BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


{قال اللَّه تعالى : {وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

 {وقال تعالى : {وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ  إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ

{وقال تعالى : {قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ

{وقال تعالى : {فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

{وقال تعالى : {فإن تنازعتم في شيء فردوه إلى اللَّه والرسول إن كنتم تؤمنون بالله واليوم الآخر

{وقال تعالى : {مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّهَ

{وقال تعالى : {وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

{وقال تعالى : {فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

{وقال تعالى : {وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ وَالْحِكْمَةِ

والآيات في الباب كثيرة


Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho.]     [Suuratul Al H'ashri:7]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Wala hatamki kwa matamanio.Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;]     [Suurat Annajm:3-4]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu.]     [Suurat Al 'Imran:31]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.]     [Surat An-Nisaai:65]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.] Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu chungu.]    [Surat An-Nur:63]     [Surat An-Nisaai:59]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu]     [Surat An-Nisaai:80]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka]     [Suuratul Ash-shuura:52]

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima]    [Al-Ah'zab:34]

Na Aya katika Mlango huu ziko Nyingi.


شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



تتمة التعليق على آيات الباب



 
comments