SHIRKI
MAANA YA SHIRKI
Nayo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta´ala) pamoja na kiumbe mwengine au kitu chochote kile kingine katika haki za Mwenyezi Mungu. Au sema ni kumsawazisha asiyekuwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu katika yale mambo ambayo ni haki zake Mwenyezi Mungu.
Basi atakaeomba asiye Mwenyezi Mungu, au kuwapa majina ya Mwenyezi Mungu, au kuamini kwamba kuna Mola mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu, atakuwa amefanya shirki.
Na Shirki ni katika dhambi kubwa zaidi kuliko dhambi nyingine yoyote ile.
Mwenyezi Mungu mtukufu amesema:
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ} لقمان:13}
[Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa] [Luqmaan:13].
Kwa nini Shirki ni dhulama kubwa, kwa sababu yeye Mwenyezi Mungu ndie anae umba na kuruzuku waja wake,na yeye ndie anaehuisha na ndie anafisha,na hakuna lolote linalokuwa katika ulimwengu huu ila ni kwa uwezo wake na matakwa yake Mwenyezi Mungu aliye tukuka,kasha mwanadamu akamwacha Mwenyezi Mungu aliye mneemesha neema zote hizi na akaenda kuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu basi mja huu huwa amefanya dhulma ya hali juu.
Na kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu amemuharamishia kuingia peponi kwa yoyote yule atakae kufa hali ya kuwa ni Mushik,Mwenyezi Mungu anasema:
إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ} المائد:72}
[Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.] [Al Maaida:72]
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu hamsamehe mja atake kufa hali ya kuwa ni mushrik,lakini allah huenda akamsamehe anaye mtaka ambae amekufa na madhambi mengine lakini hakuwa amemshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu,Mwenyezi Mungu anasema:
إِنَّ اللَّهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا} النساء:48}
[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa] [Al Nisaai:48]
SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.