KITAAB AT-TAWHIID
كتاب التوحيد
{وقول الله تعالى: {وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
وقوله: {وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولاً أَنِ اعْبُدُواْ اللّهَ وَاجْتَنِبُواْ الطَّاغُوتَ النحل:36
وقوله: {وَقَضَى رَبُّكَ أَلاَّ تَعْبُدُواْ إِلاَّ إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا} الإسراء:23
وقوله: {وَاعْبُدُواْ اللّهَ وَلاَ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئًا} النساء:36
وقوله: {قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ أَلاَّ تُشْرِكُواْ بِهِ شَيْئًا} الآيات الأنعام:151
قال ابن مسعود رضي الله عنه: من أراد أن ينظر إلى وصية محمد صلى الله عليه وسلم التي عليها خاتمة فليقرأ قوله تعالى: {قُلْ تَعَالَوْاْ أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ} – إلى قوله – {وَأَنَّ هَـذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا..} الآية
وعن معاذ بن جبل رضي الله عنه قال: كنت رديف النبي صلى الله عليه وسلم على حمار فقال لي: [يا معاذ أتدري ما حق الله على العباد، وما حق العباد على الله؟] فقلت: الله ورسوله أعلم. قال: "حق الله على العباد أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئاً، وحق العباد على الله أن لا يعذب من لا يشرك به شيئاً" فقلت: يا رسول الله أفلا أبشر الناس؟ قال: [لا تبشرهم فيتكلوا] أخرجاه في الصحيحين
فيه مسائل: الأولى: الحكمة في خلق الجن والإنس
الثانية: أن العبادة هي التوحيد؛ لأن الخصومة فيه
{الثالثة: أن من لم يأت به لم يعبد الله، ففيه معنى قوله تعالى : { ولا أنتم عابدون ما أعبد
الرابعة: الحكمة في إرسال الرسل
الخامسة: أن الرسالة عمَّت كل أمة
السادسة: أن دين الأنبياء واحد
{السابعة: المسألة الكبيرة أن عبادة الله لا تحصل إلا بالكفر بالطاغوت؛ ففيه معنى قوله: {فمن يكفر بالطاغوت ويؤمن بالله
الثامنة: أن الطاغوت عام في كل ما عُبِد من دون الله
التاسعة: عظم شأن ثلاث الآيات المحكمات في سورة الأنعام عند السلف. وفيها عشر مسائل، أولها النهي عن الشرك
العاشرة: الآيات المحكمات في سورة الإسراء، وفيها ثماني عشرة مسألة، بدأها الله بقوله: {لا تجعل مع الله إلها آخرفتقعد مذموماً مخذولاً} وختمها بقولـه: {ولا تجعل مع الله إلهاً آخر فتلقى في جهنم ملوماً مدحوراً}، ونبهنا الله سبحانه على عظم شأن هذه المسائل بقوله: {ذلك مما أوحى إليك ربك من الحكمة
الحادية عشرة: آية سورة النساء التي تسمى آية الحقوق العشرة، بدأها الله تعالى بقوله: (واعبدوا الله ولا تشركوا به شيئاً
الثانية عشرة: التنبيه على وصية رسول الله صلى الله عليه وسلم عند موته
الثالثة عشرة: معرفة حق الله تعالى علينا
الرابعة عشرة: معرفة حق العباد عليه إذا أدوا حقه
الخامسة عشرة: أن هذه المسألة لا يعرفها أكثر الصحابة
السادسة عشرة: جواز كتمان العلم للمصلحة
السابعة عشرة: استحباب بشارة المسلم بما يسره
الثامنة عشرة: الخوف من الاتكال على سعة رحمة الله
التاسعة عشرة: قول المسؤول عما لا يعلم: الله ورسوله أعلم
العشرون: جواز تخصيص بعض الناس بالعلم دون بعض
الحادية والعشرون: تواضعه صلى الله عليه وسلم لركوب الحمار مع الإرداف عليه
الثانية والعشرون: جواز الإرداف على الدابة
الثالثة والعشرون: فضيلة معاذ بن جبل
الرابعة والعشرون: عظم شأن هذه المسألة
KITAAB AT-TAWHIID
Na kauli ya Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.] [Adh-dhaariyaat:56]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.] [An Nahl:36]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema] [Al Israai:23]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili] [An-Nisaa: 36]
Na kauli yake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote] [An'aam:151]
Amesema Ibn Mas’uwd (Radhi za Allah ziwe juu yake): [Anayetaka kuangalia wasiya wa Muhammad ﷺ ambao ulikuwa na muhuri wake, basi asome neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ: [Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote] hadi kauli yake: [Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine.]
Na Imepokelewa kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: Nilikuwa nyuma ya Mtume ﷺ juu ya punda akasema: [Ewe Mu’aadh! Unajua nini haki ya Mwenyezi Mungu juu ya waja Wake, na nini haki ya waja juu ya Mwenyezi Mungu?] Nikajibu: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi: Akasema Mtume ﷺ: [Haki ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote. Na haki ya waja kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba Hatomwadhibu yeyote ambaye hamshirikishi na chochote]. Nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Niwabashirie watu? Akasema: [Usiwabashirie wasije kuitegemea] [wakaacha kufanya juhudi katika Iba]ada] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Masuala Muhimu Yaliyomo (katika Mlango huu):
1- Hekima ya kuumbwa Majini na Binadaamu.
2- Kwamba Ibada ndio Tawhiyd kwa sababu uhasama unapatikana kwenye Tawhiid (Kumpwekesha Mungu).
3- Asiyeteye kuwa na Tawhiyd, (Kumpwekesha Mungu) atakuwa hajamwabudu Mwenyezi Mungu. ndio Maana ya neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.] [Al-Kafirun: 3)]
4- Hekima ya kutumwa Mitume.
5- Kwamba Ujumbe umefikishwa kwa kila umma.
6- Kwamba Dini ya Mitume wote ni moja.
7- Suala lenye umuhimu mkubwa hapa ni kwamba, kumwabudu Mwenyezi Mungu hakutambuliki pasina kukanusha Twaghuti. Na hiyo ndio maana ya neno lake Mwenyezi Mungu ﷻ:
[Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika.] [Al-Baqarah:256]
8- Neno ‘Twaghuti’ humaanisha kwa ujumla kila kitu kinachoabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
9- Umuhimu mkubwa wa Aya tatu Muhkamat (zenye maana wazi) katika Surat Al-An’aam kwa wema walio tutangulia (Salaf). Na katika Aya hizi kuna Mas'ala kumi na la awali ni kukatazwa shirki.
10- Aya za Muhkamaat (zenye maana wazi) katika Surat Al-Israa zina Mas'ala kumi na nane, na Mwenyezi Mungu Anaanza kwa neno lake:
[Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, usije ukawa wa kulaumiwa uliye tupika.] [Al-Israa: 22]
Na Akakhatimisha kwa neno lake ﷻ:
[Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi] [Al-Israa: 39]
Na Mwenyezi Mungu akatutanabahisha juu ya umuhimu wa Mas'ala haya kwa kusema:
[Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi.] [Al-Israa: 39]
11- Aya ya Suratu An-Nisaa ambayo imeitwa Aya za haki kumi. Mwenyezi Mungu ﷻ Amezianza kwa kusema:
[Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili] [An-Nisaa: 36]
12- Tanbihi ya wasiya wa Mtume wa Mwenyezi Mungu wakati wa kufariki kwake.
13- Kuzijua haki za Mwenyezi Mungu juu yetu.
14- Kuzijua haki za waja juu yake pindi wakitekeleza haki Zake.
15- Maswahaba wengi hawakuwa wakijua jambo hili.
16- Ruhusa ya kuficha Elimu inapokuwa na manufaa. Kama hapo ilikuwa ni kwa ajili wajitahidi zaidi kumwabudu Mwenyezi Mungu.
17- Inapendekezeka kumbashiria Muislamu khabari njema ya kumfurahisha.
18- Khofu (ya watu) kutegemea wingi wa rahma za Mwenyezi Mungu.
19- Kauli ya mtu anayeulizwa pindi asipojua jibu, “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Wanajua zaidi.”
20- Ruhusa ya kutoa baadhi ya Elimu kwa baadhi ya watu bila wengine.
21- Unyenyekevu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ kupanda mnyuma pamoja na Swahaba.
22- Kufaa watu wawili kupanda mnyama mmoja.
23- Fadhila za Mu’aadh bin Jabal (Radhi za Allah ziwe juu yake).
24- Umuhimu mkubwa wa jambo hili (la Tawhid).
Today | 316 |
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.