AL-USWUL ATH-THALATHA (Misingi Mitatu)


misingi


الْمَرْتَبَةُ الثَّانِيَةُ: الإِيمَانُ

وَهُوَ:

[بِضْعٌ وَسَبْعُونَ شُعْبَةً، فَأَعْلاهَا قَوْلُ لا إلٰه إِلا اللهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ]

وَأَرْكَانُهُ سِتَّةٌ كما فى الحديث:

أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ]    رواه مسلم]

:وَالدَّلِيلُ عَلَى هَذِهِ الأَرْكَانِ السِّتَةِ قَوْلُهُ تَعَالَى

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ}    البقرة:177}

:ودليل القدر قَوْلُهُ تَعَالَى

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ}   القمر:49}


Daraja Ya Pili: Imani

Nayo ni:

[Ina tanzu (matawi) Sabiini na kitu. Ya juu yake ni kauli ya "Laa ilaaha illa-Allaah” [hapana Muabudiwa wa haki ila Mwenyzi Mungu], na ya chini yake kabisa ni kuondosha uchafu njiani.Na kuona hayaa ni utanzu [tawi] katika tanzu za Imani]   (1)

Na nguzo zake ni sita kama ilivyo kuja katika Hadithi:

[Ni kumwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mitume Wake na Siku ya Mwisho, na kuamini Qadari kheri yake na shari zake][Imepokewa na Muslim]

Na dalili ya hizi nguzo sita ni kauli yake Mwenyezi Mungu :

[Sio wema kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Bali wema ni wa anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii,]   [Al-Baqara:177]

Na dalili ya Al-Qadr (majaaliwa) ni kauli ya Mwenyezi Mungu :

[Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.]     [Al-Qamar:49]

 


SHEREHE YA KITABU USUULU THALATHA NA SHEIKH SHADDAD  ALI 



1) Hii ni Hadithi iliopokewa na Muslim kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Alke.

 

comments