KINGA YA MUISLAMU


 dua ya wasiwasi


 

 أعوذ بالله من الشيطان الرجيم واتفل على يسارك ]   ثلاثاً]

 مسلم 4/1729

[Najilinda na Mwenyezi Mungu   kutokana na shetani aliyelaaniwa]

Kisha utatema vijimate vichache upande wa kushoto mara tatu.

Imepokelewa kutoka kwa Uthman Ibn Al-Ass Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: [Nilimwambia Mtume  Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hakika shetani amenikalia kati yangu na kati ya swala yangu na kisomo changu, ananitatiza.  Akasema Mtume [Huyo ni shetani aitwae “Khanzab” ukimuhisi amekujia basi muombe hifadhi Mwenyezi Mungu nae, na tema vijimate vichache kushotoni kwako mara tatu]

……nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu  akaniondoshea.    [Imepokewa na Muslim.]


DUA YA ALIYEINGIWA NA WASIWASI 



comments