Menu

Sehemu ya Misimo


MWEZI WA RAJAB


 images 2


Mwezi wa Rajab ni mwezi wa saba katika kalenda ya kiislamu na ni katika miezi mitakatifu ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu ameusia waja wake wasijidhulumu katika Miezi hiyo,

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukfu:

 

إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ   التوبة:36

 

[Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo]     [Tawba:36]


Na Allah subhanahu Wata’ala kwa hikma yake amefadhilisha baadhi ya siku kuliko siku nyingine, kama alivyo ifadhilisha siku ya ijumaa katika Wiki,na ameifadhilisha baadhi ya Miezi kuliko miezi mengine kama alivyo ifadhilisha miezi hii minne mitakatifu ,Dhulqa’ada, Dhul hijja, Muharram,na Rajab kuliko miezi mengine katika Mwaka,na kadhalika Mitume kwa Hikma yake Subhanah.
Na Waarabu kabla ya Uislamu walikuwa wakiutukuza mwezi huu wa Rajab na wakiuhishimu wakiacha kupigana vita na uhasama, na wameupatia majina tofauti kwa sababu ya kuutukuza kwao, miongi mwa majina hayo;
1 Al’aswam (Kiziwi) kwa sababu walikuwa wakiacha kupigana na kuwa haisikiki milio ya silaha
2. Al’Aswab (wenye kumiminwa) Maqureshi walikuwa wakitakidi kuwa Mwezi wa Rajab Mwenyezi Mungu humimina kheri yake kwa Wingi.
3. Rajm (kufukuzwa) kwa sababu Mashetani hufukuzwa katika Mwezi huu.
Na walikuwa na majina mengi lakini tutosheke na hayo, na majina yote hayo ni kuwa mwezi huu wa Rajab ulikuwa ukihishimiwa na kutukuzwa na waarabu kabla ya kuja Uislamu .
Na Mtume ﷺ asema katika hadithi iliyopokelewa na Abi bakara radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ alikhutubu katika hija yake akasema:

 

إن الزمان قد استدار كهيئته يوم خلق الله السموات والأرض، السنة اثنا عشر شهرًا منها أربعة حُرُم، ثلاثة متواليات ذو القعدة وذو الحجة والمحرم، ورجب مُضر الذي بين جمادى وشعبان       متفق عليه

 

[Hakika zama zimezunguka kama siku alivyo umba Mwenyezi Mungu mbingu na Ardhi, Mwaka una miezi kumi na mbili, katika hiyo (Miezi ) kuna minne mitakatifu, mitatu imefuatana Dhulqaada, dhulhijja, Muharram na Rajab Mudhwar ulioko kati ya Jumada na Shabani.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Na Mtume  ameuita Rajab Mudhwar kwa sababu kabla ya Uislamu kulikuwa na Ikhtilafu kuhusu mwezi huu wa Rajab kabila la Rabii’a walikuwa wakisema Rajab ni mwezi wa Ramadhani kwa sababu hiyo wao walikuwa hawau hesabu mwezi huu wa rajab kuwa ni katika miezi mitakatifu na kabila la Mudhwar walikuwa wakiuhishimu Mwezi Huu, ulipokuja Mtume akabainisha kuwa Mwezi mtukufu ni Mwezi huu wa rajab Mudhwar yaani unaotukuzwa na kabila la Mudhwar na akutaka kuweka wazi akabainisha kuwa ni Mwezi ulioko kati ya Jumad na Shabani,na kumesemwa kuwa kabila hili la Mudhwar walikuwa wakiuhishimu mwazi huu wa Rajab zaidi kuliko makabila mengine.

JE KATIKA MWEZI HUU KUNA IBADA MAALUM.

Pamoja na kuwa Mwezi wa Rajab ni katika Miezi Mitakatifu lakini Mwezi Mungu Mtukufu,na Mtume wake  hawakuhusisha Mwezi huu na ibada Makhsusi, wala hakupokelewa kwa bwana Mtume  kuwa alikuwa akiuhusisha Mwezi huu wa Rajab kwa ibada, linalo takikana kwa kila muislamu ni kufuata mafundisho tulio fundishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nao ni kujiepusha na kufanya Madhambi katika Mwezi huu,na tusiwe ni wenye kujidhulumu nafsi zetu kama alivyo sema Menyezi Mungu:

 

{فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ}

[Basi msidhulumu nafsi zenu humo]

Na wala tusifanye lolote lile ambalo hatukufunzwa na dini yetu.

Asema Ibnu Hajar Mwanachuni maarufu Mungu amrahamu:


 لم يرد في فضل شهر رجب، ولا في صيامه، ولا في صيام شيء منه معين، ولا في قيام ليلة مخصوصة فيه حديث صحيح يصلح للحجة              تبيين العجب  ص:6

"Haikupokelewa katika kufadhilsha Mwezi wa rajab,wala katika kufunga kwake, wala katika kufunga siku Fulani katika mwezi huu wala kuhusisha usiku kwa kisimamo hadithi sahihi ambao inaweza kuitolea hoja."    [Tabyinul Ujab uk 6] 

MAMBO YALIOZUSHWA KATIKA MWEZI WA RAJAB 

Katika mwezi huu wa rajab kuna baadhi ya waislamu wanaitakidi mambo mengi ambayo yamezuliwa katika dini na mambo ambayo hayakujulikana wakati wa Bwana Mtume  wala zama za Makhalifa waongofu, wala karne tatu zilizo bora,na baadhi ya mambo hayo watu wamemzulia Mtume  hadithi za urongo na waislamu wengi wakaitakidi kuwa ni katika mambo ya kheri kwa sababu ya kutoijuwa dini yao,katika baadhi ya mambo ya uzushi ni kama yafuatavyo:

1. Kusherehekea usiku wa Israa na Miraaj

Baadhi ya waislamu wanasherehekea usiku wa ishrini na saba wa mwezi huu wa Rajab kwa kuwa ndio usiku wa Israai na Miraaji (usiku aliopelekwa Mtume kutoka Makkah hadi Masjidul Aqswaa na kutoka Masjidul Aqswa mpaka uwingu wa saba) na jambo hili si sahihi bali wanazuoni wa tarekhe wamekhitalifiana juu ya hilo,kuna wanaosema kuwa ilikuwa ni 27 mwezi wa mfungo sita na kuna wanaosema ni mwezi wa mfungo saba.Na hata kama tarehe hiyo ya mwezi wa Rajab ni sawa lakini haijapokelewa kutoka kwa Mtume wetu  wala kwa Maswahaba wa tukufu kuwa walikuwa wakisherehekea siku hiyo, na bila shaka kama ingelikuwa ni Sunna au ni katika jambo la dini wao wangelikuwa wa kwanza kulifanya hilo.

2. Kukhusisha Mwezi wa Rajab na Kufunga

Kuna baadhi ya wailsamu wanaitakidi kuwa ni Sunna kufunga mwezi huu wa Rajab na Shaban na Ramadhan yani kufululiza kufunga miezi mitatu hii kwa pamoja, na kuna Hadithi za kuhimiza waislamu kufunga mwezi huu lakini hadithi hizo karibu zote ni Hadithi Dhaifu na nyingine ni hadithi Maudhui za kupangwa kama walivyosema wanachuoni wa Hadithi.
Asema Ibnul Jawziyah katika kuelezea muongozo wa Mtume  katika kufunga saumu za Sunna


لم يصم الثلاثة الأشهر سردًا ـ رجب وشعبان ورمضان ـ كما يفعله بعض الناس، ولا صام رجبًا قط، ولا استحب صيامه، بل روي عنه النهي عن صيامه ذكره ابن ماجه       زاد المعاد (2/64

"Hakufunga miezi mitatu kwa mfululizo Rajab na Shaban na Ramadhani kama wanavyo fanya baadhi ya watu,wala hakufunga mwezi wa Rajab kabisa,wala hakusunisha kufunga,bali imepokewa kukataza kufunga kama alivyo taja Ibnu Maajah."    [Zaadul Ma'aad 2/64]

3. Swalatu Raghaib

Baadhi ya waislamu wanaitakidi kuwa ni Sunna muislamu kuswali Al hamisi ya kwanza katika Mwezi wa Rajab au usiku wa kuamkia ijumaa rakaa kumi na mbili,na imekuja hadithi Maudhui kuhusu swala hii ikielezea namna ya kuswaliwa kwake haina haja ya kuelezea hadithi kama hiyo,la muhimu ni kujuwa kuwa haikuthubutu kutoka kwa mtume Swala Maluum katika Mwezi huu wa Rajab

Asema Imamu Annawawiy Mwanachuoni Marufu wa Madhehebu ya Imamu shafiy Mungu amrahamu


هي بدعة قبيحة منكرة أشد إنكار، مشتملة على منكرات، فيتعين تركها والإعراض عنها، وإنكارها على فاعلها"     فتاوى الإمام النووي  ص:57"

 

"Hiyo ni Bid’a mbaya yenye kupingwa sana, na imekusanya mambo ya munkar,ni lazima kuiwacha na kuipuuza na kumpinga anae ifanya"     [Fatawal Imamu Annawawiy uk 57]
Hizi ni baadhi ya mambo ya uzushi yaliozushwa katika Mwezi huu wa Rajab,na ni wajibu kwa kila Muislamu ambae alikuwa hajui na akiitakidi mambo kama haya basi akomeke na kuachana na Bid’a kama hizi
Twamuomba allah atujalie tuwe ni wenye kufuata Sunna za bwana Mtume na atuepushe na mambo ya Bid’aa na uzushi.



MWEZI WA MFUNGO SITA


  3644120812245 thumb2


Mwenyezi Mungu mtukufu ameitukuza baadhi ya miezi kuliko miezi mengine na akawataka waja wake wasijidhulumu katika miezi hiyo kwa kufanya Madhambi na kuasi.Mwenyezi Mungu asema katika Qur'ani tukufu:

 

إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ    التوبة:36

[Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo]      [Al-Tawba:36]

Na Mtume wetu akaja kubainisha Miezi hiyo mitakatifu kuwa ni mwezi wa Dhulqaada, Dhulhijja, Muharram na Rajab, hii ndio miezi mitakatifu iliyotajwa na Mwenyezi Mungu alietukuka.
Ama kuhusu Mwezi wa Mfungo sita hakuna dalili katika Qur'ani wala katika Hadithi za Bwana Mtume  kuwa ni katika Miezi ambayo ni mitakatifu, ila tu katika Mwezi huu kumetokea matukio muhimu katika tarekhe ya Uislamu,na katika matukio hayo:

1.KUZALIWA MTUME WETU MUHAMMAD  

Ni kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad kwa kauli ya wengi katika wanazuoni wa tarekhe ya Kiislamu, ila tu kuna wanao sema kinyume na mwezi huu kwani hakuna dalili ya wazi ya kuonyesha kuwa mtume alizaliwa mfungo sita lililo afikiana na siku ya kuzaliwa kwake nayo ni siku ya juma tatu kama ilivyo kuja kwenye hadithi alipoulizwa kuhusu kufunga siku ya ijuma tatu akasema:

 

فِيهِ وُلِدْتُ وَفِيهِ أُنْزِلَ عَلَيَّ]    رواه مسلم]

 

[Siku hiyo (Juma tatu) nilizaliwa na siku huyo nikateremshiwa wahyi (ufunuo).]

2.KUGURA KWA BWANA MTUME MUHAMMAD  

Mtume baada ya kupata pingamizi makkah katika Da'wa yake na kupata udhia kwa Maquraish na kufanya njama za kutaka kumuuwa, Mwenyezi Mungu alimwamrisha mtume wake kugura kutoka Makkah na kuhamia Madina; Mtume alitoka makkah tarehe mosi ya mwezi wa mfungo sita na kufika madina tarehe kumi na mbili katika mwezi huo.

3.KUFARIKI MTUME MUHAMMADA 

Tukio la tatu katika Mwezi huu wa Mfungo sita ni tukio kubwa sana nalo ni kufariki Mtume wetu Muhammad  tukio lililo kuwa zito sana kwa Maswahaba wa Bwana Mtume na waislamu wote, Mtume  alifariki siku ya ijuma tatu tarehe kumi na mbili mwezi wa mfungo sita na tarehe hii ndio rai ya Jamhuri ya wanachuoni.
Kwa hivyo haya ndio matukio muhimu yaliyotokea katika Mwezi huu wa mfungo sita. Lakin leo watu wamezua mengi katika Mwezi huu mambo ambayo yalikuwa hayajulikani wakati wa Mtume  na Maswhaba wake, na jambo lolote lisilo kuwa ni dini wakati wa Mtume  na Maswahaba wake basi haliwezi kuwa ni Dini wakati wowote ule.
Na katika mambo yaliyozuliwa katika mwezi wa mfungo sita ni kusherehekea kuzaliwa kwa Bwana Mtume , hili ni jambo ambalo limezuliwa katika dini wala Maswahaba na Qarni tatu zilizo bora jambo hili walikuwa hawalijui, na kama ni jambo zuri hili la kusherehekea Mazazi ya Bwana Mtume ﷺ basi wao wangelikuwa ni wa kwanza kulifanya hilo kwani wao walikuwa wakimpenda Mtume kutuliko sisi.
Na hapa napenda tutafautishe kumsifu mtume  na kumswalia Mtume  na kusherehekea mazazi ya Mtume  maana kuna watu wachanganya mada hizi na kufanya ni jambo moja.
Hakuna anaepinga kumswalia Mtume ﷺ wala kumsifu Mtume , kwani tumeamrishwa na dini yetu kumswalia Mtume katika swala mara tano kwa siku na kumswalia wakati wowote. Na kumsifu Mtume Muhammad  amesifiwa na Allah aliyemtukufu ila tu nawe usivuke mipaka katika sifa zako na kumsifu kwa sifa ambazo hastahiki kuwa nazo. Linalo pingwa nikuweka sherehe Maluum ya kusherehekea kwa kuzaliwa kwake kama wengi wanavyo fanya hili ndilo jambo linalo pingwa kwani hilo ni Uzushi lililozushwa katika dini.

 

NI NANI ALIE ANZISHA SHEREHE ZA MAULIDI

Jambo hili la kusherehekea kwa kuzaliwa Mtume  lilianzishwa na Mashia katika zama za dola ya Fatimiya na aliezuwa jambo hili ni Al-Muizz lidinillah Al Fatwimiy na wanachuoni wasema kuwa hawa walikuwa ni Mazandiki na lengo lao lilikuwa ni kutaka kuwaiga manaswara kwa hilo, kwa fikra ya kwanini wakiristo wako na siku ya kusherehekea siku ya kuzaliwa Nabii Issa Alayhi salaam na sisi waislamu hatuna. Hawajui kuwa dini yetu imekataza Waislamu kujifananisha na Mayahudi na Manaswara, hata jambo la ibada ya kufunga Mtume  alipofunga Ashuraa akasema atafunga na taasua ili awakhalifu Mayahudi.
Mwisho:
Waislamu tusomeni dini yetu na tuifahamu vyema na tusiwe washindani katika mambo ambao yako wazi kuwa ni kinyume na Mafunzo ya Bwana Mtume rehma na amani zimfikie yeye… twamuomba Allah atujalie tuwe ni wenye kufaidika Na tunayosoma. Amin


IDUL-ADH'HA

maxresdefault

Idul Adhaha (Iddi ya kuchinja) ni mojawapo ya idd mbili katika Uislamu na inakuwa tarehe kumi Dhulhijaa baada ya kusimama Arafa sehemu ambayo wamesimama mahujaj katika kutekeleza Hijja, na kwisha Iddi hiyo tarehe 13 Dhulhija. Iddi hiyo ni kukumbuka kisa cha Nabii Ibrahim alipotaka kumchinja mwanawe Ismail kwa ajili hiyo wanasimama Waislamu kuchinja wanyama.

 

Hekima ya Swala ya Iddi

 

Imeshurutishwa swala ya Iddi ili kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu na kushibisha matamanio ya binadamu.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

{فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ}   الروم:30

 

"Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru."     [Al-Rruum:30]

Iddi ni Mkusanyiko wa Mambo Manne:

  1. Kukusanyika kwa watu.
  2. Kukusanyika kwa sehemu.
  3. Kukusanyika kwa wakati.
  4. Kukusanyika kwa ibada maalum.

Amesema Mwenyezi Mungu  Subhaanahu wa Taala:

 

{وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۗ فَإِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ}     الحج:34

 

"Na kila umma tumewafanyia mahala pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyo ruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tuJisalimishieni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu."     [Al-Hajj:34]

Imepokewa na Anas (R.A.) kwa Mtume  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  alipokwenda Madina aliwakuta watu wa Madina wana siku mbili wanacheza, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akawaambia [Mwenyezi Mungu amekubadilishieni siku mbili hizi kwa iddul Adha(kuchinja) na Iddul-fitr (baada ya Ramadhani]

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ}      {الكوثر:2

"Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi."    [Al-Kawthar:2]

Hukumu ya Kuchinja katika Siku ya Iddi Pamoja na Sharti Zake na Namna ya Kuchinja.

 

Amesema Ibnu ‘Umar (R.A.) "Kuchinja ni sunnah”. Na Amesema Imam Sha’abi: Mungu Amrehemu “ Haruhusiwi mtu kuacha kuchinja isipokuwa kwa mwenye kuhiji na kusafiri”.

Na Imepokewa na Ibnu Majah kwa Mtume  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam ameamrisha kugawanya nyama ya Udhiya mara tatu akisema kuleni, toeni sadaka na muhifadhi.

Kushurutishwa Kupiga Takbira pamoja na Hukumu Zake na Namna yake

Imepokewa na Ibnu Abbas amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  [hakuna siku kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, wala siku zinazopendekezwa kwake amali kama siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhulhija, zidisheni Tasbihi na Takbiri na Tahlil (Lailaha ila Allah).]





FADHLA YA KUFUNGA SIKU YA ASHURA'A


  فضل عاشوراء


Mwezi wa (muharram) ni katika miezi mitukufu na ndio mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiuslamu na tarehe 10 ya mwezi huu (Ashuuraa) ni siku adhimu na ina historia kubwa kwani siku hii ndiyo siku ambayo ALLAH alimuokoa Nabii (Mus a.s) na wana waisraeli kutokana na mateso na vitimbi vya fir'aun.Siku hii Mtume  aliwakuta maqureish wakifunga zama za ujahiliyyah na mtume alifunga kama ilivyo kuja kwenye hadithi iliyokelewa na Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesem:

 

كان يوم عاشوراء تصومه قريش في الجاهلية، وكان رسول اللَّه صلى الله عليه وسلم يصومه في الجاهلية]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Ilikuwa siku ya Ashuraa maqurish wakifunga zama za ujahilihiya na alikuwa Mtume rehma na amani zimfikiyeye alikuwa akifunga zama za Al-Jaahiliyah.]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na Mtume  alikuwa akiwahimiz awaislamu kuifunga siku hii ya ashura kabla ya kufaradhiwa mwezi wa Ramadhani.

 

وعن قيس بن سعد بن عبادة رضي اللَّه عنه قال: " أمرنا النبي صلى الله عليه وسلم أن نصوم عاشوراء قبل أن ينزل رمضان، فلما نزل رمضان، لم يأمرنا ولم ينهنا، ونحن نفعله      أخرجه النسائي في الكبرى وأحمد

 

Kutoka kwa Qays bin sa'd bin Ubaada radhi za Allah ziwe juu yake asema: [Alituamrisha Mtume tufunge Ashuraa kabla ya kufardhiwa ramadhani,ilipo faradhiwa Ramadhani hakutuamrisha wala hakutukataza,na sisi tulikuwa tukifunga.]      [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ahmad]

Na Mtume alivyokwenda Madina aliwakuta mayahudi wanafunga siku hii alivyowauliza wakasema hii ndio siku ambayo ALLAH alimuokoa Nabii wetu Musa kutokana na fir'aun kwahivyo musa alifunga kwa kumshukuru ALLAH na sisi twafunga kwa kumshukuru ALLAH kumuokoa Nabii wetu na fir'aun.kama ilivyo pokelewa Kutoka kwa Ibnu Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake asema:

 

" قدم رسول اللَّه صلى الله عليه وسلم المدينة فرأى اليهود تصوم يوم عاشوراء، فقال: ما هذا؟ قالوا: هذا يوم صالح، نجّى اللَّه فيه موسى وبني إسرائيل من عدوهم، فصامه، فقال: أنا أحق بموسى منكم فصامه وأمر بصيامه         رواه البخاري ومسلم

 

Mtume  ﷺ alipokwenda Madina aliwaona Mayahudi wakifunga siku ya Ashura'a akauliza ni saumu gani hii ? wakasema: Hii ni siku bora Mwenyezi Mungu alimuokowa nabii Musa na wana Waisrail kutokana na adui yao,(Musa) akafunga,

Mtume ﷺ akawaambiia [sisi tuna haki kwa nabii musa kuwashinda nyinyi basi mtume akafuna na akatuamrisha ifungwe.]        [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na ni bora kufunga pamoja na tarehe 10 tarehe 9 ili kuwakhalifu mayahudi kwani hata mtume Muhammad ﷺ alifunga miaka 9 aliyoishi madina siku ya Ashura'a na Maswahaba walipo mwambia kuwa Mayahudi waitukuza siku hii akasema:

 

"لئن بقيت إلى قابل لأصومن التاسع 

 

[Nikiisha mpaka mwakani nitafunga siku ya 9"]   Lakini mtume hakuishi.  

[Imepokewa na Muslim na Abuu Daud.] 

Na imekuja katika hadithi nyingine ya kutilia mkazo la hili la kuwakhalifu Mayahudi.

 

صوموا يوم عاشوراء، وخالفوا فيه اليهود، صوموا قبله يوماً، أو بعده يوماً]    أخرجه أحمد وإبن خريمة والبيهقي]

 

[fungeni siku ya Ashuura'a na muwakhalifu Mayahudi, fungeni siku kabla yake, au siku baada yake.]      [Imepokewa na Ahmad na Ibnu Khuzaymah na Al-Bayhaqiy.]  

 

FADHLA YA KUFUNGA SIKU HII 

 

Na katika kufunga siku hii kuna fadhla nyingi.

kwanza: ni kufwata sunna ya mtume Muhammad ﷺ.

Pili: imekuja katika hadithi ya mtume kwamba amesema:

 

عن أبي قتادة رضي اللَّه عنه ، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: " صيام يوم عاشوراء، أحتسب على اللَّه أن يكفر السنة التي قبله    أخرجه مسلم وأبوداود

Kutoka kwa Abii Qatada radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume  amesema: [kufunga siku ya ashura'a natarji kwa ALLAH kwamba inafuta madhambi ya mwaka uliyopita]       [Imepokewa na Muslim na Abuu Daud.

Na madhambi yanayosamehewa ni madhambi madogo,ama madhambi makubwa ni lazima mtu alete Tawba kwa Allah.

Na hii ni fadhla kubwa kutoka kwa ALLAH.

 

UTARATIBU WA KUFUNGA SIKU YA ASHURA'A 

 

Na kufunga swaum ya (Ashura'a) iko aina tatu.

 1- kufunga tarehe kumi peke yake yaani (Ashura'a)

 2- kufunga tarehe 9 na 10 

3- kufunga tarehe 9,10,11 Zote hizi ni sahihi.

Na ubora katika aina hizo tatu ni kufunga 9,10,11,kama walivyo elezeya wanachuoni.

Imeadnikwa na 

Fadhil Muhammad Shirazy

Mombasa –Kenya.



IDUL-FITR


ob 7b8ef5 tkm3bl


Iddi ya Fitri ni Iddi ya kwanza kwa Waislamu. Waislamu wanasherehekea katika mwezi wa Shawwal kinyume na Iddul adhha ambapo Waislamu wanasherehekea katika mwezi wa Dhulhijjah. Waislamu wanakula baada ya kufunga mwezi mzima, ni haramu kufunga siku hiyo. Na muda wa kusherehekea ni siku moja hadi siku sita.

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala kukamilisha kufunga mwezi wa Ramadhani. Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

 

[Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.]   [Al-Baqara:185]

Amesema ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake siku mbili hizi Mtume amekataa kufunga yaani Iddul-fitr (baada ya mwezi wa Ramadhani) na Idul-Adhha (Baada ya Hajj).

Amepokea Anas Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume alikwenda Madina na walikuwa wana siku mbili za kucheza, Mtume akasema:

 

إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَبْدَلَكُمْ بِهِمَا خَيْرًا مِنْهُمَا ، يَوْمَ الأَضْحَى وَيَوْمَ الْفِطْرِ]    رواه أحمد]

 

[Hakika Mwenyezi Mungu amekubadilishieni siku mbili hizo kwa Iddul-fitr na Iddul Adhha].     [Imepokewa na Ahmad]

Siku ya Iddi ni siku ya mapambo. Imepokewa kwa Ibnu ‘Umar kuwa alinunua juba sokoni akamuuzia Mtume kuwa ajipambe nalo siku ya Iddi, Amepokea Anas Ibnu Malik kuwa Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam amesema:[Haendi kuswali swala ya Iddul-fitr mpaka ale Tende].

Hukumu ya Utoaji wa Sadaka ya Fitri

Amepokea Ibnu ‘Abbas  Radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume amefaradhisha Zakatul-fitri kumtakasa aliyefunga kutokana na michezo, pia kuwa ni chakula cha maskini. Mwenye kutoa kabla ya swala basi ametoa zaka na atakayetoa baada ya swala basi hio ni sadaka miongoni mwa sadaka.

Kupiga Takbir za Iddi

Asili ya jambo hilo Neno lake Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

 وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ}      البقرة:185}

 

[Na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.]   [Al-Baqara:185]

Imepokewa na Ibnu ‘Umar  Radhi za Allah ziwe juu yake akisema kuwa: [Mtume alikuwa akipiga Takbiri alipo kwenda kuswali swala ya Iddi].


Sikiliza Mada hii na Sheikh Yusuf Abdi



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6573173
TodayToday1240
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 14

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828805165f2c14425291671747484753
title_682880516609220070414281747484753
title_68288051661f620077692031747484753

NISHATI ZA OFISI

title_6828805172bb817862585991747484753
title_6828805172c9f19696253711747484753
title_6828805172d752060209851747484753 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 13 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com