Menu

Vituko na Majabu


MASHIA NA ASHURA'A


 filemanager


Siku ya ashuraa ni siku tukufu,kwani ndio siku ambao Mwenyezi Mungu alimwngamiza Fir'aun na kumuokowa nabii Munsa Alayhi salam,siku hii nabii Musa alifunga kumshukru Mwenyzi Mungu aliyetukuka,na Mtume akatuhimiza kufunga siku hii ya Ashuraa kama ilivyo kuja kwenye Hadithi:

 

      عن أبي قتادة رضي اللَّه عنه ، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: " صيام يوم عاشوراء، أحتسب على اللَّه أن يكفر السنة التي قبله       أخرجه مسلم وأبوداود

Kutoka kwa Abii Qatada radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume amesema:[kufunga siku ya ashura'a natarji kwa ALLAH kwamba inafuta madhambi ya mwaka uliyopita]       [Imepokewa na Muslim na Abuu Daud.

Lakini siku hii kwa Mashia wameibadilisha na kuifanya ni siku ya huzuni na kuomboleza,na isitoshe kufanya mambo ambao dini imekataza, kama kujipiga kwa visu na kujikata kwa mapanga,mpaka kupelekea baadhi yao kufariki, kutokamana na majereha,eti wakidai kufanya hivyo ni katika dini.

Menyezi Mungu anasema katika Qur'ani tukufu:

 

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا}   النساء:29}

 

[Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.]       [Al-Nnisaa:29]


Na Uislamu umekataza watu kuomboleza katika kulia na Mtume asema:

 

أنا بريء من الصالقة والحالقة والشاقة]  رواه البخاري]

 

[Mimi niko mbali na anaeomboleza,na Kunyoa nywele,na mwenye kupasuo nguo (wakati wa msiba)]        [Imepokelewa na Bukhari]

Ikiwa kuomboleza kwa maneno ni haramu je mtu kujipigia na kujiumiza?
Na imekuja hadhiti nyingine:

 

 ليس منا من ضرب الخدود ، وشق الجيوب ، ودعا بدعوى الجاهلية ]   رواه البخاري  ومسلم ]

 

[Si katika sisi atakae jipiga Matavu (wakati anapo patikana na Msiba) na kupasua Mivuko (nguo) na kuita miito ya kijahiliya]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Tunaomba wale ndugu zetu walidanganywa au kutoufahamahu ushia watumia akilizi zao na wajiulize, kweli hayo wanayo yafanya ni dini?
Mbona siku hii imekuwa ni siku ya vichekesho na kuwa pingamizi dhini ya uislamu kwa wale wasio tafautisha Uislamu na ushia, na kuona kuwa haya wanayo fanywa na Mashia ni mafundisho ya Waislamu.
Ilhali Dini ya Uislamu uko mbali na haya, na imekuja kukataza kufanya mambo kama haya.
Na Uislamu umekuja kufundisha huruma mpaka kwa wanyama ,Leo utona mtu amkata mototo wake na kumwaga damu yake bila huruma kitendo ambacho hata wanyama hawafanyi hivyo,na lakusikitisha ni kutai kitendo hicho ni katika dini ,ilhali dini ya uislamu iko mbali na kitendo hicho.

Na kudai kufanya hivyo ni kuhuzunika kwa kifo cha Husein radhi za Allah ziwe juu yake.
Kisha twauliza hawa Mashia kwanini mwaomboleza kifo cha Husein peke yake? Kwani ni yeye pekeyake alieuliwa kidhulma? Sibaba yake husein Sayyidna ali bin Abiitwalib radhi za Allah ziwe juu yake,pia na yeye si aliuwa kidhulma?
Mbona hamuombolezi siku aliyouliwa??

Bila shaka wanayo yafanya Mashia siku hii ya ashuraa iko mbali na mafunzo ya Uislamu,na yote haya wanayoyafanya si katika Uislamu bali ni dini yao Mashia waliyo ibuni.

Twamuomba Mwenyzi Mungu atuthibitishe kwenye haki,na awaongoze wale waliopotea katika njia ya haki.

Ndugu tazama wanao yafanya Mashia siku hii ya Ashuraa kisha ujuilize kweli huu ndio Uislamu?


 

 

CHOZI LITAKUINGIZA PEPONI MIAKA !! 

 

Kulia anapopatikana na msimba si dhambi wala si haramu kwa sababu hili ni maumbile ya mwanadamu kufurahi na kucheka anapopata furaha huwa analia na kuhuzunika anapopatwa na msimba.
Ila tu sharia imeweka makatazo watu wasivuke mipaka wakati wa kufurahi kwa kufanya Mambo yaliyo haramishwa na kumuasi Mwenyezi mungu na vile vile wakati wa huzuni kwa kumsahu Mungu na kusema yasiofaa. Bali muislamu atakikana awe ni mwenye kuchunga mipaka ya Mungu kwa hali zote mbili furaha na msimba.
Amesema Mtume Rehma na amani zimfikie yeye:


عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال { ليس منا من ضرب الخدود ، وشق الجيوب ، ودعا بدعوى الجاهلية   رواه البخاري ومسلم 

Kutoka kwa Abdillah bin Mas'uud Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka Mtume Rehma na amani zimfikie yeye Amesema: [si katika sisi atakae jipiga Matavu (wakati anapo patikana na Msiba) na kupasua Mivuko (nguo) na kuita miito ya kijahiliya]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na dini yetu si dini inayopenda misiba na kuwa watu wawe ni wenye kukaa na kujitia huzuni kila wakati. Ndio pale sheria ikaruhusu watu waliofiliwa wakae siku tatu wala wasizidishe na hizi siku tatu ni kwa wale watu wa nyumbani waliofiliwa ili wapate kutaazi kwa wale watu wanaoishi mbali.
Lakini kwa dini ya Mashia hili la kuomboleza kwao ndio dini. Utawaona daima wako Makaburini waomboleza na kulia na utakuta bid'aa zote zinazo ambatana na kifo na tanzia utakuta zimetoka kwao.
Na isitishe wameweka mlango Makhsusi wa watu kumililia sayyidnal Husein na wameweka hadithi chungu mzima kwa fadhla za kumlilia sayyidal Hussein radhi za Allah ziwe juu yake.
Miongini mwa hadithi za uzushi na hadithi hizi.


قال الصادق (ع) : " من ذَكَرنا أو ذُكرنا عنده فخرج من عينه دمعٌ مثل جناح بعوضة ، غفر الله له ذنوبه ولو كانت مثل زبد البحر ". أمالي الصدوق مجلس 17 رقم4 ص 278

Amesema Al-Swaadiq (A.S.) "Mwenye kutukumbuka au tukatajwa mbele yake yakatoka kwenye macho yake chizi mfano wa umbu, basi Mwenyzi Mungu atamsamehe dhambi zake japo kuwa dhambi zake ni kama povu la baharini."     [Amaali Swaduuq kikao cha 17 namba 4 ukurasa 278]

Na katika hadithi nyingine za uzushi ni hadithi hii.

كان علي بن الحسين (ع) يقول : " أيمّا مؤمن دمعت عيناه لقتل الحسين بن علي دمعة حتى تسيل على خدّه ، بوّأه الله بها في الجنة غرفا يسكنها أحقابا" أمالي الطوسي ص34

Alikuwa Ali ibnul –Husein (A.S.) Akisema:  "Muumin yoyote macho yake alitokwa na machozi kwa kifo cha Husein bin Ali chozi lililo tiririka kwenye tavu lake mwenyezi mungu atamuandalia kwa chozi hilo ghorofa katika pepo aishi humo milelele"   [ Amaali Al-Tuusiy ukurasa 34].

Na kutoka na Hadithi hizi walizo wasingizia maimamu wao ndo utaona majabu na vituko juu hili,mtu atafuta kujiliza kwa namna yoyote ile hata kama hana kilio.

Na utaona siku ya Ashuraa wameibadilisha kuwa ni siku ya huzuni kila mwaka kutoka mabarabarani na kujipiga mapanga na visu wakihuzunika kwa kifo cha Husein,kisha utasikia arbainiyatul Husein na kadhalika.

Mtazame huyo Sheikh wao,hiko ni kicheko ama nikilio?




 


 


HII NISHAHADA YA KUMUINGIZA MTU PEPONI AMA MATONI ?


Sote tunajua kuwa mtu anapo taka kusilimu nilazima kwanza apige shahada mbili,nao ni kusema

Ash'hadu an laailaha illa Allah,Wa'ash'hadu anna Muhamadan Rasulullah.  

Nakuiri kwa myo na kubaini kwa ulimi ya kuwa hapana mola apase kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi mungu na kuwa Mtume Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Na mtu anapo piga shahada huwa ashakuwa Muislamu,na haya ndio Mafundisho tulio funzwa na Qur'ani na Sunna za bwana mtume Muhamad Rehma na amani zimfikie yeye.

Asema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

 

 {شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ}      آل عمران:18

[Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.]       [Al-Imraan:18]

Na katika Hadithi Mtume  amesema:

[أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى : يَشْهَدُوا أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ]  رواه البخاري ومسلم

[Nimeamrishwa nipigane na watu Mpaka washuhudie yakuwa hapana Mola apase kuabudiwa kwa haki ila MwenyeziMungu na kuwa Muhamad ni mtume wa Mungu.]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na Mtume alipo mpeleka swahaba wake Muaadh Radhi za allah ziwe juu yake Yamen alimwamrisha kwanza awalinganie watu katika Tawhiid Kumuamini mungu mmoja na mtume wake. na mtu akishuhudia hivyo huwa ashakuwa muislamu.

Lakini la ajabu na kushangaza ni kwa hawa Mashia hilo halimtoshi mtu kuwa Muislamu mpaka 

ashuhudie na mashahada mengine ili awe Muislamu.

Ushudie kuwa Abubakr na Umar na Uthman Bibi Aisha kuwa ni watu wa Motoni.

Na ushuhudie kuwa Sayyidna Ali radhi za allah ziwe juu yake ni walii wa mungu na Bibi Fatima na watoto wake ni wasii wa Allah.

Ajabu kubwa sana, yaani ukitaka kuwa Muislamu mpaka ushudie yakuwa bibi zake Mtume ni watu wa motoni,na Maswahaba wake watukuf walio itetea hii dini kwa hali na mali,pia ushuhudie kuwa ni watu wamotoni.  Subhanallah!

Ndio tukauliza Hizi ni shahada za kumuingiza mtu motoni ama peponi?

Na hili japo kuwa hawakuandika kwenye vitabu vyao kwa sababu ya (Taqqiya) lakini kwa sasa mashekhe wao wabainisha wazi katika mafunzo yao na wanapotaka kumuingiza mtu kwenye Ushia. japo kuwa Masheikhe wakishia walioko Africa hawajakuwa na ujasiri wa hilo.

Tazama huyu hapa sheikh wakishia akimtemsha Shahada alietaka kuwa Mshia.



 

PEPO  AU KUMLILIA HUSEIN RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE?? 

 

Kuingia peponi ndio matakwa ya kila muislamu na muimin,kwa sabubu pepo ndio bidhaa ilio ghali kama alivyo sema mtume wa Mwenyezi Mungu,na waumini walipo acha starehe za dunia na kufanya ibada kwa wingi lengo ni kutaka Radhi za Mungu na Mwishowe waingizwe peponi.
Kama mwenyezi Mungu alaiyetukuka aliyo sema kwenye kitabu chake kitukufu:

 

إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ     التوبة:111

 

[Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,]      [Tawba:111

Kwa sababu hiyo ndio utona Waumini wako teyari kujitolea kwa lolote lile kwa ajili ya kupata radhi za Mungu pepo.
Na Mwenyezi Mungu yeye ndie aliesema kuwa atakae epushwa na moto na kuingizwa peponi huyo ndie aliefaulu.

فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ}     آل عمران:185}

"Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu"    [Al-Imraan:185]

Na vile vile Manabi na watu Wema walikuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu awaingize kwenye pepo yake,na kila Muislamu matarajio yake ataka aingie peponi na awe ni katika watakao ambiwa:

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ }   النحل:32} 

 

[Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia:Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda.]     [Al-Nnahl:32]


Laikini la ajabu na lakushangaza ni kwa hawa Mashia pepo kwao silo lamuhimu sana,lamuhimu kwao ni kumlilia Sayyidnal Husein,wako radhi lau watakhiyarishwa wakifa waingie peponi au wakae duniani kwa ajili ya kumlilia husein watakhiyari kubaki dunani ili wapatai kumlilia Husein kama hili la kulia ndilo lengo kubwa la huyu Mwanadamu.


                 MSIKILIZE MWANACHUONI WAO ANAVYOSEMA 




Labda mtu huweza akajadili kuwa huo sio msimamo wa mashia wote,ni kweli huenda ikawa ni hivyo lakini mbona hatupati mwanachuoni wa kishia alie mrudi na kumpinga kuwa si sawa ?
Mashia hili la kumlilia Husein kwao limekuwa ni ibaada kubwa,kama kwamba dini imeamrisha kufanya hivyo haliyakuwa dini limekataza watu kuommoleza katika Msiba amesema Mtume rehma na amani zifikie yeye sikatika sisi atakae jipiga matafu,na kupasuwa mifuko (nguo) na kuomba maombi ya kijahiliya.


HAWA NI MIUNGU AMA NI MAIMAMU?

 

Mwenyzi Mungu aliyetukuka ndie peke yake Mwenye sifa za ukamilifu na ndie mumba mbingu na aradhi na viliomo 

baina yake.Yeye peke ndie anaejua ilimu ya gheyb na hana mshirika na yoyoye katika umbaji wake wala kuabudiwa kwake.

Allah anasema katika kitabu chake kitukufu:

{قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ}   النمل: 65

 

[Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.]     [Al-Naml:65]

Hata manabii walio tumilizwa wala Malaika walio karibu hawajui ilimu ya Gheyb ila kwa wale walifunuliwa na yeye Allah Subhnahu Wataala.

Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

{عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَى غَيْبِهِ أَحَدًا * إِلَّا مَنِ ارْتَضَى مِنْ رَسُولٍ}     الجن:26-27

"Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia."

Lakini la ajabu na Kushangaza ni kwa itikadi za hawa Mashia wanodai Uislamu.Hebu tuangalia namna wanavyo

itakidi kwa Maimamu wao kwa mujibu wa vitabu vyao wanavyo vitegemea.

Maimu wajua ilimu ya Gheyb.

Yamekuja katika kiabu chao wanacho kiegemea zaidi [Al-Kaafiy]

قال أبو عبد الله " إني لأعلم ما في السماوات وما في الأرض وأعلم ما في الجنة والنار وأعلم ما كان وما يكون" (الكافي 1/204 (

Amesema Abuu Abdillah " hakika yangu mimi najua yaliyomo mbinguni na yaliyomo Ardhini na ninajua yaliyomo

Peponi na Motoni na ninajua yaliokuwa na yatakao kuwa."  Al-Kaafiy   1/204

Wanauwezo wakufisha na kuhuisha.

Kama yalivyo kuja kwenye kitabu chao "Bihaarul- Anwaar"  

وقال سلمان -كما يفترون-: "لو أقسم أبو الحسن على الله أن يحيي الأوّلين والآخرين لأحياهم" [بحار الأنوار: 41/201، الخرائج والجرائح ص82]

Na Amesema Salmaan " lau angeapa babayake Hassan juu ya Mwenyezi Mungu amfufulie wa mwanzo na wamwisho

basi Mungu angewahuisha.

[Bihaarul-Anwaar 41/204 na kitabu cha Al-Kharaaij wal-Jaraaih uk.82

Na waitakidi kuwa Maimu wanajua siku ya kufa kwao na Imamu asiejua hayo basi huyo hajakuwa Imamu wa kweli.

Ndio tukauliza hawa ni Maimamu ama ni Miungu?

Ndio utaona Mashia badala ya Kumuaomba Mungu wanapo kuwa na shida  wao huwaomba Maimamu wao,Badala

 ya kusema Yaa ALLAH, Yaa Rahmaan wao husema Yaa ALI.Yaa Husein.


Msikile Mmoja katika Mashekhe wao vile anavyo sema Kuhusu Maimu wao


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6573205
TodayToday1272
Highest 01-07-2025 : 4073
US
Guests 28

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6828805165f2c14425291671747484753
title_682880516609220070414281747484753
title_68288051661f620077692031747484753

NISHATI ZA OFISI

title_6828805172bb817862585991747484753
title_6828805172c9f19696253711747484753
title_6828805172d752060209851747484753 Add content here

HUDUMA MPYA

: 10 + 14 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com