Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitabu tawhid


باب ما جاء من التغليظ فيمن عبد الله عند قبر رجل صالح فكيف إذا عبده

في الصحيح عن عائشة رضي الله عنها أن أم سلمة ذكرت لرسول الله ﷺ كنيسة رأتها في أرض الحبشة وما فيها

من الصور. فقال: [ أولئك إذا مات فيهم الرجل الصالح أو العبد الصالح بنوا على قبره مسجدا، وصوروا فيه تلك الصور

أولئك شرار الخلق عند الله]، فهؤلاء جمعوا بين الفتنتين، فتنة القبور، وفتنة التماثيل. ولهما عنها قالت: لما نُزل برسول الله

ﷺ طفق يطرح خميصة له على وجهه، فإذا اغتم بها كشفها، فقال وهو كذلك : [ لعنة الله على اليهود

والنصارى، اتخذوا قبور أنبيائهم مساجد ] يحذر ما صنعوا، ولولا ذلك أبرز قبره، غير أنه خشي أن يتخذ مسجدا. أخرجاه.

ولمسلم عن جندب بن عبد الله قال: سمعت النبي ﷺ قبل أن يموت بخمس وهو يقول: [ إني أبرأ إلى الله أن

يكون لي منكم خليل، فإن الله قد اتخذني خليلا، كما اتخذ إبراهيم خليلا، ولو كنت متخذا من أمتي خليلا، لاتخذت أبا بكر خليلا، ألا وإن

[من كان قبلكم كانوا يتخذون قبور أنبيائهم مساجد، ألا فلا تتخذوا القبور مساجد، فإني أنهاكم عن ذلك

فقد نهى عنه في آخر حياته، ثم إنه لعن - وهو في السياق - من فعله، والصلاة عندها من ذلك، وإن لم يُبْنَ مسجد، وهو معنى

قولها: خشي أن يتخذ مسجدا، فإن الصحابة لم يكونوا ليبنوا حول قبره مسجدا، وكل موضع قصدت الصلاة فيه فقد اتخذ مسجدا، بل

كل موضع يصلى فيه يسمى مسجدا، كما قال ﷺ: [ جعلت لي الأرض مسجدا وطهورا ]. ولأحمد بسند جيد

[عن ابن مسعود رضي الله عنه مرفوعا: [ إن من شرار الناس من تدركهم الساعة وهم أحياء والذين يتخذون القبور مساجد

رواه أبو حاتم في صحيحه

فيه مسائل

الأولى: ما ذكر الرسول ﷺ فيمن بنى مسجدا يعبد الله فيه عند قبر رجل صالح، ولو صحت نية الفاعل

الثانية: النهي عن التماثيل، وغلظ الأمر في ذلك

الثالثة: العبرة في مبالغته ﷺ في ذلك. كيف بيّن لهم هذا أولا، ثم قبل موته بخمس قال ما قال، ثم لما كان في

السياق لم يكتف بما تقدم. الرابعة: نهيه عن فعله عند قبره قبل أن يوجد القبر

الخامسة: أنه من سنن اليهود والنصارى في قبور أنبيائهم

السادسة: لعنه إياهم على ذلك

السابعة: أن مراده ﷺ تحذيره إيانا عن قبره

الثامنة: العلة في عدم إبراز قبره

التاسعة: في معنى اتخاذها مسجدا

العاشرة: أنه قرن بين من اتخذها مسجدا وبين من تقوم عليهم الساعة، فذكر الذريعة إلى الشرك قبل وقوعه مع خاتمته

الحادية عشرة: ذكره في خطبته قبل موته بخمس: الرد على الطائفتين اللتين هما شر أهل البدع، بل أخرجهم بعض السلف من

الثنتين والسبعين فرقة، وهم الرافضة والجهمية. وبسبب الرافضة حدث الشرك وعبادة القبور، وهم أول من بنى عليها المساجد

الثانية عشرة: ما بلي به ﷺ من شدة النزع

الثالثة عشرة: ما أكرم به من الخلّة

الرابعة عشرة: التصريح بأنها أعلى من المحبة

الخامسة عشرة: التصريح بأن الصديق أفضل الصحابة

السادسة عشرة: الإشارة إلى خلافته


MLANGO WA 19 KUTILIWA MKAZO HARAMISHO LA KUMUABUDU MWENYEZI MUNGU KWENYE KABURI LA MTUM MWEMA BASI AKIMUABUDU ALIE KABURINI?


Katika Sahih (Bukhari), Imepokelewa kutoka kwa ‘Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Ummu Salamah alimtajia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ kwamba aliona kanisa zuri Abyssinia lilojaa picha na Masanamu. Akasema: [Hao, anapokufa mtu mwema miongoni mwao, au mja mwema, hujenga Msikiti juu ya kaburi lake. Kisha wakazichora ndani yake picha hizo. Hao ni viumbe waovu mbele ya Allaah. Basi hao wamejumuisha baina ya fitnah mbili; fitnah ya makaburi na fitnah ya masanamu]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na kutoka kwao (Bukhari na Muslim) Vile vile, Amesema ‘Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake): Mauti yalipomkaribia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alianza kuchomoa kipande cha kitambaa [cha shuka ya kitanda] akijiwekea usoni mwake Akasema alipokuwa katika hali hiyo: [Mwenyezi Mungu Awalaani Mayahudi na Manaswara kwa kufanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa ‘ibaada]. Akawatahadharisha watu kuhusu vitendo vyao. Ingelikuwa si kuchelea hivyo [khofu ya kufanya kaburi la Nabiy kuwa mahali pa ‘ibaadah], basi kaburi lake lingeliwekwa wazi [kama yalivyowekwa wazi makaburi ya Maswahaba wake]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na Muslim kasimulia kutoka kwa Jundub bin ‘Abdullah (Radhi za Allah ziwe juu yake) Amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema siku tano kabla ya kufariki kwake: [Mimi sina hatia kwa Allaah kumfanya mmoja wenu kuwa khalili. Hakika Mwenyezi Mungu Amenifanya mimi kuwa ni khalili Wake kama alivyomfanya Ibrahim kuwa khalili. Ningekuwa wa kufanya khalili katika Umma wangu, basi ningemfanya Abuu Bakr kuwa khalili wangu Tahadharini! Waliotangulia kabla yenu walikuwa wakifanya makaburi ya Manabii wao mahali pa ‘ibaadah. Tahadharini! Msifanye makaburi [yoyote] kuwa ni mahali pa ‘ibaadah nakukatazeni kufanya hivyo] [Imepokewa Muslim]

Amekataza hilo katika mwisho wa umri wake. Kisha akalaani yeyote atakayefanya kitendo hicho. Na kuswali makaburini ni sawa na kulifanya kaburi kuwa ni Msikiti hata kama hamna Msikiti uliojengwa hapo kaburini. Hii ndio maana ya kauli yake Mtume ﷺ: [Khofu ya kufanya (kaburi lake) kuwa ni Msikiti’. Maswahaba hawajapato kujenga Msikiti kaburini mwake. Na kila mahali panaposwaliwa panaitwa Msikiti kama alivyosema Mtume ﷺ: [ Imefanywa Ardhi kwangu kuwa ni Miskiti na mahali Twahara]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Amepokea Ahmad kwa isnaad nzuri kutoka kwa Ibn Mas’ud (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesimulia Hadith Marfuw’ (kutoka kwa Mtume ﷺ) : [Hakika watu waovu kabisa kitakaowadiriki Qiyama nao ni hai, na wale wanaofanya makaburi kuwa ni Misikiti [mahali pa ‘ibaadah]] [Ahmad na amesimulia Abuu Haatim katika Swahiyh yake]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Onyo la Mtume ﷺ kuhusu ujenzi wa Misikiti ya kumwabudu Mwenyezi Mungu katika makaburi ya watu wema, hata kama anayefanya hivyo ana niah njema.

2. Haramisho la masanamu na vitu kama hivyo (mapicha) na uzito wa jambo hilo.

3. Funzo katika msisitizo wa Mtume ﷺ wakati wa kufikisha hili, ambapo kwanza aliwaeleza (kwa upole), kisha siku tano kabla hajafariki alisema kama hapo awali. Halafu baadaye wakati wa Sakaraatul-Mawti akarudia hilo hilo.

4. Aliharamisha kwa kusisitiza kuwa hili lisifanywe kaburini kwake, kabla ya kuweko kaburi lenyewe.

5. Hiyo ni miongoni mwa matendo ya Wayahudi na Wakristo kuhusu makaburi ya Manabii wao.

6. Aliwalaani Mayahudi na Wakristo kwa sababu hiyo.

7. Kusudio la kufanya hivyo ni kutuonya sisi kuhusu kaburi lake tusilifanyie ‘ibaada.

8. Sababu ya kutokujengewa kaburi lake.

9. Maana halisi ya: (makaburi) “kuyafanya Misikiti.”

10. Mtume ﷺ amefananisha wanaofanya makaburi kuwa Misikiti na watakaodiriki Qiyama wakiwa hai. Akataja njia zinazopeleka katika shirki kabla hazijatokea, pamoja na natija zake.

11. Alilitaja hili siku tano kabla hajafariki. Hapa kuna kukanusha makundi mawili ambao ni miongoni mwa waovu zaidi katika watu wa bid’ah (uzushi). Bali baadhi ya Wanachuoni wameyatenga kabisa makundi hayo mawil kutoka ule mjumuiko wa makundi 72 ya Waislamu. Mawili hayo ni Ar-Raafhidhwah (Shia) na Aj-Jahmiyyah. Na ni kwa sababu ya Raafidhwah (Mashia) ndio ikaanza shirki ya kuabudu makaburi nao ndio wa kwanza kuyajengea Misikiti.

12. Shida aliyoipa Mtume ﷺ katika Sakaartul-Mawt.

13. Mwenyezi Mungu Amemkirimu (Mtume ﷺ) kumfanya kuwa ni khalili. (kipendi chake)

14. Ubainisho kuwa ukhalili huo ulikuwa zaidi ya upendo mwingine.

15. Ubainisho kuwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhi za Allah ziwe juu yake) ni Swahaba alikuwa ni mbora wa Maswahaba.

16. Ishara ya ukhalifa wa (Abuu Bakr).


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6487331
TodayToday437
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 36

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5e7dd23cc11102007151735286397
title_676e5e7dd24af14330305181735286397
title_676e5e7dd25857164319481735286397

NISHATI ZA OFISI

title_676e5e7dd3aaa7233855621735286397
title_676e5e7dd3b817206691171735286397
title_676e5e7dd3c5a10944032841735286397 Add content here

HUDUMA MPYA

: 11 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com