Menu

HAKI YA MUISLAMU JUU YA MUISLAMU MWENZAKE


642


Uislamu ni dini kubwa imeweka muongozo ambao kwamba inakusanya haki na uwajibikaji, miongoni mwa haki hizo ni haki ya Muislamu juu ya Muislamu mwenzake. Lengo kubwa ya haki hizi ni kuleta mapenzi na udugu wa kiislamu. Kila Muislamu akijua haki yake na ya mwenzake, basi itakuwa ni wepesi Waislamu kushikamana na kuwa kitu kimoja.

 

UHAKIKA WA UDUGU KATIKA DINI 

Umma wa kiislamu leo umekuwa kama povu la bahari, umevunjika nguvu zake na kuwa wanyonge. Na ulimwengu hauna heshima isipokuwa watu wenye nguvu. Na sababu ya kudhoofika umma wa kiislamu ni kufarikiana kati yao. Na nguvu ni matunda ya umoja na mapenzi na haukudhoofika umma huu ila baada ya kukosa umoja nao ni udugu.
Uhakika wa udugu ni pale Mtume alipounganisha maswahaba walipokuwa Makkah pamoja na kuhitalifiana rangi zao na maumbile yao na ndimi zao na malengo yao ya maisha. Amemuunga Hamza ambaye ni mkureishi na Salman ambaye ni mfursi na Bilal ambaye ni mhabasha na Suheib ambaye ni mrumi na wote wakawa wanaimba qaswida hii: Uislamu ndio baba yangu Wakijifakhiri kwa kabila la Qais au Tamim. Na wote walikuwa karibu na Neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:

 

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ}   الحجرات:10}

 

[Kwa hakika Waislamu wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na Mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe].  [Al-Hujuraat:10]
Hii ndio daraja ya kwanza katika udugu wa kiislamu, kisha Mtume ﷺ akaunganisha watu wa Madina amabao ni kabila la Aus na Khazraj baada ya kupigana vita muda mrefu kati yao.
Kisha Mtume akaunganisha watu wa Makka (waliogura) na watu wa Madina. Kulipatikana tukio ambalo halina mfano kwa mwanadamu. Amepokea Anas hadithi akisema:
[Alikuja AbdurRahman bin ‘Auf kwa Mtume ﷺ akamuunga na Sa’ad bin Rabiya na alikuwa na mali nyingi, akasema Sa’ad: nitakugawiya nusu ya mali yangu na nitakupatia mmoja kati ya wake zangu. Tazama anayekupendeza zaidi nimuache. Akasema AbdurRahman Mwenyezi Mungu akubariki, (nionyeshe soko)].
Kwa sasa hatuwezi kupata mfano wa Sa’ad!?. Mmoja wa watu wema alisema: Wako wapi wanaotoa mali yao usiku na mchana, siri na dhahiri akajibiwa: Wameenda pamoja na wasioomba watu wakafanya ung’ang’anizi.
Haki ya Muislamu juu Muislamu mwenzake ni kumpenda kwa ajili ya Mungu. Amepokea Anas Bin malik akisema :
[Mambo matatu mtu akiwa nayo anapata imani; moja wapo ni kumpenda mtu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu].

 

MIONGONI MWA HAKI YA MUISLAMU JUU YA MUISLAMU MWENZAKE

Kutembeleana kwa lengo ya kujuana hali. Amepokea Abu Huraira hadithi kutoka kwa Mtume akisema: [Mtu alimtembelea ndugu yake katika kijiji kingine Mwenyezi Mungu akamtuma Malaika kwa sura ya binadamu, akamuuliza waenda wapi? Akasema: naenda kumtembelea ndugu yangu. Akasema: Je ana neema unayotarajia (kutoka kwake)? Akasema: Hamna neema yoyote, isipokuwa nimempenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Akasema Malaika: Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu nimetumwa kwako. Jua Mwenyezi Mungu anakupenda kama unavyompenda ndugu yako].
Kuitikia Salamu. Amepokea Abu Dawud akisema Mtume :

 

لا تدخلون الجنة حتى تؤمنوا ولا تؤمنوا حتى تحابوا أولا أدلكم على شيء إذا فعلتموه تحاببتم أفشوا السلام بينكم]   رواه مسلم]

 

[Mguu hautoingia peponi mpaka muamini, na hamtomuamini mpaka mpendane. Je Nikujulisheni jambo mkilifanya mtapendana? Toleaneni salamu kati yenu]. [Imepokewa na Muslim]
Kufuata janeza na kwenda mazikoni. Amepokea Abu Huraira hadithi kutoka kwa Mtume akisema:

 

حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ سِتٌّ قِيلَ مَا هُنَّ يَا رَسُولَ اللَّهِ : قَالَ إِذَا لَقِيتَهُ فَسَلِّمْ عَلَيْهِ وَإِذَا دَعَاكَ فَأَجِبْهُ وَإِذَا اسْتَنْصَحَكَ فَانْصَحْ لَهُ وَإِذَا عَطَسَ فَحَمِدَ اللَّهَ فَسَمِّتْهُ وَإِذَا مَرِضَ فَعُدْهُ وَإِذَا مَاتَ فَاتَّبِعْهُ    رواه مسلم

 

[Haki ya Muislamu juu ya Muislamu mwenzake ni sita akalizwa ni zipi ewe Mtume wa Mungu ? akasema kumsalimu pindi ukikutana nae, kuitikia wito anapo kuita, kuchukua nasaha yake anapo kunasihi, akichemua na akamuhimidi Mwenyezi Mungu kumuambia Mwenyezi Mungu akurehemu, kumtembelea anapokuwa mgonjwa, kumzika anapokufa]. [Imepokewa na Muslim]

Kutokuwa na chuki. Anas amepokea hadithi kutoka kwa Mtume :

 

لا تباغضوا ولا تحاسدوا ولا تدابروا ولا تقاطعوا وكونوا عباد الله إخواناً]      رواه مسلم]

 

[Msichukiane, wala musihusudiane,musipeane migogo, wala Musikatane kueni ndugu katika waja wa Mwenyezi Mungu]. [Imepokewa na Muslim]
Hasadi ni maradhi hatari jee huridhiki kwa aliyegawanya riziki ambaye ni Mwenyezi Mungu. Inapaswa kumuomba Mwenyezi Mungu yeye ndiye mtoaji. Amesema Mwenyezi Mungu :

 

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ }    الحشر:10}

 

[Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Tusamehe sisi na ndugu zetu waliotangulia katika Uisalmu].     [Al-Hashri:10]
Amepokea Anas akisema: Ilikuwa tumekaa pamoja na Mtume makasema Mtume:
[Atakuja mtu wa peponi, akatokea mtu wa Answaar ndevu zake zilikuwa safi, na ameshika vitu vyake kwa mkono wa kushoto. Na siku ya pili Mtume akasema hivyo hivyo, na akatokea mtu yule yule hata siku ya tatu. Abdullah bin Amru akamfuata nyumbani kwake na akawa naye muda wa siku tatu, wala hakumuona akisimama usiku isipokuwa akishtuka usiku humtaja Mwenyezi Mungu katika kitanda chake mpaka ikifika swala ya alfajiri. Na alikuwa hamsikii isipokuwa akizungumza maneno ya kheri. Akamsimulia ‘Abdallah Bin ‘Amru sababu ya kumfuata kwa kuwa wewe ni mmoja kati ya watu wa peponi. Akasema: sina chuki na Muislamu yoyote].
Kumsaida Muislamu mwenzake akiwa na shida. Amesema Mtume :

 

مَن نفَّس عن مؤمنٍ كربةً من كُرَب الدنيا، نفَّس الله عنه كربةً من كُرَب يوم القيامة، ومن يسَّر على معسرٍ، يسَّر الله عليه في الدنيا والآخرة، ومن ستر مسلمًا ستره الله في الدنيا والآخرة     رواه مسلم

 

[Mwenye kumsaidia Muislamu kwa kumuondoshea shida. Menyezi Mungu atamsaidia kumuondoshea shida ya siku kiyama. Na mwenye kumfanyia wepesi mtu mwenye uzito. Mwenyezi Mungu Atamfanyia upesi duniani na kesho akhera. Na mwenye kumsitiri ndugu yake Muislamu duniani na kesho akhera, Mwenyezi Mungu Atamsitiri dunuani na kesho akhera]. [Imepokewa na Muslim]

Kumnusuru Muislamu sawa akiwa amedhulumu au amedhulumiwa. Amesema Mtume :

 

انصر أخاك ظالماً أو مظلوماً، فقال: رجل يا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنصره إذ كان مظلوماً، أفرأيت إذا كان ظالماً كيف أنصره؟! قال: تحجزه أو تمنعه من الظلم، فإن ذلك نصره     رواه البخاري

 

[Mnusuru ndugu yako anayedhulumu au anayedhulumiwa. Akasema mtu: ewe Mtume wa Mungu tunamnusuru anayedhulumiwa, lakini vipi tunamnusuru anayedhulumu? Akasema Mtume: ni kumzuia anapodhulumu huko ndiko kumnusuru kwake].   [Imepokewa na Bukhari]

Kusitiri aibu ya Muislamu na kumuombea Mungu msamaha kwa kosa lake. Kwani Muisalmu si Malaika wala si nabii kwani yeye ni mwanadamu.

Wamesema wanavyuoni: Watu ni aina mbili:-
Watu wanaojulikana kwa wema na kuepukana na maasi, basi wakikukosea unapaswa kusitiri na kutofunua aibu yake.
Watu wanaofanya maasi kwa uwazi wala hawamuonei haya Mwenyezi Mungu, hao ni waovu.
Kwa hivyo linalo takikana kwa kila Muisalmu achunge haki ya Muislamu mwenzake ili jamii zetu ziishi katika mazingara bora na kuishi kama Mwenyezi Mungu alivyo taka tuishi kwa Upendo na Mahaba ili tupate radhi zake ALLAH


SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SWADI ALI



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6490191
TodayToday84
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 4

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6770f84e317c812065941051735456846
title_6770f84e3190c16320730831735456846
title_6770f84e31a5410020816921735456846

NISHATI ZA OFISI

title_6770f84e338e115151405331735456846
title_6770f84e33a0414737285461735456846
title_6770f84e33b1f12669329971735456846 Add content here

HUDUMA MPYA

: 8 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com