Menu

DHANA MBAYA

753 5020tumblr m31vck1bKD1qcejh9o1 500

 

Miongoni mwa maafa yaliyowasibu watu na jamii ni dhana mbaya, jambo ambalo linakata mapenzi kati ya watu, na mwenye dhana mbaya huwaangalia watu kwa jicho ovu, na bila shaka dhana mbaya ni kinyume na sheria ya kiislamu.

Ili mafungamano baina yetu na watu yabaki kuwa ni imara ni kuwakabili watu hali ya kuwa nyoyo zetu zimesalimika pia kuwa safi na nyuso kuwa na bashasha na kuwadhania watu kwa dhana nzuri pindi tunaposalimiana nao. Tunapozingatia mafungamano ya Waislamu yamesambaratika kutokana na dhana mbaya. Unaposikia maongozi ya Waislamu tunasikia wakisema fulani amekusudia hivi, na fulani ametaka jamabo hili. Yote yanapelekea kupatikana kwa chuki na mwisho ni kuvunjika au kusambaratika kwa mafungamano. Dhana mbaya inapeleka kufuatilia aibu za watu na kuchunguzana kwa ajili hiyo utasikia kwa mwenye dhana mbaya akisema ‘Nitajaribu kuhakikisha’ basi atachunguza na kusengenya na kumtaja mwenzake kwa uovu. Kuenea kwa dhana mbaya kunakosekana uaminifu kati ya watu na kukatana jambo ambalo kwamba linapelekea kutofaulu katika mambo yetu.

Anasema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

 

وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ ۖ وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ}     الأنفال:46}

 

"Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri."      [Al-Anfaal:46]

Dhana mbaya haileti kheri na ni njia ya kuenea kwa uadui na kupatikana kwa madhambi hayo duniani ama kesho akhera ni majuto. Tazama watu waovu walivyo wakejeli Waislamu na kuwadhania maovu pindi Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Aliposema:

{وَقَالُوا مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ الْأَشْرَارِ  أَتَّخَذْنَاهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ الْأَبْصَارُ}        ص:62-63

"Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?  Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni ?"     [Sw'aad:62-63]

Anasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala

فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ  عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ  هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ}     المطففين:34-36

 

"Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?"     [Al-Mutaffifin:34-36]

Anasema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

 

    {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ}        { الحجرات:12}

"Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi."     [Al-Hujuraat:12]

Inajulisha Aya katika kuhifadhi heshima ya Muislamu kwa kutangulia na katazo la dhana. Ni uzuri ulioje kwa mujtama ulio salimika na dhana mbaya. Mtume  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam amesema

[Jiepusheni na dhana hakika ya dhana ni maongezi ya uongo wala msichunguzane wala msichukiane kuweni ndugu katika waja wa Mwenyezi Mungu].

Wamesema baadhi ya wanavyuoni dhana ambayo inafaa kuepukwa ni ile ambayo kwamba haijulikani njia yake kuwa ni ya sawa na sababu iliyokuwa ya wazi, mfano anayedhaniwa akiwa ni mtu mwema na akapewa amana kuwadhania kuwa amekhini ni haramu. Kinyume na ambae anajulikana anayefanya maovu wazi wazi kwa ajili hiyo wamesema wanavyuoni dhana mbaya kwa mtu mwema haifai na hapana tatizo kudhania uovu mtu muovu.

Imepokewa hadithi Said ibn Musaib akisema: “Amewaandikia baadhi ya maswahaba kutowacha kufanya wema kwa jambo la ndugu yake maadamu hujashindwa wala asidhani neno baya limetoka kwa ndugu yako ikiwa inawezekana kuchukulia kwa uzuri na huo ndio mfano wa watu wema pindi wanaposhindwa kuelewa baadhi ya maneno, kwa kuwahukumu makosa watu wengine bila ya kuzingatia nia na hali ya yule mtu”.

Na Ibn Qayyim amesema: “Neno moja husemwa na watu wawili mmoja wao anakusudia haki na mwingine wao anakusudia batili kwa ajili hiyo hahukumiwi mtu kuwa kafiri kwa aliyesema “ Ewe mola wangu wewe ni mja wangu na mimi ni mola wako” hakukusudia kujifanya Mwenyezi Mungu.

Na Amesema Sheikhul Islam Ibn Taymiyya "pindi anaponukuu maneno ya wenye kumkhalifu akisema “Maneno haya yana upana, na haki huchukuliwa kwa uzuri na batili huwa na mambo mengi”

Mwanadamu hana haki kwa ndugu yake isipokuwa kwa mambo yaliyo wazi. Amepokea Abdulrazaq kutoka kwa ‘Umar Ibn Khattab (R.A.)

akisema: “ Watu walikuwa wakipokea wahyi wakati wa Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) na wahyi ukakatika, lakini tunachukua sasa kwa yale yaliyodhihiri kutokana na vitendo vyenu kwa atakae dhihiri kheri tutamuamini na tutamkaribisha haitujalishi sisi usiri wake na Mwenyezi Mungu ndiye atakaye muhesabu kutokana na usiri wake na atakae dhihiri shari lake kwetu hatutomuamini wala hatutomsadiki hata akisema kuwa usiri wake ni mwema”. Kwa Muislamu ahesabu kuwa kila neno analozungumza au hukumu anayotamka na akumbuke Neno lake Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

         وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا}        الإسراء:36 

Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa." [ Al-Israai:36]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7668626
TodayToday291
Highest 04-18-2026 : 16767
US
Guests 621

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_69f18c157f9f34877219591777437717
title_69f18c157fa433777563801777437717
title_69f18c157fa904873107651777437717

NISHATI ZA OFISI

title_69f18c158006918302457131777437717
title_69f18c15800b712666251041777437717
title_69f18c158010311876447411777437717 Add content here

HUDUMA MPYA

: 2 + 1 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com