BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين 


عن جابرٍ رضي اللَّه عنه أَنْ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَمَر بِلَعْقِ الأَصابِعِ وَالصحْفةِ وقال: « إِنَّكُــم لا تَدْرُونَ في أَيِّهَا الْبَرَكَةَ »     رواه مسلم

وفي رواية لَهُ : « إِذَا وَقَعتْ لُقْمةُ أَحدِكُمْ  فَلْيَأْخُذْهَا فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أَذًى ، وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلا يَدَعْهَا لَلشَّيْطانِ ، وَلا يَمْسَحْ يَدَهُ بِالْمَندِيلِ حَتَّى يَلْعَقَ أَصَابِعهُ ، فَإِنَّهُ لا يدْرِي في أَيِّ طَعَامِهِ الْبَركَةَ
وفي رواية له : « إِنَّ الشَّيْطَانَ يَحْضُرُ أَحَدكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيءٍ مِنْ شَأْنِهِ حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ ، فَإِذَا سَقَطَتْ مِنْ أَحَدِكُمْ اللُّقْمَةُ فَلْيُمِطْ مَا كَان بِهَا منْ أَذًى، فَلْيأْكُلْها ، وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيْطَانِ


Kutoka kwa Jaabir Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume    ameamrisha kulamba vidole na sahani, akasema: [Ninyi hamjui ni wapi penye baraka. ]   [Imepokewana Muslim]

Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema:

[Linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aliokote na aondoe taka iliyoingia na alile, wala asimuachie shetani, wala asiupanguse mkono wake kwa kitambaa mpaka avilambe kidole vyake; kwani hajui ni katika chakula kipi kuna baraka.]

Na Riwaya nyingine tena ya Muslim imesema:

[Hakika shetani anahudhuria katika kila jambo la mmoja wenu hata anahudhuria kwenye chakula chake. Basi linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aondoe sehemu iliyoingia taka na alile,wala asimuachie shetani.] 


 
comments