Menu

Sehemu ya Jamii


UMOJA WA KIISLAMU SEHEMU YA TATU


umoja2


Tulizungumza katika sehemu ya pili mambo yenye kutilia nguvu umoja wa kiislamu ,tukasema kuwa ni umoja katika itikadi (imani ) na tukafafanua kwa kadri tulivo afikiwa na mwenyezimgu sub hana hu wa taala.

Leo tukizungumzia jambo lengine lenye kutilia nguvu Umoja katika Uislamu;


UMOJA WA SHERIA NA SHAAIR (ALAMA ,NEMBO, VITAMBULISHI)

Ukitazama mambo yote wanao yafanyia kazi waislamu katika mambo yao ya kiibada utaona kuwa hakuna tofauti katika misingi ya utekelezaji wa mambo yenyewe, vilevile katika mambo ya kuhukumiana kwao.Mwenyezi Mungu anasema:

 

{شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ}

[Allah anasema :amekuamrisheni dini ile aliyo muusia nuhu na tulio kufunulia wewe ,na tulio wausia Ibrahim na musa na issa ,kwamba shikamaneni na dini wala msifarikane kwayo.]    [shuraa: 13]

Anasema Sheikh Al Saady Allah amrehemu:"Na miongoni mwa ijtimai katika dini ni kuto tafautiana ni yale mambo yalio amrishwa na sharia katika mikusanyiko ya pamoja kama mikusanyiko ya ibada ya hajj ,idi mbili ,swala tano ,na jihad na mengineo katika mambo ya ibada ambayo hayawezi kukamilika ispokuwa kwa kuwa pamoja".
Allah ameweka sheria kwa waislamu katika dini mambo ambayo yatakuwa ni yenye kuwakurubisha waumini kwa mola wao na kumtukuza ,miongoni mwa sheria hizo tukufu ni nguzo tano za uisilamu, kama ilivo pokewa na ibnu umar anasema ,anasema Mtume :

 

[بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ : شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ]

 

[Uislamu umejengwa kwa mambo matano, shahada mbili , swala ,zaka, hajj na swaumu ya mwezi wa ramadhani.]       [imepokewa na Bukahri]

Na nguzo hizi tano zina muhusu kila Muislamu na Allah ameweka sheria kwa nguzo hizi ili kuthubitisha nguvu za Umma wa Kiislamu na mshikamano na kusaidiana kati yao.kama ambavyo sheria hizi ni upeo wa uzuri na uwadilifu na umoja kwa lengo la kuwapangia maisha na kupata mafanikio ya maisha ya Duniani na Akhera kwa Wanaadamu.
Pindi unapo tazama malengo matukufu ya sharia utaona kwa ujumla wake yapo kwa lengo la kuyathibitisha maslahi ya Umma wa Kiislamu kwa upande wa nguvu ,Umoja na kusaidiana kati yao, kwa mfano miongoni mwa malengo ya kuwekwa Sharia ya vita ni kuwasaidia wanyonge na kuondosha dhulma kati ya wanaadamu ,Allah anasema katika Qur'ani Tukufu:

 

وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا

 

[Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako]      [Al Nnisaa:75]

Pia ukiitazama Ibada ya zaka utaiona kuwa ni faradhi inao wahusu wana jamii inaotoka katika nyoyo za Matajiri kwa lengo la kuwatakasa na uchoyo na ubakhili na kuyasafisha Mali yao,na hii ni njia pekee ilio faulu katika kupambana na ufukara ulio kithiri katika miji.
Vilevile katika utekelezaji wa ibada ya Swala kwa pamoja pia ibada ya Hajj ambapo Mahujaji wote wanaitikia mwito wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa sauti moja wakiwa katika viwanja vya Minaa na Arafa bila ya kutafautisha kati ya kiongozi (mfalme ) na raia na kati ya mweupe na mweusi na kati ya muarabu na asiekuwa muarabu.
Na katika kuzifanyia kazi Sharia hizi za Uislamu hakuna tofauti kati ya Mke na Mume,au Mkumbwa na Mdogo au kati ya Muungwana na Mtumwa,wote wapo sawa mbele ya Sharia ya Mwenyezi Mungu.kama ilivo pokewa katika hadithi ya Aisha kuhusu mwanamke wa kabila la Quraishi alieiba ,likawa kubwa jambo lake kwa kuwa atapishiwa hukumu ya kukatwa mkono na yeye ni mwanamke mtukufu jamaa zake wakamtuma Usama ili awaombee kwa bwana Mtume hukumu hii iondoshwe kwa huyu mwanamke …Mtume akakasirika mno akasema :

 

إِنَّمَا أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ أَنَّهُ إِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ , وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ قَطَعُوهُ , وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَوْ كَانَتْ فَاطِمَةُ ابْنَةُ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا

 

[hakika waliangamia walio pita kabla yenu alipo kuwa akiiba Mtukufu kati yao wakimuacha na anapo iba Mnyonge (asiekuwa na hadhi katika jamii) wakimsimamisha hukmu ,Wallahi napa kwa jina la Mwenyezimgu lau kama Fatima binti yangu angekuwa ndie alie iba ningemkata mkono wake.]    [imepokewa na Muslim]

Hii ndio sharia ya Mwenyezi Mungu imekuja kwa ajili ya Maslahi ya watu wote..
Itaendelea katika sehemu ya nne inshallah…

Imeandikwa na Hussein Ali Omar Swidiq

+255 717755358…+254 733666396



UMOJA KATIKA UISILAMU SEHEMU YA PILI


55oma ohda


Tukiendelea na mfululizo wa mazungumzo yetu tulikomea kwenye maneno haya (Kwa hio waislamu ni umma mmoja kwa kuafikiana kwao katika misingi ya itikadi na ya kisheria japo wakitafautiana katika juziiyati (mambo yasio kuwa misingi )….inaendelea

swala litakalo jitokeza, jee ni yapi mambo ambao Waislimu wakiyafanya watautilia nguvu uislmau wao na itakuwa ni sababu ya kupatikana kwa umoja?
Miongoni mwa mambo hayo ni kama yafuatavyo :
1) Kuwa na Itikadi moja .
Itikadi za waisilamu kwa upande wa kumuamini kwao mwenyezi Mungu ni moja kama ilivyo katika misingi ya imaani (nguzo za imani) hakuna tofauti kati yao katika misingi hii ,wote wana amini upweke wa mwenyezimgu (الله وحدانية) uwepo wa Malaaika ,wanaamini Vitabu walivyo teremshiwa manabii walio tangulia,wana amini mitume na manabii walio tangulia,wana amini uwepo wa siku ya mwisho ( siku ya malipo ) na vile vile wanaamini kadar kuwa kheir na shari zinatoka kwa mwenyezimgu. kama mwenyezimgu alivyo lizungumzia hilo katika Qur’ani kwenye sura ya pili aya 285.

Na kama vile ilivyo kuja katika mapokezi mengi sahihi kutoka kwa bwana Mtume akilithibisha hilo.
Na hii ndio itikadi ya waislamu wote katika zama zote na yeyote atakae pinga moja katika misingi hio atakuwa ametoka katika mila ya Mislamu ,Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’ani:

[ومن يَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِط عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ}  [سورة المائدة: 5}

 

[Na yeyote atakae kataa kuamini bila shaka amali yake imepotea naye katika akhera atakuwa mioangoni mwa wenye khasara]    [Al Maida:5]

Ibnu abasi anasema katika kutafsiri maneno haya

Yaani kukataa kuamini ni kule kutoamini aliyo teremshiwa Mtume ﷺ.

Kwa maana hiyo yoyote katika Waislamu akawa na imani tofauti na misingi hii ima akazindisha lolote katika haya au akapunguza chochote hazingatiwi kuwa ni katika Waislamu hata akawa na muonekano wa uislamu .
Kama mfano kwa wale wanao amini kwenye nguzo hii ya kwanza ya imani ambao ni kuamini upweke wa Allah katika kumfanyia yeye ibada,wao wakaigeuza imani hii kuwa msingi wa kukubaliwa matendo ya mwanadamu ni kuamini uwepo wa Maimamu kumi na mbili …wakawafanya maimam hawa ni wasila baina ya mja na mola wake na kwamba Maimamu wana uwezo wa kuweka sheria ya kuhalalisha au kuharamisha.
Kwenye imani ya kuwepo kwa malaika sisi tunaamini kuwa malaika ni viumbe wa Allah wameumbwa kwa Nuru hawamuasi mola kwa lolote na wana fanya walio amrishwa..lakini wao wana amini kuwa malaika wameumbwa kutokana na nuru ya maimamu kumi na mbili na wao (malaika ni watumishi wa maimamu) "Mwenyezi Mungu aliumba kutoka kwenye Nuru ya uso wa Ali Bin Abii Twalib Radhi za Allah Malaika elfu sabiini wakimtakia yeye msamaha na kuwatakia vipenzi vyake ." Biharul anwar 23/320.
Na mengine mengi ambao yapo kinyuma na misingi ya imani.

Kwa hio ili kuupata umoja wa kiislamu kwanza tushikamane kwenye msingi huu wa imani…itaendela…
imeandikwa na

Hussein Ali Omar Swidiq +255717755358.


 


ZAKA NA FAIDA YAKE KATIKA JAMII


 show 3


Je, waijua ibada ya kutoa mali yako wewe Muislamu? Je, wajua kwamba ibada hii ukiifanya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Atakuzidishia baraka katika mali yako hapa duniani na malipo makubwa kesho Akhera? Je, hujui kwamba mali uliyonayo ni mali ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) na Amekupa mtihani katika mali hayo? Je, watarajia kufaulu mtihani huo?.
Mtu akitioa mali yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), mali yake huzidi na kupata malipo makubwa kwa Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Taala) na ni nguzo ya tatu katika Uislamu si nyingine nayo ni zaka. Ni wajibu wa kila Muislamu mwenye mali yaliyofika kiwango kutoa fungu maalum. Mola (Subhaanahu wa Taala) amesema ndani ya Qur’an tukufu:

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ}     النور:56}

 

[Na simamisheni Swala na mtoe Zaka na mumtii mtume huenda mukarehemewa]    [Al-Nnuur:56]
Na katika hadithi za Bwana Mtume amesema:

 

بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان .    رواه البخاري ومسلم

 

[Uislamu umejengwa na mambo matano; kupwekeshwa Mwenyezi Mungu, kusimamisha Swala, kutoa Zaka, na kufanya hija na kufunga mwezi wa Ramadhani.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Yamekuja maonyo mbali mbali na tahadhari kwa Muislamu katika suala nzima la kuikwepa Zaka na kufanya ubakhili wa kutekeleza ibada hiyo. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameahidi adhabu kali kwa kila ambaye haitekelezi ibada hii tukufu. Amesema Mola Subhaanahu wa Taala:

 

وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلِلَّهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ     آل عمران:180

 

[Na wala wasidhani wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni bora kwao. La ni vibaya kwao. Watafungwafungwa kwa yale waliyofanyia ubakhili Siku ya Kiama, na urithi wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ana khabari za yote mnayoyafanya]      [Al-Imraan:180] .


Vile vile Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:


وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ ۖ هَٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ     التوبة:34-35 

[Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.Siku zitapo tiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mlio jilimbikia nafsi zenu, basi onjeni mliyo kuwa mkilimbika]      [Al-Ttawba:34-35]

 

FAIDA ZA ZAKA KWA UPANDE WA TABIA

 

Zaka ina faida nyingi sana, nyingine za kidini, za kitabia na pia faida za kijamii.

1. Kwanza Kutoa Zaka ni kusimamisha nguzo, katika nguzo za Uislamu ambayo ni sababu ya utukufu duniani na kesho akhera.
2. Zaka zinamkurubisha mja kwa Mola wake na zinamzidishia mtu imani.
Mtu atoapo zaka hupata ujira na malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Asema Mola Subhaanahu wa Taala:

 

يَمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ}   البقرة:276}

 

 

[Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.]      [Al-Baqara:276]
3. Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala humfutia madhambi Muislamu atoapo zaka. Mtume Amesema:

 

 

والصدقة تطفئ الخطيئة كما يطفئ الماء النار]    رواه الترمذي]

 

[Na sadaka(zaka)inaondosha maovu kama maji yanavyozima moto]    [Imepokewa na Tirmidhiy]

 

FAIDA ZA ZAKA KWA UPANDE WA TABIA

 

Na miongoni mwa faida za kitabia:
1. Kutoa zaka inamuweka mtu katika kundi la watu wakarimu na wenye kujali maslahi ya watu,
2. Kutoa zaka kunamfanya mtu kusifika na sifa ya huruma na upole kwa ndugu zake.Kwani Waislamu wenye huruma Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) pia huwahurumia.
3. Kutoa zaka kunasafisha vifua vya watu wenye kupewa mali ile na watampenda mtoaji kwa kule kuwajali ndugu zake na kuwasaidia.
4. Kutoa zaka kunamsafisha mtoaji na sifa ya ubakhili na uchoyo. Na tabia mbaya hii ya ubakhili ni miongoni mwa tabia mbaya ambazo haitakiwi Muislamu kujipamba nayo. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema katika kitabu chake kitukufu:

 

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ}   التوبة:103}

 

[Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.]    [Al-Ttwaba:103]

 

FAIDA ZA ZAKA KWA UPANDE WA JAMII

 

Na miongoni mwa faida za kijamii katika kutoa zaka:
Kutoa zaka huwaondolea watu matatizo ya kiuchumi waliyonayo na kama illvyo ni kwamba wanaohitajia ni wengi.
Kutoa zaka hutilia nguvu mambo ya Waislamu wanayotaka kuyafanya kwa mfano kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala).
1. Zaka huondoa chuki baina ya maskini na matajiri na kuleta mapenzi baina yao.
2. Zaka hukuza mali na kuyazidisha na kuwa na baraka. Amesema Mtume : [Haipungui mali inayotolewa zaka].
3. Kutoa zaka hueneza mali baina ya watu na haibaki kwa matajiri bali huzunguka kati yao.
Na hizi faida tulizozitajaza ziwe ni za kijamii au za kidini au za kitabia zinaonesha kwamba kutoa zaka ni jambo muhimu sana na dharura Ili kutengeneza nafsi ya mtu na jamii kwa ujumla.
Kutoa zaka kuna athari katika nafsi ya mtu na jamii kwa ujumla. Kwani kutoa zaka ndio nidhamu ya kwanza waliyoijua watu katika kuwasaidia wanaohitaji na uadilifu katika jamii nzima ya kiislamu. Kwani mali inatoka katika tabaka ya matajiri na kwenda katika tabaka ya maskini na wanaohitajia. Ukweli ni kwamba zaka inasafisha mali ya mtoaji na kuikuza kama ambavyo inamtakasa moyo wa mtoaji zaka kutokana na tabia ya ubakhili, tamaa na kutojali wanaohitajia. Vilevile inasafisha moyo wa anayepewa zaka kutokana na tabia mbovu ya uhasidi na chuki kwa mwenye mali.
Tukiangalia vyema pia kutoa zaka kunazidisha mshikamano kati ya jamii inayoishi pamoja na kuondoa umaskini na pia kuangamiza matatizo ya kijamii, kiuchumi na ya kitabia endapo itatolewa na kupewa wanaostahili.

 

MALI YANAYOTOLEWA ZAKA

 

Miongoni mwa mali ambayo hutolewa zaka ni dhahabu, fedha kwa sharti ifike kiwango na wajibu ni robo ya kumi ya dhahabu au fedha.Na katika mali ambayo ni lazima kutolewa zaka ni bidhaa za biashara nazo ni kila kilichofanyiwa biashara kwa mfano:majumba, magari, nafaka, mifugo, vitambaa na vyingenevyo. Na ni wajibu kutoa katika mali tuliyo yataja robo ya kumi.

Ama vitu vilivyoandaliwa kwa matumizi ya kawaida kama Magari ya matumizi, Majumba ya kuishi na vitu mfano wa vitu hivi havitolewi Zaka. Kwa neno la Mtume :

 

ليس على المسلم في عبده ولا فرسه صدقة]    رواه البخاري]

 

[Halazimiki Muislamu kwa mtumwa wake wala farasi wake zaka].  [Imepokewa na Bukhari]

 

WANAOSTAHIKI KUPEWA ZAKA

 

Miongoni mwa watu wanaostahiki Kupewa zaka Mwenyezi Mungu aliyetukuka amewataja watu sampuli nane ndani ya Qur’an Tukufu Aliposema:

 

{إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ}

 

[Hakika zaka hupewa mafukara na maskini na wanazikusanya na waliosilimu karibu na watumwa na wenye madeni na katika jihadi na kupewa msafiri zaka hii ni faradhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikma.]    [Al-Ttwawba:60]

Nachukue tena nafasi hii kuwafafanulia aliyowataja Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) katika wanaostahiki kupewa zaka.

 

WANAOSTAHIKI KUPEWA ZAKA

 

1. Fukara: ni mtu ambaye hapati cha kumtosha isipokuwa kidogo chini ya nusu.Kwa hivyo ikiwa mtu hapati cha kujisimamia yeye na familia yake nusu mwaka basi huyo ni fukara. Kwa hiyo atapewa cha kumtosha yeye na familia yake mwaka mzima.

2. Maskini: ni mtu ambaye anapata cha kumtosha nusu na zaidi lakini hapati cha mwaka mzima kwa hiyo hupewa zaka ili kumkamilishia mahitaji.

3. Wenye kukusanya zaka: ni wale ambao wanamuwakilisha kiongozi kwa kukusanya mali ya zaka kutoka kwa wenye mali na kuwapelekea wanaostahiki na kuyahifadhi.

4. Waliosilimu karibu: hawa hupewa ili kuzitia nguvu imani zao hatimaye wawe walinganizi wa dini ya kiislamu na kuwa mfano mzuri.

5. Mtumwa: anaingia katika tamko hili ni mtumwa ambaye husaidiwa kujikomboa kwa mali ya zaka.

6. Wenye madeni: endapo hawana cha kulipa madeni yao na wenye madeni watapewa kile cha kulipa madeni yawe madeni yao ni mengi au machache.

Hata kama wanao uwezo wa kujitafutia chakula lakini hawezi kulipa.

7. Kutoa zaka katika jihadi: hutolewa katika jihadi kinachowatosha wapiganaji katika vita kununulia silaha na matumizi mengine ya kivita.

8. Msafiri: ni msafiri aliyekatikiwa na safari. Msafiri hupewa mali ya zaka ili ziweze kumfikisha mjini kwake anakokwenda.

Na hawa ndio ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewataja kwenye Kitabu Chake, na Akaelezea kwamba ni lazima kutekelezwa ibada hii kwa ajili yake. Wala haifai kutolewa zaka katika sehemu nyingine kwa mfano; kujenga Misikiti, kutengeneza njia, kuchimba visima na mengineyo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu Amewataja Mwenyewe wanaostahiki na wasiokuwa wao haifai kabisa kupewa zaka.

Mwisho

Kuitekeleza nguzo hii ni kumsafisha mtoaji kutokana na sifa ya ubakhili na madhambi. Pia ni kutakasa mali yake na kuzidisha baraka kwa kutoa zaka, kuondoa chuki na uhasidi katika nafsi za wenye kupokea zaka, bali kuleta mapenzi kati ya tajiri na maskini.

Mwisho kabisa tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Atujaalie tuwe miongoni mwa wanaotekeleza ibada ya zaka, pia tunamuomba Ayabariki mali zetu, Atupe ujira mkubwa kwa tunachokitoa kesho akhera.


KWA FAIDA ZAIDI SIKILA MADA HII NA DR.MAJID HOBENI




UMUJO KATIKA UISLAMU.


show


Baada ya kumuhimidi ALLAH na kumsifu na kumuombea rehma na amani kipenzi chake kiongozi wa waumini mtume wetu Muhammad ﷺ na jamaa zake na maswahaba wake na kila aliefuata mwenendo wake mpaka siku ya malipo.
Kwa hakika maudhi hii ya umoja katika uislamu au waislamu kuwa kitu kimoja ,nimoja kati ya maudhui muhimu sana haswa katika zama hizi tunazo ishi ,japo sio maudhui (geni ) mpya kuzungumzwa au hata kuandikwa imezungumzwa na wengi na kuandikwa pia na wengi na kila mmoja kwa namna yake na kwa misingi alio itegemea.
wapo walio andika wakiwa wamebebwa sana na hisia za kutaka tuwe kitu kimoja bila ya kuzingatia misingi na kanuni za kisheria zinazo weza kutuweka pamoja , wakawa na matarijio na matamanio yasio weza kufikika kwa kuutaka umoja..wakalisimamia la umoja kwa kuyahusisha makundi mbali mbali yenye mitazamo tofauti kati ya wenye kufuata muongozo wa Qur'ani na Sunna ya bwana Mtume na yale ambayo yako kinyume na msimamo huo wakawa na matumaini ya kuyaunganisha kuwa kitu kimoja kwa lengo la kutaka umoja wa waisilamu wakiamini kuwa haya tulio tafautiana ni mambo madogo tu na sio misingi katika dini na haya hayana athari lau tukawa pamoja.
Na wapo wenye kulingania umoja kwa ku ufunga katika mazingira madogo kwa namna ambao unaonekena kama ni jambo lisilo wezekana ispokuwa kwa nafasi ndogo mno.
Na kati ya hawa na hawa wapo wenye kulingania umoja kwa elimu na ujuzi na uadilifu,wana walingania umma kuwa kitu kimoja na kuisimamia haki ,wakalipa uzito jambo la kumfuata na kumtii kiongozi na jambo la kuwa kitu kimoja pamoja na kuzingatia kanuni na misingi ya itikadi na ya kisheria .

MAKUSUDIO YA UMJOJA KATIKA UISLAMU

Umoja katika uislamu : ni mkusanyiko wa wanao jinasibisha na uislamu kwa misingi na kanuni za kisheria kupitia muongozo wa bwana mtume na wema walio tangulia, kwa lengo la kuisambaza dini na kukiinua kila cha

لاإله الا الله محمد رسول الله 

na kuithibitisha makusudio ya aya katika Qur'ani:

 

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ     آل عمران:110

 

[nyinyi ni umma bora muliotolewa katika watu ,muna amrishana mema na kukatazana mabaya na munamuamini mwenyezimgu, na lau wange amini waliopewa kitabu ingekuwa ni bora kwao,katika wao wapo waumini na wengi wao ni mafasiki].    [Al Imraan:110]

Kwa hakika Allah amewasifu wamunini katika aya hii tukufu kwamba wao ni umma bora na lililo wapa ubora huu ni hizi sifa tatu ..kuamrishana mema …kukatazana mabaya…kumuamini mwenyezimgu, na maneno yote haya yamekuja kwa sifa ya ujumla ,hili linatuonyesha umuhimu wa umoja wao na kuafikiana kwao katika misingi ya dini.
Na umma kama aliovo uchambua AL mannawiy ..(kila umma walio jikusanya katika jambo Fulani ..sawa likiwa la kidini, au zama au sehemu moja ,sawa sawa ikiwa ni jambo la lazima au la kujichagulia.
Umma ulio jichagulia ni kila jamnii uliojikusanya katika imaani ya dini au dhehebu kama umma wa kiislamu au umma wa kiyahudi au umma wa kinaswara. ALLAH anasema akimfahamisha Mtume wake


[فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِن كُلِّ أمَّةٍ بِشَهِيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هَـؤُلاء شَهِيداً}    [سورة النساء: 41}

 

[Basi itakuwaje pindi tukiwaleta kutoka kila umma shahidi , na tukakutaka wewe kuwa shahidi wa hawa?. ]     [Annisaa:41]
Kwa hio waislamu ni umma mmoja kwa kuafikiana kwao katika misingi ya itikadi na ya kisheria japo wakitafautiana katika juziiyati (mambo yasio kuwa misingi).


Itaendelea…
Imeandikwa na. Hussein ali Omar swidiq

+255717755358 This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.



KUUNGA KIZAZI


  501


Amesema Mtume Muhammad aliyesema [Hatoingia peponi anayewakata jamaa zake].
Na jamaa ya mtu ni mamake, babake, watoto wake na kila ambaye karibu naye kinasaba.
Aya na hadithi zinazozungumzia jambo hili ni nyingi hebu niwatajie baadhi. Mola (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

 

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ}    محمد:22

 

[Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa zenu?]  [Muhammad:22]
Mtume miongoni mwa mambo aliyoyalingania mwanzo ni kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuacha ibada za mababu, kuswali, kutoa sadaka, kujihifadhi na uchafu na kuunga jamaa. Na kuunga jamaa ni kuwafanyia wema na kutowaudhi. Pia ni katika kuwafanyia wema kuwapa nasaha, kuwapa ushauri, kuwapenda na kuwapendelea kheri, kuwafanyia uadilifu, kuwaelekeza, kuwafundisha, kuwapa haki zao za lazima na kuvumilia na kusubiri katika maudhi yao.

 

FADHLA ZA KUUNGA KIZAZI

 

Kuunga jamaa kuna fadhila nyingi na katika fadhila hizo ni kuzidishiwa mtu umri wake na vile vile kukunjuliwa mali yake. Amesema Mtume :

 

مَنْ سَرَّهُ أَنْ يُبْسَطَ لَهُ فِي رِزْقِهِ أَوْ يُنْسَأَ لَهُ فِي أَثَرِهِ فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Anayependa kukunjuliwa riziki yake na kurefushiwa umri wake basi aunge jamaa zake].   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Na kuunga jamaa kuna daraja kubwa katika Uislamu.
Je tumesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu? Je tumetekeleza amri zake? Je makemeo yake na makatazo umeyaepuka? Je twawafanyia wema jamaa zetu na tunawatembelea ?
Tunapo taka kheri duniani na kesho akhera tuungeni jamaa zetu na tukaeni nao vizuri.

 

FAIDA YA KUUNGA KIZAZI

 

1. Kuunga jamaa ni alama kubwa za ukamilifu wa imani.
2. Kuunga jamaa ni sababu ya kukunjuliwa mtu katika riziki.
3. Kuunga jamaa ni sababu ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

 

NASWAHA ZA WATU WEMA JUU YA KUUNGA KIZAZI

 

Wema waliotangulia wametoa wasia unaoonesha umuhimu wa kuunga jamaa. Amesema ‘Umar ibn Khattwab, Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Jifundisheni nasaba kisha muwafanyie wema jamaa zenu." Amesema ‘Atwaa ibn Abi Rabaa: "Kutoa dirham kumpa jamaa yangu inapendeza zaidi kuliko kutoa dirhamu elfu kumpa maskini, mtu akamuuliza: Hata kama jamaa yako ni tajiri? Akasema ‘Atwaa : Ndio, hata kama jamaa yangu ni tajiri"
Vile vile amesema Said ibn Musayyab Mwenyezi Mungu amrehemu hakika aliwacha Dinari kadhaa: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe wajua sikuyakusanya mali zangu isipokuwa kwa ajili ya kuhifadhi Dini yangu,. Hana kheri asiyekusanya mali yake kulipa deni lake na kuwafanyia wema jamaa zake”.
Ndugu katika Imani zama tunzao ishi tumeona namna Waislamu namna wanvyo katana na jamaa zao utapata ndugu hawaseshani wala hawajuni, nah ii ni hatari kubwa sana.
Niwajibu wa kila Muislamu kusimama na jukumu hili la kuunga kizazi chake ili awe ni mwenye kutekeleza Mamrisho ya Mwenzi Mungu na Mafundisho ya Bwana Mtume na apate radhi za Mwenzi Mungu na fadhla zake.

 

HASARA YA KUWAFANYIA UBAYA JAMAA ZAKO

 

1. Kuwakata jamaa ni miongoni mwa sababu za mtu kutoingia peponi. Mtume ﷺ Amesema ya kwamba:

 

لا يدخل الجنة قاطع]    رواه مسلم]

 

[Hatoingia peponi mtu anayewakata jamaa zake].   [Imepokewa na Muslim]
2. Kupata laana ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema kwenye Kitabu chake kitukufu:

 

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ}    محمد:22-23}

 

[Ndiyo yanayotarajiwa kwenu kuleta uharibifu katika ardhi na kuwakata jamaa zenu wakati mukipata ukubwa. Hao ndio waliolaaniwa na Mwenyezi Mungu Akawatia uziwi masikio yao na akayapofua macho yao.]     [Muhammad:22-23]

Na kosa kubwa kabisa ni mtu kuwakata wazazi wake wawili kisha akawakata walio karibu zaidi naye. Mtume ﷺ Amesema:

 

ألا أخبركم بأكبر الكبائر قالوا بلى يا رسول الله قال الإشراك بالله وعقوق الوالدين]    رواه البخاري]

 

[Je siwajulishi dhambi ambalo ni miongoni mwa madhambi makubwa kabisa? Wakasema maswahaba: Tujulishe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema Mtume ﷺ: [Kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwakata wazazi wawili].   [Imepokewa na Bukhari]

3. Kufanyiwa haraka mtu kuadhibiwa hapa duniani kabla kuadhibiwa kesho akhera. Amesema Mtume ﷺ:

 

 

 ما من ذنب أجدر أن يعجل الله لصاحبه العقوبة في الدنيا مع ما يدخره له في الآخرة من البغي وقطيعة الرحم]    رواه الترمذي وأبوداود]

 

[Hakuna kosa ambalo Mwenyezi Mungu analiharakisha zaidi adhabu yake kwa mwenye kulifanya duniani pamoja na kuwekewa adhabu nyingine akhera kuliko kuwakata jamaa na kufanya maasia].   [Imepokewa na Al Tirmidhiy na Abuu Daud]

DARAJA ZA JAMAA YAKO

 

Hakika jamaa wana daraja tofauti tofauti katika kuishi nao:

Jamaa wenye kushikamana na Dini na jamaa aina hii hufanyiwa wema kwa kule kushikamana kwao na Dini.
Jamaa ambao wazushi ni katika Dini na wenye kufanya maovu. Na hawa wamegawanyika vigawanyo viwili:-
Wanaotangaza bidaa na uzushi wao na maovu yao tena wanalingania kwenye uovu huo. Jamaa hao hupigwa vita kabisa kwa ajili ya kushikamana kwao na uovu. Inafaa kuwaonesha uso wa bashasha, lakini haifai kuwa nyoyo zetu haziko radhi nao moyoni kwa ule uovu wao. Ushahidi wa hilo ni kwamba Mtume ﷺ: [Alimwonesha bashasha ‘Uyaina ibn Hiswhiy aliyekuwa mtu muovu kabisa. Alipokuwa akibisha kwake huku akisema : Ni ndugu muovu katika jamii. Alipoingia Mtume alizungumza naye vizuri akasema: [Hakika tunawaonesha uso wa bashasha watu (waovu) na huku nyoyo zetu zawalaani].

Jamaa wafichao bidaa na vitendo vyao viovu, jamaa aina hii hufanyiwa muamala wa Waislamu wasiojulikana maovu yao.
Jamaa walio makafiri na wanafiki na jamaa aina hii wamegawanyika mara mbili:
Jamaa wanaoupiga vita Uislamu jamaa aina hii hukatwa na hauwaungwi kwa ajili ya kuogopwa shari lao.
Jamaa wasiopiga vita Dini yetu ya uislamu jamaa aina hii hufanyiwa wema kwa njia zifuatazo:
Kuwalingania katika Uislamu kwa njia nzuri.
Kuwaombea dua Mwenyezi Mungu Awaongoze katika Uislamu.
Kuwasaidia wanapokuwa na shida na kuwafanyia wema kuwavutia katika Uislamu.

Mwisho

Tufahamu ya kuwa Jamaa ni msingi wa jamii ya kiislamu, na jamaa ikishikamana, jamii itashikamana. Tukifanya hivyo, tutaweza kujenga umma mmoja wa kiislamu, na kuanzishwa kwa serikali ya kiislamu. Bila ya kujenga msingi wa jamaa moja, hatuwezi kufikia lengo la kurejesha Ukhalifa katika ardhi. Ni jukumu la kila Muislamu kufanya bidii kuunga jamaa yake na kujenga jamii ya kiislamu iliyoshikamana. Tunamuomba Allah atuwezeshe kurejesha umoja wa kiislamu na Atujaalie ni wenye kuwatendea wema jamaa zetu na tufaulu kuipata pepo yake.


Sikiliza Mada hii na Sheikh Uthman Shee (Mungu amrahamu)



LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487808
TodayToday914
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 66

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e6cb06b33019276927701735290032
title_676e6cb06b4347881895101735290032
title_676e6cb06b53316107244951735290032

NISHATI ZA OFISI

title_676e6cb06ce568415302421735290032
title_676e6cb06cf5318347166711735290032
title_676e6cb06d04d13191818431735290032 Add content here

HUDUMA MPYA

: 5 + 6 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com