KITAAB AT-TAWHIID
باب الخوف من الشرك
{وقول الله : {إِنَّ اللَّهَ لا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ
{وقال الخليل عليه السلام: {وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَنْ نَعْبُدَ الْأَصْنَامَ
وفي الحديث: [أخوف ما أخاف عليكم: الشرك الأصغر، فسئل عنه، فقال: الرياء] رواه أحمد والطبراني والبيهقي
وعن ابن مسعود رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [من مات وهو يدعو من دون الله ندا دخل النار] رواه البخاري. ولمسلم عن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: [من لقي الله لا يشرك به شيئا دخل الجنة، ومن لقيه يشرك به شيئا
دخل النار] رواه مسلم
:فيه مسائل
.الأولى: الخوف من الشرك
.الثانية: الرياء من الشرك
.الثالثة: أنه من الشرك الأصغر
.الرابعة: أنه أخوف ما يخاف منه على الصالحين
.الخامسة: قرب الجنة والنار
.السادسة: الجمع بين قربهما في حديث واحد
السابعة: أنه من لقيه لا يشرك به شيئا دخل الجنة، ومن لقيه يشرك به شيئا دخل النار، ولو كان من أعبد الناس
.الثامنة: المسألة العظيمة: سؤال الخليل له ولبنيه وقاية عبادة الأصنام
{التاسعة: اعتباره بحال الأكثر لقوله: {رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيراً مِنَ النَّاسِ
العاشرة: فيه تفسير " لا إله إلا الله "، كما ذكره البخاري
.الحادية عشرة: فضيلة من سلم من الشرك
MLANGO WA KUOGOPA SHIRK (KUMSHIRIKISHA MWENYEZI MUNGU)
Na kauli Yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye] [An-Nisaa: 48]
Na amesema Khalil (Ibraahim Alayhi salaam):
[Na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu.] [Ibrahim: 35]
Na katika Hadithi: [Nnachokukhofieni zaidi juu yenu ni shirki ndogo] Akaulizwa kuhusu hiyo shirki akasema: [Riyaa (Kujionyesha)] [Imepokewa na Ahmad katika Musnad yake]
Na Kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Yeyote atakayekufa hali anamshirikisha Mwenyezi Mungu ataingia Motoni] [Imepokewa na Bukhari]
Na Imeokolewa na Muslim kutoka kwa Jaabir (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Atakayekutana na Mwenyezi Mungu hali hamshirikishi na chochote ataingia Peponi. Na atakayekutana Naye hali anamshirikisha na chochote ataingia motoni] [Imepokewa na Muslim]
Masuala Muhimu Yaliyomo:
1- Kuogopa Shirk (Kumshirikisha Mwenyezi Mungu)
2- Riyaa (kujionyesha) ni aina ya shirki.
3- Riyaa ni shirki ndogo.
4- Riyaa inakhofiwa sana na waja wema (kwani rahisi mno mtu kutumbukia ndani yake)
5- Ukaribu wa Pepo na Moto.
6- Ukaribu huo wa Pepo na Moto umetajwa katika Hadithi moja.
7- Mwenye kukutana na Mwenyezi Mungu (Siku ya Qiyama) akiwa hakumshirikisha na chochote ataingia Peponi; na mwenye kukutana Naye, huku amemshirikisha na kitu, ataingia Motoni, hata kama alikuwa ni mwenye kumuabudu Mungu sana.
8- Umuhimu mkubwa mno wa suala hili, kiasi kwamba Al-Khalil (Ibrahim) aliomba yeye na wanawe waepushwe na kuabudu masanamu.
9- Kuzingatia kwake (Ibrahim) jinsi watu wengi (walivyoingia katika ibada ya masanamu ) aliposema:
[Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hayo yamewapoteza watu wengi] [Ibrahim:36]
10- Tafsiri ya maana ya (kauli ya) “Laa ilaaha illaa Allaah” kama alivyoitaja Al-Bukhari.
11- Fadhila za aliyesalimika na shirki.
Today | 357 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.