KINGA YA MUISLAMU
Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ } البقرة:152}
[Nitajeni nami nitawataja, na nishukuruni na wala msinikufuru] [Suratul Baqaraha: 152]
Na akasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً} الأحزاب:41}
[Enyi mlioamini mtajeni Mwenyezi Mungu sana] [Suratul Ahzaab: 41]
Akasema tena:
{ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيراً وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْراً عَظِيماً} الأحزاب:35}
[Nawasifu wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu sana na nawasifu wanawake wanaomtaja, Mwenyezi Mungu kawaandalia wote hao msamaha na malipo makubwa] [Suratul Ahzaab: 35 ]
Akasema tena :
وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعاً وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلاَ تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ} الأعراف:205}
[Mtaje Mola wako moyoni mwako kwa unyenyekevu na kwa uwoga, pasina kudhihirisha sauti, mtaje asubuhi na jioni, nawala usiwe nikatika wenye kughafilika] [Suratul A’raaf: 205]
Mtume ﷺ amesema :
[ وقال صلى الله عليه وسلم :[ مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت
[Mfano wa anaemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti.]
Na akasema Mtume ﷺ:
وقال صلى الله عليه وسلم :" ألا أنبئكم بخير أعمالكم , وأزكاها عند مليككم، وأرفعها في درجاتكم ، وخير لكم من إنفاق الذهب والورق ، وخير لكم من أن تلقوا عدوكم فتضربوا أعناقهم ويضربوا أعناقكم ؟ قالوا بلى .قال : ذكر الله تعالى
[Hivi niwaambieni khabari yamatendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno, mbele ya Mola wenu, na ambayo ni yajuu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko kukutana na adui zenu, mkawapiga shingo zao, nao wakakupigeni shingo zenu?] Wakasema masahaba; Ndio . Akasema Mtume ﷺ [Ni kumtaja Mwenyezi Mungu.]
وقال صلى الله عليه وسلم :" يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة
Amesema Mtume ﷺ Mwenyezi Mungu anasema
[Mimi niko mbele ya dhana ya mja wangu kwangu, akinitaja moyoni nami ninamtaja moyoni na akinitaja katika kundi, nami namtaja katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha kwangu paa moja, basi mimi najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha kwangu kiasi cha dhiraa, basi mimi nitajikurubisha kwake kiasi chakuyoosha mkono hadi kati ya kifuwa, na akinijia kwa mwendo mdogo basi nami nitamjia kwa mwendo wa kasi.]
وعن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال :" لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله
Imepokelewa kutoka kwa Abdalla Bin Busra radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alisema :Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu ambacho nitaweza kudumu nacho. Mtume ﷺ akamwambia : [Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba (yaani sio ukavu ) kwakumtaja Mwenyezi Mungu.]
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قرأ حرفاً من كتاب الله به حسنة ،والحسنة بعشر أمثالها ، لا أقول : {الم } حرف؛ ولكن : ألف حرف ،ولام حرف ،وميم حرف
Na amesema tena Mtume ﷺ [Atakaesoma harufu moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi anapata thawabu za jema moja na jema ni kwa mema kumi, sisemi kuwa ‘Alif Laam Miim’ ni harufu moja lakini ni kwamba ‘Alif’ peke yake ni harufu moja, na ‘Laam’ ni harufu , na ‘Miim’ ni harufu.]
وعن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال : خرج رسول الله صلى الله عليه وسلم ونحن في الصفة فقال :[ أيكم يحب أن يغدو كل يوم إلى بطحان أو إلى العقيق فيأتي منه بناقتين كوماوين في غير إثم ولا قطيعة رحم ؟] فقلنا : يا رسول الله نحب ذلك . قال : [ أفلا يغدو أحدكم إلى المسجد فيعلم ، أو يقرأ آيتين من كتاب الله عز وجل خير له من ناقتين ، وثلاث خير لهُ من ثلاث ٍ، وأربع خير لهُ من أربع ، ومن أعدادهن من الإبل
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir radhi za Allah ziwe juu yake, amesema : Ametoka Mtume wa Mwenyezi Mungu na sisi tuko sehemu iitwayo Assufah, akasema [Nani kati yenu anapenda aende kila siku sehemu iitwayo But-haan au Aqiq aje na ngamia wawili walio nenepa pasi na dhambi wala kukata udugu?] Wakasema maswahaba “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tunapenda hivyo’ akasema Mtume ﷺ [Hivi haendi (asubuhi ) mmoja wenu msikitini akajuwa au akasoma Aya mbili, za kitabu cha Mwenyezi Mungu? Hizo aya mbili ni bora kwake kuliko kupata ngamia wawili, na endapo atasoma aya tatu zitakuwa ni bora kwake kuliko ngamia watatu, na aya nne ni bora kwake kuliko ngamia wanne, na vilevile zaidi ya hapo. Aya zozote atakazo zisoma basi ni bora kwake kuliko hisabu yake kwa ngamia]
وقال صلى الله عليه وسلم:" من قعد مقعداً لك يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة ومن اضطجع مضجعاً لم يذكر الله فيه كانت عليه من الله ترة
Na Anasema Mtume ﷺ [Anaekaa kikao chochote kile asimtaje Mwenyezi Mungu katika kikao hicho basi ana dhambi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na anaelala sehemu yeyote ile kisha asimtaje Mwenyezi Mungu wakati wakuinuka sehemu hiyo basi ana dhambi kwa Mwenyezi Mungu.]
وقال صلى الله عليه وسلم : " ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله فيه ، ولم يصلوا على نبيهم إلا كان عليهم ترة ، فإن شاء عذبهم وإن شاء غفر لهم
Amesema Mtume ﷺ [Hapana watu wowote wale, wanaokaa kikao kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu humo, wala wasimswalie Mtume wao ila watakuwa wana dhambi. Akipenda Atawaadhibu na Akipenda Atawaghufuria.]
وقال صلى الله عليه وسلم :" ما من قوم يقومون من مجلس لا يذكرون الله فيه إلا قاموا عن مثل جيفة حمار وكان لهم حسرة
Amesema Mtume ﷺ [Hapana watu wowote wale wanaosimama katika kikao walichokaa, kisha wasimtaje Mwenyezi Mungu ila watakuwa wanasimama kama mzoga wa punda, na watakuja juta kwa kutomtaja Mwenyezi Mungu.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.