الحديث السابع والعشرون
"البر حسن الخلق"
عن النّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ رضيَ اللهُ عَنْهُ عن النَّبي صلى الله عليه وسلم قَالَ: [ الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في نَفْسِكَ وَكَرِهْتَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِ النَّاسُ
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وعن وَابصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ رضي اللهُ عَنْهُ قالَ: قالَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم [جِئْتَ تَسأَلُ عَنِ الْبِرِّ؟] . قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: [اسْتَفْتِ قَلْبَكَ، الْبِرُّ مَا اطْمَأَنَّتْ إلَيْهِ النَّفْسُ وَاطْمَأَنَّ إلَيْهِ الْقَلْبُ، وَالإِثْمُ مَا حاكَ في النَّفْسِ وَتَردَّدَ في الصَّدْرِ وَإنْ أَفْتَاكَ النّاسُ وَأَفْتَوْكَ
حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَيْنَاهُ في مُسْنَدَي الْإِمَامَيْنِ أَحْمَدَ بْنِ حَنْبَلٍ وَالدَّارِمِيّ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى
HADITHI YA 27
WEMA NI TABIA NZURI
Kutoka kwa An-Nawwaas Ibn Sam'aan Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye alisema kuwa Mtume ﷺ kasema:
[Wema ni tabia nzuri na udhalimu ni kile kitu ambacho huyumbayumba (chenye mashaka) katika nafsi yako na hupendelei watu kukitambua.]
[Imepokelewa na Muslim]
Na kutoka kwa Waabisah Ibn Ma'abad Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye alisema:
Nilikuja kwa Mtume ﷺ naye akasema:
[Umekuja kuuliza juu wema ?] Nikasema: Ndio . Akasema: [Ushaurishe moyo wako. Wema ni kile ambacho nafsi yako inakihisi shwari na moyo wako pia unahisi shwari, na udhalimu ni kile kinachoyumbayumba katika nafsi na kwenda na kurudi kifuani ijapokuwa watu wamekupa shauri lao la kisheria (kukipendelea).]
[Ni Hadithi hasan imepokelewa katika Musnad mbili ya Imam Ahmad na Al-Ddaarimiy]
Today | 787 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.