BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين 


عنْ أَبِي عبدِ اللَّه النُّعْمَانِ بْنِ بَشيِرٍ رضي اللَّه عنهما، قال: سمِعْتُ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقولُ : « لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللَّه بَيْنَ وُجُوهِكمْ »   متفقٌ عليه

وفي روايةٍ لِمْسلمٍ : كان رسولُ اللُّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يُسَوِّي صُفُوفَنَآ حَتَّى كأَنَّمَا يُسَوي بِهَا الْقِداحَ حَتَّى إِذَا رأَى أَنَّا قَدْ عَقَلْنَا عَنْهُ ثُمَّ خَرَجَ يَوماً ، فقامَ حتَّى كَادَ أَنْ يكبِّرَ ، فَرأَى رجُلا بادِياً صدْرُهُ فقالَ : « عِبادَ اللَّه لَتُسوُّنَّ صُفوفَكُمْ أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللَّه بيْن وُجُوهِكُمْ »


Kutoka kwa Abuu ‘Abdillaah, An-Nu’maan bin Bashiyr  Radhi za Allah ziwe juu yake Nilimsikia Mtume akisema: [Wa-Allaahi mtazisawazisha safu zenu au Mwenyezi Mungu Atazibadilisha nyuso zenu]    [Imepokea na Bukhari na Muslim] 

Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema:

alikuwa Mtume ﷺ  akizisawazisha safu kana kwamba alikuwa anasawazisha kwazo mshale, mpaka alipo tuona tumelifahamu hilo. Kisha siku moja akatoka, akasimama hata alipokaribia kupiga Takbiri, akamuona mtu kifua chake kimetokeza, akasema: [Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, mtasawazisha safu zenu au Mwenyezi Mungu Atazibadilisha nyuso zenu]


 
comments