadhi yanaoendana na maumbile, endapo tutafahamu UISLAMU wetu ipasavyo hapo tutaweza kuongoza Ulimwengu nakua mfano bora zaidi sababu ndio Mfumo wa Mwenyeezimungu (s.w) wa haki.

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّهِ الْإِسْلَامُ}    آل عمران:19}

[Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.]     [Al-Imraan:19]

Sasa nimefahamu.


Imeandikwa na Sheikh Yusuf Abdi

Mombasa-Kenya


UKATI NAKATI KATIKA QUR'ANI NA SUNNA


 مظاهر الوسطية في الإسلام


Makusudio ya Ukati na kati ni mfumo na njia ya kufuata Qur’an na Sunna za Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam bila ya kuzidisha au kupunguza. Na huo ndio mfumo wa Mtume na Masahaba zake na watu wema walio tangulia. Dini ya Kiislamu imekamilika, hakuna mtu ambae atakuja baada ya Mtume na kudai ana mambo ya ziada katika dini. Na vile vile, hakuna mtu ambae atadai ya upungufu wa Dini. Njia zote mbili hazikubaliki, kwasababu, Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

 

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا}    المائدة:3}

 

[Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. ]   [Al-Maaida:3]
Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

 

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ}     الحجر:9}

 

[Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.]     [Al-Hijr:9]
Kwa hivyo, Mfumo na Manhaj ya dini ya Kiislamu ni moja nayo ni kufuata Qur’an na Sunna bila ya ziada wala kupunguza.

 

UKATI NAKATI KATIKA QUR'ANI

Maelezo ya neno lake Allah Subhaanahu wa Taala Aliposema:

 

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ}      البقرة:143}

 

 

[Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.]    [Al-Baqara:143]

Kwa sababu Allah amewaeleza vizuri katika Qu’rani Aliposema Subhaanahu wa Taala:

 

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ   آل عمران:110

[Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.]    [Al-Imraan:110]

Ulinganizi wa Mitume wote ulikuwa Mfumo wake na Wakati Na kati
Ushahidi wake ni neno la Mtume lililopokewa kwa Abu Huraira Radhi zaAllah ziwe juu yake amesema Amesema  Mtume ﷺ:

 

إن الدين يسر، ولن يشاد أحد الدين إلا غلبه، فسددوا وقاربوا وأبشروا]     رواه البخاري]

 

[Hakika dini ni nyepesi wala mtu hatoifanyia dini mkazo isipokuwa itamshinda fanyeni usawa na karibisheni na mubashirie mazuri].    [Imepokewa na Bukhari]
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: 

 

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ}      الأنعام:162}

 

[Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.]    [Al-An'aam:162]

Ndugu Muislamu, Hapana shaka Mwenyezi Mungu anawaamrisha kati ya watu kuhukumu kwa uadilifu. Hapana shaka Allah anawapa mawaidha mazuri, hapana shaka Allah ni mwenye kusikia, kuona.
Na amesema Allah Subhaanahu wa Taala:

 

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ   القصص:77

[Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.]   [Al-Qaswas:77]

Ukati na kati wa Ahlu Sunnah wal Jamaah katika Itikadi na Kufuata Twaa
Amesema Allah Subhaanahu wa Taala:

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّهُ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ سُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا     النساء:171

 

[Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha]    [Al-Nnisaa:171]

Kutoka kwa Anas Ibn Malik Radhi za Allah ziwe juu yake. alisema: "Walikuja watu watatu mpaka kwa nyumba za wakeze Mtume wakauliza namna ya ibada za Bwana Mtume . Walipoambiwa walisema sisi tuko wapi na Mtume na yeye amekwisha samehewa madhambi yake yaliyotangulia na yatakayo kuja. Akasema mmoja wao ama mimi nitaswali usiku siku zote. Na mwingine akasema mimi nitafunga siku zote na na sitoacha kufunga na akasema mwingine na mimi nitajiepusha na wanawake sitooa kabisa. Mtume akawajia akawambia:

 

أَنْتُمْ الَّذِينَ قُلْتُمْ كَذَا وَكَذَا !! أَمَا وَاللَّهِ إِنِّي لَأَخْشَاكُمْ لِلَّهِ وَأَتْقَاكُمْ لَهُ ، لَكِنِّي أَصُومُ وَأُفْطِرُ ، وَأُصَلِّي وَأَرْقُدُ ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي

[Nyinyi ndio mliosema kadha wa kadha naapa kwa Allah mimi ni mnyenyekevu mno kwa Allah kuliko nyinyi na mimi numuogopa Allah kuliko nyinyi lakini nafunga na siku nyingine sifungi na naswali usiku na siku nyingine nalala na mimi huoa wanawake basi mwenye kuacha mwenendo wangu si miongoni mwa watu wangu].    [Imepokelewa na Bukhari na Muslim]

 

MANENO YA WANAVYONI KUTHIBITISHA UKATI NA KATI WA AHLU SUNNA

Amesema ibn Jarir At-Twabary Mungu Amrehemu kwamba Allah Subhaanahu wa Taala Amewasifu Umma huu ya kwamba wao ni watu wakati na kati, kwa ajili ya ukati na kati wao katika dini hawakupita mpaka katika dini. Kama walivyofanya wakristo ambao wamepita mipaka katika (tarhib) na wakasema kuhusu nabi issa ambaye nabii issa hakuyasema wala wao si watu (watakasirika) na kama (taksira) ya mayahudi ambao wamebadilisha kitabu cha Allah na wameuwa Mitume yao na wakamsingizia uongo mola wao (Waislamu) ni watu wa kati na kati na wamelingana katika hilo, wakasifu Allah kwa hilo, likawa jambo linalo pendeza zaidi kwa Allah ni lililo kati na kati.
Na Amesema Imam Shatwiby.Mungu Amrehemu ‘Ukiangalia katika kitendo cha sheria na ukazingatia utapata ndani yake kuna ukati na kati, na ukipata umelemea sehemu katika sehemu zake hilo ni kutoka na kukabiliana na ile hali ilivyo au ni kutokea katika sehemu nyingine. Sehemu (upande) uliomgumu sana ni kwa kulihofisha na kuhimiza na kukataza. Na upande au sehemu yenye ukhafifu sana inakuwa katika kutoa ruhusa na kuhimiza inakuwa mara nyingi ni uzito kulifanya jambo kuwa gumu, isipokuwa hivi au vile utaona Na upande wa usawa uko wazi nao ni msingi ambao wenye kurejelewa na mwenye akili ni yule ambaye atauelekea”.


KWA FAIDA ZAIDI SIKILA MADA HII NA AHMAD M.MUSALLAM




UMUHIMU WA KUTAFUTA ILIMU YA DINI


 148210 0


Ilimu ni msingi muhimu katika dini ya Kiislamu. Dini ya Kiislamu imejengwa juu ya Ilimu. Kwasababu Ilimu ndio mwangaza wa kuonyesha njia ya sawa na kuonyesha njia ya mbaya. Aya za kwanza alizo teremshiwa Mtume Muhammad Swalla Llahu ‘alayhi wasallam zilikuwa ni za kufundisha ilimu, na kuhimiza Waislamu wafanye bidii kutafuta ilimu. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ}

 

[Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.]   [Al-Alaq"1-5]
Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala)Ametumia katika Aya hizo maneno kama; soma, ilimu, kalamu, kufundisha, yote haya ni kuonyesha umuhimu wa kutafuta ilimu kwa kupitia njia tofauti za kuweza kukufikisha wewe kupata ilimu hio. Katika Aya hizo kuna ishara ya kuonyesha kwanza kabla ya kufanya vitendo vingine ni lazima mwanadamu apate ilimu ili aweze kutekeleza vitendo vyake kwa ujuzi zaidi na maarifa ya kutosha kinyume na mafundisho hayo, basi mwanadamu atafanya mambo kwa ujinga na baada ya kupata faida na mambo hayo, atapata hasara tupu ima kwa kudhuru nafsi yake au jamii kwa jumla.
Wajibu wa kutafuta Ilimu kabla ya kila kitu katika Mafundisho ya Qur’ani na Sunna

 

KATIKA QUR'ANI TUKUFU:

Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:

 

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ}    محمد:19}

 

[Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake.]   [ Mahammad:19]
Amesema Imam Bukhari katika kitabu chake Sahihi Al-Bukhari: "Mlango unaozungumzia kusoma ilimu kabla ya maneno na vitendo" Makusudio ya Imamu Bukhari ni kutafsiri Aya iliyotangulia ya kumaanisha ilimu mwanzo kabla ya vitendo. Ilimu imetangulizwa kwanza kabla ya kusema au kutenda, kwa sababu, ikiwa maneno na vitendo havikujengwa juu ya msingi wa Ilimu, maneno hayo na vitendo hivyo havina faida kwa mwenye kufanya. Khasara yake ni kubwa kuliko faida yake. Ndio Dini ya Kislamu kwanza ikatilia mkazo watu kusoma na kujuwa kabla ya kufanya vitendo.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ}     فاطر:28}

 

[Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni.] [Fatir:28]

Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Amesema:

 

وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا يَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ}    العنكبوت:43}

 

[Na hiyo ni mifano tunawapigia watu, na hawaifahamu ila wenye ilimu.]    [Al-Ankabut:43]

KATIKA SUNNA ZA MTUME ﷺ

Amesema Mtume ﷺ:

 

من سلك طريقاً يلتمس فيه علماً سهل الله له به طريقاً إلى الجنة]     رواه مسلم]

 

[Mwenye kufuata njia kwa ajili ya kutafuta Ilimu. Mwenyezi Mungu atafanyia wepesi njia ya kuingia peponi ].   [Imepokewa na Muslim]
Na Amesema Mtume katika Hadithi nyingine:

 

مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ]      رواه البخاري ومسلم]

 

[Mwenyezi Mungu akimtakia kheri mja wake humfundisha ilimu ya dini].   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Muislamu hawezi Kufahamu Qur’an na Sunna za Mtume ila kwa Ilimu. Ni lazima kwanza ajilazimishe na kusoma ili apate ujuzi wa kufahamu. Bila ya kufanya hivyo, atakuwa ni miongoni mwa waliosifiwa na sifa ya ujinga. Ndugu katika Imani, haya ndio mafundisho ya Allah na Mtume wake, yameweka wazi umuhimu wa kusoma kabla ya vitendo. Kwa hivyo, Allah (Subhaanahu wa Taala) hatokubali kwa mja wake ibada au vitendo vilivyo fanywa bila ya ilimu. Kwa sababu hio, ndio Sheria ya Kiislamu ikaamrisha Waislamu kusoma na ikawa hukumu ya kusoma ni wajibu juu ya kila Muislamu.

 

MAMBO YANAYO LAZIMU KATIKA KUTAFUTA ILIMU

Kuwa na Ikhlasi, nayo ni kusoma kwa ajili ya Allah Subhaanahu wa Taala. Muislamu lazima awe na lengo kubwa katika kutafuta ilimu nalo ni kusoma kwa ajili ya kutaka raadhi za Allah Subhaanahu wa Taala. Malengo mengine yanakuja baadae. Lakini, la msingi ni kusoma kwa ajili ya Allah Subhaanahu wa Taala.
Kuchunga haki za Mwalimu, kwa kumuheshimu na kumsikiliza vizuri wakati wa kusoma na kuuliza masuali kwa njia ya heshima.
Kupanga mikakati ya kusoma, kwa kutanguliza ilimu ambayo ni muhimu sana,kabla ya nyingine, Mfano wa kusoma ilimu ya faradhi kabla ya ilimu ya sunna.
Kufanyia kazi ilimu, na kuwa na hisia ya jukumu kubwa ulilo libeba. Na kujuwa ya kwamba utaenda kuulizwa ilimu yako mbele ya Allah. Je ulifanyia nini?
Kufundisha watu. Ilimu ni amana kutoka kwa Allah (Subhaanahu wa Taala). Na ili tuweze kutekeleza amana hii kama anavyotaka Mwenyezi Mungu, ni lazima tufanye bidii ya kuwafundisha wengine wasio bahatika kusoma. Amesema Mtume :

 

خيركم من تعلم القران وعلمه]    أخرجه البخاري]

 

[Mbora wenu, ni Yule aliye jifunza Qur’ani na akafundisha].  [ Imepokewa na Bukhari]

Kwa hakika, ni jukumu kubwa juu ya wasomi kufanya bidii kuifundisha ilimu waliopewa na Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala.


KWA FAIDA ZAIDI SIKILIZA MADA NA HII NA SHEIKH HAMMAD QASIM




ULINGANIZI WA MITUME


images 1


Kazi kubwa ya Mitume ni ulinganizi. Mitume wote walitumwa kuwalingania viumbe kushikamana na Tawhidi. Tawhidi ndio msingi wa ulinganizi.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:


وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ}    النحل:36}

 

[Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.]    [Al-Nnahl:36]

Mitume ya Allâh ni watu waliochaguliwa walio bora ushahidi neno Lake Allâh Subhaanahu wa Taala:

 

قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ}   هود:62}

 

[Wakasem a: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyo kuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayo tuitia.]   [Huud:62]
Na Neno Lake Allah  Subhaanahu wa Taala:

 

وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِإِنَّا أَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ  وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ}    ص:45}

 

[Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na busara.Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera. Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora. ]  [Swaad:45]
Mitume wote walikuja na ulinganizi mmoja. Wote waliwaambia wafuasi wao kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.

MFUMO WA ULINGANIZI

Kutanguliza Tawhidi kuliko ibada nyingine. ‘Abdullah bin ‘Abbass amesema: Mtume alimwambia Mu’adh Ibn Jabal Radhi za Allah zimfikie yeye wakati alipomtuma kwenda Yemen:

 

إنك ستأتي قوما أهل كتاب، فإذا جئتهم فادعهم إلى أن يشهدوا أن لا إله إلا الله، وأن محمدا رسول الله، فإن هم أطاعوا لك بذلك فأخبرهم أن الله فرض عليهم خمس صلوات كل يوم وليلة، فإن هم أطاعوا لك بذلك، فأخبرهم أن الله فرض عليهم صدقة تؤخذ من أغنيائهم فترد على فقرائهم، فإن هم أطاعوا لك بذلك فإياك وكرائم أموالهم، واتق دعوة المظلوم فإنه ليس بينها وبين الله حجاب

[Hakika unawaendea watu ambao ni Ahlul-Kitâb. Utakapowaendea, walinganie washuhudie kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh, na kuwa mimi ni Mtume wa Allâh. Watakapokutii kwa hilo, wajulishe kuwa Allâh Amewafaradhia Swala tano kila mchana na usiku. Watakapokutii kwa hilo, wajulishe kuwa Allâh Amewafaradhia Zaka, inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na wanarudishiwa mafukara wao. Watakapokutii katika hilo, basi tahadhari mali yao yenye thamani. Na uogope dua ya mwenye kudhulumiwa, kwani hakuna pazia baina ya dua hiyo na Allâh]. [Imepokwea na Bukhary]

Kutumia Lugha inayo fahamika na walinganiwa. Ushahidi ni Neno Lake Allâh Subhaanahu wa Taala:



وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُم}   إبراهيم:4}

 

[Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.]   [Ibrahim:4]

Amesema Mtume ﷺ :
[Atakapowajia mkarimu wa watu basi mkirimuni]. [Imepokewa na Ibu Majah.]

Mwangalie Nabii Nuh aliwaambia watu wake: Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. Mimi si chochote ila ni Mwonyaji wa dhahiri shahiri. Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. Basi Hukumu baina yangu na wao kwa Hukumu Yako, na Uniokoe na walio pamoja nami, Waumini.
Kuchagua washirika wazuri katika kusaidiana kulingania watu. Ushahidi ni Neno Lake Allâh(Subhaanahu wa Taala)Alipomfanya Musa waziri wake kuwa ni Harun:


وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي هَارُونَ أَخِي اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا}   طه:29-34}

 

[Na nipe waziri katika watu wangu, Harun, ndugu yangu. Kwake yeye niongeze nguvu zangu. Na umshirikishe katika kazi yangu. Ili tukutakase sana. Na tukukumbuke sana.]  [Twaha:29-34]

 

قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ}    هود:63}

 

[Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake - je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamtanizidishia ila khasara tu.]   [Huud:63]
Mwangalie Mtume Muhammad , Aliposema Allah Subhaanahu wa Taala:

 

وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا   الإسراء:73-74

 

[Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya rafiki , Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo. Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu mardufu ya uhai, na adhabu mardufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi.]   [Al-Israai:73-75]
Aya na Hadithi zinabainisha wazi mfumo wa Mitume ya Allah katika kulingania wanadamu. Na haya ni mafundisho kwa kila Muislamu atakaye fanya kazi hii ya mitume. Ni lazima afuate mfumo sahihi wa kulingania nayo ni mfumo wa Mitume.


 KWA FAIDA ZAIDI SIKILA MADA HII NA SHEIKH ABUU HAMZA




VYOMBO VYA HABARI NA ATHARI YAKE


 show 1


Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe vyote na rehma na amani zmfikie Mtume Muhammad. Napenda kuitanguliza mada hii ya vyombo vya utangazaji, kuwatajia umuhimu wake. Na pia nitawabainishia vipi vyombo vya utangazaji vinaweza kuitumikia Dini na matatizo yanayo vikabili vyombo hivyo.

Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Ametupa neema ya ulimi ili tumshukuru kwa neema hiyo kwa kuitumia vilivyo kwa mujibu wa mafunzo mema ya kiislamu. Ametuamrisha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala kuutumia ulimi vizuri tunapozungumza.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا}

 

[Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa.]    [Al-Ahzaab:70]

Na Mtume ﷺ asema:

 

من كان يؤمن بالله واليوم الآخر، فليقل خيرًا أو ليصمت]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, basi aseme maneno mazuri au anyamaze].    [Imepokewa na Bukahri na Muslim]

Na Ametilia nguvu mshairi akisema: ‘Zungumza vizuri uwezavyo kwani maneno yako ni yako na kunyamaza ni vizuri na ikiwa hutapata maneno mazuri ya kuzungumza basi kunyamaza bila ya kufanya vizuri ni vizuri’. Asema mshairi mwengine: ‘Kuzungumza ni vizuri na kunyamaza ni usalama basi unapozungumza usiwe na maneno mengi kwani sijajuta kwa kunyamaza hata mara moja lakini nimejuta juu ya maneno yangu mara nyingi’.

Kwa mujibu wa Aya na hadithi na mashairi tuliyoyataja inaonesha wazi kuwa Muislamu hafai kabisa kuutumia ulimi wake kinyume na maagizo ya Allah (Subhaanahu wa Taala), huku tukijua ya kwamba kila siku watu wanawasilina kupitia njia tofauti tofauti kama kutumia simu, barua, na vyombo vingine vya mawasiliano, bali wengine kupitia vyombo vya utangazaji. Na kwa kweli watu wamevielekea mno vyombo hivyo ili kupata habari mbali mbali.

Kwa kweli vyombo vya utangazaji vina faida zake na hasara zake. Kwa hivyo hatusemi kwamba haifai kutumia vyombo hivyo, lakini isiyofaa ni kuvitumia katika njia mbaya isiyokubalika kiislamu. Kwani makafiri wakiwemo Waamerika na Wamagharibi wame vitumia vyombo hivi katika kuwapotosha wanaadamu na njia ya sawa, vikiwemo vyombo vya kusikiliza kama redio na vyombo vya kuonesha kama runinga na vya kusoma kama magazeti, majarida na vyenginevvyo.

Kwa kweli vyombo vya utangazaji vimechukua nafasi kubwa kabisa katika kuwaathiri na kuwapotosha watu kimaadili. Sasa wajibu wetu ni mambo gani ya upotofu yanayoenezwa na makafiri katika vyombo vya utangazaji?. Bila shaka wajibu wetu ni kuwatahadharisha watu na uovu unaoenezwa na vyombo hivyo, kwa kuwalingania katika Uislamu na kuacha upotofu. Napenda kuchukua fursa hii kukuliza maswali yafuatayo:

Ulinganizi ni nini ndugu zangu katika imani?

Ni upi umuhimu na ubora wa ulinganizi?

Ni lipi lengo na hukumu ya ulinganizi?

Ni ipi misingi ya ulinganizi ?

Ni zipi nguzo za ulinganizi?

Ni zipi njia na aina za ulinganizi?

Umuhimu wa Ulinganizi

Ulinganizi ni kuwaita watu na kuwafundisha uislamu na kuutekeleza kimatendo kwa ajili ya kuwatakia kheri katika maisha yao hapa duniani na kesho akhera.

Umuhimu wa kulingania watu ni kwamba mlinganizi ana daraja kubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu kwa sababu anawaita watu kuwacha ibada zote mbaya na kushikamana na ibada ya Mwenyezi Mungu peke yake. Amesema Mola (Subhaanahu wa Taala): “ Na hakuna mwenye maneno mazuri kuliko yule anayewalingania watu kwa Mwenyezi Mungu na akafanya vitendo vizuri na akasema Mimi ni katika Waislamu”.

Umuhimu wa ulinganizi ni kwamba anapata anayelingania ujira mkubwa. Mtume amesema:

 

مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنْ الْأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا]   رواه مسلم]

 

[Anayelingania katika uongofu atapata ujira sawa na atakayeufuata uongofu huo na hatapunguziwa katika ujira wake kitu chcchote].   [Imepokewa na Muslim]

Umuhimu wa kulingania vile vile ni kutii na kutekeleza amri ya Mtume aliposema:

 

بلِّغوا عني ولو آية]   رواه البخاري]

 

[Nifikishieni hata kama ni Aya moja].   [Imepokewa na Bukhari]

Kulingania hupatikana ndani yake ukamilifu wa kumfuata Mtume katika ulinganizi wake wa busara. Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala Aasema:

 

قُلْ هَٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ}     يوسف:108}

 

[Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.] [Yusuf:108]

Wametofautiana wanavyuoni katika hukumu ya ulinganizi, je ni lazima kwa kila mtu au wakifanya baadhi huwatosheleza wengine?. Wanavyuoni wengine wamesema kwamba ni lazima kwa kila Muislamu na wengine wamesema kwamba wakifanya baadhi ya Waislamu huwatosheleza waliobakia. Lakini ilivyo ni kwamba ulinganizi ni lazima kwa kila Muislamu kulingana na uwezo wake. Amesema Mola Subhaanahu wa Taala:

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ

 

[Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.]    [Al-Imraan:110]

Amesema Mtume :

 

من رأى منكم منكرًا، فليغيره بيده، فإن لم يستطع فبلسانه، فإن لم يستطع فبقلبه، وذلك أضعف الإيمان]    رواه مسلم]

 

[Atakayeona jambo baya katika nyinyi basi aliondoshe kwa mkono wake na ikwa hawezi basi aliondoshe kwa ulimi wake(kwa kusema)na ikiwa hawezi basi achukie kwa moyo wake na huo ni udhaifu wa Imani][Imepokewa na Muslim]

Nachukua tena fursa hii kuitaja misingi inayotegemewa katika kulingania, nayo ni:

Qur’an Tukufu,

Hadithi za bwana Mtume rehma na amani zimfikie yeye

Sira ya Mtume  na

Historia ya makhalifa wema waongofu. Misingi tuliyoitaja ndiyo ambayo anayelingania huitumia kuwaita watu katika kheri.

Nguzo za Ulinganizi

Nguzo ambazo ni lazima zipatikane ndio upatikane ulinganizi na nguzo hizo ni kama

zifuatazo:

Mlinganizi

Anayelinganiwa

Kinacholinganiwa

Njia na aina za ulinganizi.

Yatakiwa mlinganizi asifike na apambike na sifa njema alizokuwa nazo Mtume rehma amani zimfikie sifa hizo ni ukweli, uaminifu, kumtakasia Mwenyezi Mungu ulinganizi, ushujaa, upole, maneno mazuri, subira, uadilifu, na sifa nyingine nzuri.

Wanaolinganiwa ni aina tofauti za watu. Kuna Waislamu, wanafiki, makafiri, viongozi, raia, wakubwa na wadogo. Na kila mmoja katika hawa kuna njia na namna yake ya kumlingania.

Kinacholinganiwa ni Uislamu na hii kazi ya Mitume wote. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ}

 

[Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.]    [Al-Nnahl:36]

Njia za ulinganizi ni nyingi.

Miongoni mwa njia hizo kuwasiliana na mtu moja kwa moja, kutoa khutba, kuandika vitabu, kufundisha madrasa au vyuo vikuu, kuandika makala gazetini, kutumia vyombo vya utangazaji kufikisha ujumbe kama redio, runinga na vyinginevyo. Kwa hivyo inatakiwa tuwe makini na ufisadi unaopatikana katika vyombo vya habari inatakiwa tuwatahadharishe Waislamu popote waliopo na uovu unaoenezwa na vyombo hivi.

Miongoni mwa aina na sampuli za ulinganizi ni kuwa mfano mzuri wa katika jamii, kujadiliana kwa lengo la kuelimishana, kutumia hikma, pia kutumia mawaidha mazuri, kutumia mifano kwa kutoa visa, na kutumia vitisho na kutia moyo katika mawaidha. Na inatakiwa mlinganizi achague aina ya ulinganizi ambao anaona itakuwa wepesi kukubaliwa ulinganizi wake.

 

{وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا}

 

[Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa.]    [Al-Israa:36]

Pia Amesema Mola Subhaanahu wa Taala:

 

{وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ}

 

[Na msemapo semeni kwa uadilifu ingawa ni jamaa.]   [Al-An'am:152]

Na pia Amesema tena Allah Subhaanahu wa Taala:

 

{وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنزَغُ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوًّا مُّبِينًا}

[Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.]   [Al-Israa:53]

 

MISINGI YA VYOMBO VYA UTANGAZAJI 

Uislamu umeweka misingi kuvifanya vyombo vya utangazaji kuwa imara.

Msingi wa kwanza na muhimu kabisa katika maisha ya watu ni kumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Amesema Mwenyezi Subhaanahu wa Taala:

 

{اعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ }

 

[Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu]   [Muhammad:19]

Mwingine ni kuhisi majukumu wa kuwalingania watu katika njia ya kheri, kuwa mkweli katika maneno na matendo, pia kuwa muadilifu na kuzingatia adabu za mjadala wakati anapojadiliana na kupeana mawaidha mazuri. Amesema Allah Subhaanahu wa Taala:

 

{ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ}

 

[Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.]    [Al-Nnahl:125]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487896
TodayToday1002
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 60

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e7044b6ad09634840651735290948
title_676e7044b6bc217259627221735290948
title_676e7044b6cae12775446531735290948

NISHATI ZA OFISI

title_676e7044b84314950492441735290948
title_676e7044b85846966636061735290948
title_676e7044b86aa9613568581735290948 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 9 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com