BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


عَنْ أبي هُرَيْرَةَ رضي اللَّهُ عنه قال : قِيلَ : يا رسولَ اللَّهِ مَن أَكْرَمُ النَّاسِ ؟ قال : « أَتْقَاهُمْ » فقَالُوا : لَيْسَ عَنْ هَذا نَسْأَلُكَ ، قَالَ : « فيُوسُفُ نَبِيُّ اللَّهِ ابن نَبِيِّ اللَّهِ ابن نَبيِّ اللَّهِ ابنِ خَلِيلِ اللَّهِ » . قَالُوا : لَيْسَ عن هَذَا نَسْأَلُكَ ، قال :« فعَنْ مَعَادِنِ الْعَرَب تسْأَلُونِي ؟ خِيَارُهُمْ في الْجاهِليَّةِ خِيَارُهُمْ في الإِسلامِ إذَا فَقُهُوا »     متفقٌ عليه


Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:  aliulizwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ : Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani bora katika watu? Akajibu: [Ni yule aliyewazidi kwa kumcha Mungu.] Wakamwambia: Hatukuulizi kuhusu hili. Akawaambia: [Basi ni Yusuf Nabii wa Mumgu, Mtoto wa Nabi wa Mungu, Mtoto wa Nabii wa Mungu, Mtoto wa rafiki wa Mungu.] Wakasema: Hatukuulizi kuhusu hili. Akasema: [Mwaniuliza kuhusu koo za Waarabu? Wabora wao katika ujahiliyyah ndio wabora wao katika Uislamu iwapo watafahamu Dini.]    [Imepokelewa na Bukhari na Muslim]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



 
comments