UMUJO KATIKA UISLAMU.
Baada ya kumuhimidi ALLAH na kumsifu na kumuombea rehma na amani kipenzi chake kiongozi wa waumini mtume wetu Muhammad ﷺ na jamaa zake na maswahaba wake na kila aliefuata mwenendo wake mpaka siku ya malipo.
Kwa hakika maudhi hii ya umoja katika uislamu au waislamu kuwa kitu kimoja ,nimoja kati ya maudhui muhimu sana haswa katika zama hizi tunazo ishi ,japo sio maudhui (geni ) mpya kuzungumzwa au hata kuandikwa imezungumzwa na wengi na kuandikwa pia na wengi na kila mmoja kwa namna yake na kwa misingi alio itegemea.
wapo walio andika wakiwa wamebebwa sana na hisia za kutaka tuwe kitu kimoja bila ya kuzingatia misingi na kanuni za kisheria zinazo weza kutuweka pamoja , wakawa na matarijio na matamanio yasio weza kufikika kwa kuutaka umoja..wakalisimamia la umoja kwa kuyahusisha makundi mbali mbali yenye mitazamo tofauti kati ya wenye kufuata muongozo wa Qur'ani na Sunna ya bwana Mtume ﷺna yale ambayo yako kinyume na msimamo huo wakawa na matumaini ya kuyaunganisha kuwa kitu kimoja kwa lengo la kutaka umoja wa waisilamu wakiamini kuwa haya tulio tafautiana ni mambo madogo tu na sio misingi katika dini na haya hayana athari lau tukawa pamoja.
Na wapo wenye kulingania umoja kwa ku ufunga katika mazingira madogo kwa namna ambao unaonekena kama ni jambo lisilo wezekana ispokuwa kwa nafasi ndogo mno.
Na kati ya hawa na hawa wapo wenye kulingania umoja kwa elimu na ujuzi na uadilifu,wana walingania umma kuwa kitu kimoja na kuisimamia haki ,wakalipa uzito jambo la kumfuata na kumtii kiongozi na jambo la kuwa kitu kimoja pamoja na kuzingatia kanuni na misingi ya itikadi na ya kisheria .
MAKUSUDIO YA UMJOJA KATIKA UISLAMU
Umoja katika uislamu : ni mkusanyiko wa wanao jinasibisha na uislamu kwa misingi na kanuni za kisheria kupitia muongozo wa bwana mtume na wema walio tangulia, kwa lengo la kuisambaza dini na kukiinua kila cha
لاإله الا الله محمد رسول الله
na kuithibitisha makusudio ya aya katika Qur'ani:
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ آل عمران:110
[nyinyi ni umma bora muliotolewa katika watu ,muna amrishana mema na kukatazana mabaya na munamuamini mwenyezimgu, na lau wange amini waliopewa kitabu ingekuwa ni bora kwao,katika wao wapo waumini na wengi wao ni mafasiki]. [Al Imraan:110]
Kwa hakika Allah amewasifu wamunini katika aya hii tukufu kwamba wao ni umma bora na lililo wapa ubora huu ni hizi sifa tatu ..kuamrishana mema …kukatazana mabaya…kumuamini mwenyezimgu, na maneno yote haya yamekuja kwa sifa ya ujumla ,hili linatuonyesha umuhimu wa umoja wao na kuafikiana kwao katika misingi ya dini.
Na umma kama aliovo uchambua AL mannawiy ..(kila umma walio jikusanya katika jambo Fulani ..sawa likiwa la kidini, au zama au sehemu moja ,sawa sawa ikiwa ni jambo la lazima au la kujichagulia.
Umma ulio jichagulia ni kila jamnii uliojikusanya katika imaani ya dini au dhehebu kama umma wa kiislamu au umma wa kiyahudi au umma wa kinaswara. ALLAH anasema akimfahamisha Mtume wake
[فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَـؤُلاء شَهِيداً} [سورة النساء: 41}
[Basi itakuwaje pindi tukiwaleta kutoka kila umma shahidi , na tukakutaka wewe kuwa shahidi wa hawa?. ] [Annisaa:41]
Kwa hio waislamu ni umma mmoja kwa kuafikiana kwao katika misingi ya itikadi na ya kisheria japo wakitafautiana katika juziiyati (mambo yasio kuwa misingi).
Itaendelea…
Imeandikwa na. Hussein ali Omar swidiq
+255717755358 This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.