BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين 


عن أَبِي مسلمٍ ، وقيلَ : أَبِي إِيَاسٍ سلَمةَ بْنِ عَمْرو بن الأَكْوَعِ رضي اللَّه عنه ، أَنَّ رَجُلاً أَكَلَ عِنْدَ رسولِ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بِشِمَالِهِ فقالَ : « كُلْ بِيمِينكَ » قَالَ : لا أَسْتَطِيعُ . قالَ : « لا استطعَت » ما منعَهُ إِلاَّ الْكِبْرُ فَمَا رَفعَها إِلَى فِيهِ ،      رواه مسلم


Kutoka kwa Abuu Muslim, pia anaitwa Abuu Iyaas, Salamah bin ‘Amruw bin Al-Akwa’ Radhi za Allah ziwe juu yake amesimulia: Kwamba mtu mmoja alikula akiwa na Mtume ﷺ kwa mkono wake wa kushoto. Mtume  akamwambia: [Kula kwa mkono wako wa kulia.] Yule mtu akasema siwezi. Mtume ﷺ akamwambia: [Hutaweza!] Hakuna kilichomzuia isipokwa ni kibri. Basi hakuweza tena kuinua mkono wake hadi kinywani mwake.     [Imepokewa na Muslim]


 
comments