KITAAB AT-TAWHIID


kitab altawheed


باب (11) من الشرك: النذر لغير الله
وقول الله تعالى: {يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْماً كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيراً}   الإنسان:7

وقوله: {وَمَا أَنْفَقْتُمْ مِنْ نَفَقَةٍ أَوْ نَذَرْتُمْ مِنْ نَذْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ يَعْلَمُهُ}    البقرة:270
وفي الصحيح عن عائشة رضي الله عنها: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [من نذر أن يطيع الله فليطعه ; ومن نذر أن يعصي الله فلا يعصه]      رواه البخاري
:فيه مسائل
الأولي: وجوب الوفاء بالنذر
الثانية: إذا ثبت كونه عبادة الله، فصرفه إلى غيره شرك
الثالثة: أن نذر المعصية لا يجوز الوفاء به


MLANGO WA 11 KUWEKA NADHIRI KWA ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU NI SHIRKI


Na kauli ya Mwenyezi Mungu:

[Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,]  [Al-Insaan: 7]

Na kauli Yake  :

[Na chochote mnacho toa au nadhiri mnazo weka basi hakika Mwenyezi Mungu anajua.]    [Al-Baqarah: 270]

Na katika Asw-Swahihi: Imepokelewa kutoka kwaAisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume amesema: [Atakayeweka nadhiri kumtii Mwenyezi Mungu na amtii. Na atakayeweka nadhiri kumuasi Mwenyezi Mungu basi asimuasi]    [Imepokewa na Bukhari]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1. Uwajibu wa kutekeleza nadhiri.

2. Ikiwa imethibitika kuwa nadhiri Ibada ya Mwenyezi Mungu , basi kumfanyia mwengine ni shirki.

3. Kwamba nadhiri ya masia haifai kutekeleza.


comments