EWE ALI, WEWE KWANGU NI KAMA MFANO WA HARUNI KWA MUSA
Katika shubuhati za mashia katika kuitetea itakadi yao ya Uimamu ni hadithi ya Bwana Mtume alipomwambia Sayyidna Ali Radhi za Allah ziwe juu yake,
يا علي أنت مني بمنزلة هارون من موسى إلا أنه لا نبي بعدي] رواه البخاري ومسلم]
[Ewe Ali, wewe kwangu mimi, ni kama cheo cha Haruun kwa Musa ila tu hakuna Nabii baada yangu]
Mashia wanadai kwa Hadithi hii, kuwa Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake ndie anaestahiki wilaya na Ukahlifa baada ya kufa Mtume ﷺ .
Jawabu:
1. Bila shaka hadihti hii ni swahihi na Imepokelewa na Bukhari na Muslim na wengineo katika wanachuoni wa hadithi,ndio wanachuoni wakiweka katika fadhila za sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake.
Ama walio dai Mashia kuwa Sayyidna Ali (r.a) ndie anaestahiki ukhalifa na uongozi hakuna dalili juu ya hilo katika Hadithi, kwa sababu hadithi hii Mtume ﷺ alimwambia Ali radhi za Allah ziwe juu yake alipomtaka sayyidna Ali abaki Madina wala asishiriki katika vita Tabuuk na walikuwa Maswaba wote wameshiriki na hakubaki Madina ila wanawake,na watoto na watu wenye nyudhuru. Jambo hio likampa taabu Sayyinda Ali kuona amebakishwa na wanawake na watoto,akamwendea Mtume ﷺ na akamwambia:
أتخلفني في النساء والصبيان
Waniacha na wanawake na watoto, ndio Mtume akamwambia :
[أما ترضى أن تكون مني بمنزلة هارون من موسى]
[Je huridhi uwe kwangu mimi ni kama cheo cha Haruun kwa Musa.]
Na kulikuwa baadhi ya wanaafiq wamesema hangemuacha isipokuwa Hampendi, ndio Mtume akamwambia Sayydna Ali maneno hayo.
[ تاريخ الطبري 3/103-104، والبداية والنهاية لابن كثير 5/7]
[Tarekh- Al-Twabariy 3/103-104 na Al-Bidaaya wa Al-Nnihaya ya Ibnu Kathir 5/7]
2. Na hili la kubakishwa mtu Madina halikuwa ni jambo Hasa kwa Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake, bali kuna Maswahaba kadha Mtume aliwabakisha madina wakati anapo taka kwenda vitani au kwenda Umra au hajji.
Katika vita vya Badru alimbakisha Abdullah ibnu Ummi Maktuum,Radhi za Allah ziwe juu yake
Na katika vita vya Baniy Sulaym,alimuweka Madina Sibaa'I bin Urfatwa Al-Ghifaariy,na katika vita vya Al-Ssawiq alimuweka Bashir Ibnu Al-Mundhir,na katika vita vya Baniy Al-Mustaliq alimuweka Abuu Dhari Al-Ghifariy na katika vita vya Al- Hudaybiyah alimuweka Numayla bin Abdillah Al-Laythiy na wakati wa kwenda kukomboa Makkah alimuweka Kalthum bin Husweyn bin Utba Al-Ghifay,na katika Hijjatul widai (Hijja ya kuaga) alimuweka Abuu Dujaana Al-Ssaidiy
[Tizama sera ya Ibnu Hishaam 2/650,804,806 3/1113-1133-1154]
Kwa hiyo hilo la kubakishwa Ali radhia za Allah ziwe juu yake. Kubakishwa Madina halikuhusishwa Sayydna Ali peke yake, bali walishirikishwa maswhaba wengine pia, kwa hivyo Mashia hawana hoja katika hadithi kuwa Ali ndie anaestahiki Ukhalifa kwa kudai kuwa Mtume alimuweka Madina awe ni khalifa wake.
Na wanachuoni wamelielezea hilo zamani kuwa Mtume alimwambia sayyidna Ali hilo ili kumridhisha na asihisi vibaya hasa pale wanaafik walipo sema kuwa amemchosha ndio akachukia kufuatana na yeye.
Na kufananishwa kwake na Harun ni pale Musa alipo muacha ndugu yake Harun na yeye kuenda kunon’gona na Mola wake, kisha Mash-huri cha Nabii Musa ,amani ya Mungu iwe juu yao.
3. Na Haruun (a.s) hakuwa khalifa wa Nabii Musa, kwa sabubu Haruni alikufa katika uhai wa Nabii Musa,na Kabla ya kufa Nabii Musa (a.s.) kwa Miaka arubaini kwa hivyo hakuna hoja ya kudai kuwa Sayyidna Ali ndie anaestahiki ukhalifa kwa kufananishwa na Haruun.
Na kule kuambia kuwa wewe ni kama cheo cha Harun kwa Musa ni kwa sababu ya ujamaa wala si kwa lengine.
Kwa hivyo hoja hii wanadai mashia si hoja ya msingi wala hakuna dalili kwa yale wanaodai kuwa Sayyidna ali ndie anaestahiki ukhalifa kwa hadithi hii.
4. Kisha Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake alipa Bay'a Sayyidna Abubakar radhi za Allah ziwe juu yake, na kumkubali awe ndie khalifa wa Waumini baada ya kufa Mtume ﷺ ikiwa Sayyidna ali alifahamu nasi ya hadithi hii, kama walivyo ifahamu Mashia ni kwa nini basi ampe Bay'a Sayyidna Abubakr hali ya kujuwa kuwa yeye ndie anaestahiki ukhalifa ?
DAI LA KUPIGWA BIBI FATIMA(R.A) NA MASWAHABA
Katika shubuhati wanazo dai Mashia kuwa kikundi cha maswahaba kikiongozwa na Sayyidna Umar na Khalid bin Al-waleed radhi za Allah ziwe juu yao walivamia nyuma ya bibi Fatima radhi za Allah ziwe juu yake. Wakampiga mpaka akaangusha mimba yake na kumvuda mkono wake na kumchomea nyumba yake. Kisha kumtoa Sayyinda Ali (r.a.) kwa nguvu na kumlazimisha kwenda kuumpa (Kumvoti) sayyidna Abubakar (r.a)
Jawabu:
Kwanza hakuna riwaya swahihi ya kisa hiki cha urongo katika vitabu vya Ahlu Sunna vya kutegemewa. Kisa hiki kinaelezewa katika vitabu visio tegemewa vilivyo pokelewa na watu wasio julikana, watu warongo na baadhi wananukuu bila ya kuwa na Isnaad yoyote ile.
Na lau kitasihi kisa hiki basi kitathibitisha jambo baya sana kwa hao wanadai kisa hiki na kuonyesha haya yanayo fuata:
1. Kuutia dowa ushujaa wa Sayyidna Ali (r.a) kwani akijulikana ushujaa wake kama ilivyo kuja kwenye sifa zake,
Vipi ataridhia kwa kupigwa mke wake mpaka kuangusha mimba na kuvunjwa mkono na kuchomewa nyumba bila ya kumtetea? Tena aliye fanyiwa hivyo ni binti wa mtume wake, na binti ya ibnu Ammi yake.
Kwali hilo la ingia akilini?
Ikiwa mtume amesema :
[ومن قتل دون أهله فهو شهيد] رواه أحمد]
[Mwenye kuuliwa akitetea Ahli yake basi yeye ni Shahid] [Imepokewa na Ahmad].
Na fadhla hizi ni kwa Muislamu yoyote yule atakae simama kumtetea ahli yake.
Je? Itakuwaje kwa swahaba mtumkufu Sayyidna Ali radhi za Allah ziwe juu yake iwe atamuache mkewe na asimtete hata kama atauliwa juu ya jambo hilo.
Kwa hivyo kisa hicho wanacho kidai Mashia kwanza chamtia doa kwa Imamu wao wa kwanza.
2. Ikiwa mashia watadai kuwa Sayyidna Ali hakuweko pindi alipo pigwa bibi Fatima radhi za Allah ziwe juu yake.
Jawabu:
Hilo pia itakuwa ni kuvunda itikadi yao juu ya Maimamu wao kuwa wanajua mambo ya gheyb.
Vipi imamu Ali asijue tukio hilo na ilhali mwadai kuwa maimamu wanajua mambo yalio fichika? Na hapa ni lazima mukubali moja katika mawili:
1. Ima mukubali kuwa itikadi ya kuamini kuwa mimamu wajua gheyb ni itikadi batili?
2. Ama mukubaki kuwa wajua gheyb na Sayyidna Ali alikuwa ajua tukio hilo la kupigwa kwa bibi yake, na hili itakuwa mwamtuhum Sayyidna Ali kuwa alikuwa muoga?.
Kwa hivyo chaguo ni lenu.
Na kisa hiki kimepingwa na mwanachuoni wa kiishia katika nchi ya Libanon Mahamad Husein fadhlullah.
Subhanallah !!
Mashia wamekibuni kisha hiki kwa kutaka kuwatia doa Maswahaba wa bwana Mtume ﷺ lakini hawakujua kuwa wamtia doa Imamu wao.
3. kisha vipi Sayyidna Ali amuozeshe binti yake Ummu Kalthum mume ambae alimpiga mama yake, na kumchomea nyumaba yake?
Huko ndiko kuhifadhi tangamano la ndoa yake na bibi Fatima (r.a)
Hivi ndivyo wanavyo lipwa madhaimu?
Bila shaka si hivyo wala Sayyinda Ali hakuwa hivyo, bali alikuwa ni shujaa alie kuwa haogopi kufa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Yeye ndie fi-dai (Shujaa) wa kwanza katika dini pindi alipo lala katika kitanda cha Mtume siku ya hijra bila ya kujali wala kufikiria
Lakini hiki ni kisha cha kubuniwa na Mashia kwa lengo la kutaka kuwatuhumu maswhaba wa Mtume lakini lengo lao halikutimia.
Ni wale walio potea warudi katika dini ya haki, na wasifuate batili bali waregee katika mafundisho ya Qur'ani tukufu na hadithi za Bwana Mtume ﷺ zilizo sahihi.
SHUBHA YA KURITADI KWA MASWAHABA
Mashia wanadai kuwa Maswahaba waliritadi baada ya kufa Mtume Muhammad na hakuthubutu katika uislamu ila wachache na katika hoja yao hiyo wanaitolea dalili aya ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
وما محمدٌ إلا رسول قد خلت من قبله الرسل أفئن مات أو قتل انقلبتم على أعقابكم ومن ينقلب على عقبيه فلن يضر الله شيئاً وسيجزي الله الشاكرين آل عمران آية 144
"Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru" [Al-Imraan:144]
Wanasema kuwa aya hii yaonyesha wazi kuwa Maswahaba wataritadi baada ya kufa Mtume ila wachache wenye kuwa na shukrani ,kama alivyo sema Mwenyezi Mungu:
{وقليل من عبادي الشكور} [سورة سبأ آية 13]
"Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru" [Saba'i:13]
Jawabu:
Kwanza kabisa yaonyesha wazi ujinga na kutoelewa kwa wanaosema maneno hayo. Lau angesoma kitabu chochote cha tafsiri na kuangalia sababu ya kuteremka aya hii hawangesema walio yasema.
Aya hii imeteremka siku ya vita vya Uhud wakati walipo pata waislamu waliyo yapata kwa kuuliwa Maswhaba sabiini na kupasuliwa uso Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuvunjwa meno yake. Pia watu kueneza uvumi kuwa Mtume ameuliwa,hapo ndipo baadhi ya wanafiki waliposema ikiwa Mtume Muhamad ameuliwa basi regeeni katika dini yenu ya kwanza yaani ushirikina ndio ikateremka aya hii
{وما محمدٌ إلا رسول قد خلت من قبله الرسل أفئن مات أو قتل انقلبتم على أعقابكم ومن ينقلب على عقبيه فلن يضر الله شيئاً وسيجزي الله الشاكرين}
[سورة آل عمران آية 144]
"Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume. Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? Na atakaye geuka akarudi nyuma huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru" [Al-Imraan:144]
Amepokea imam Al-Twabariy kwa Isnadi yake katika tafsri yake kutoka kwa Al-Dhwahak amesema katika neno lake Mwenyezi Mungu:
{وما محمد إلا رسول قد خلت من قبله الرسل}
"Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume.'
Watu walio kuwa na shaka na maradhi na unafiki walisema siku watu walipomkimbia Mtume na kupasuliwa juu ya uso wake na kuvundwa meno yake,Muhamad ameuliwa rudini kwenye dini yenu ya kwanza, hilo ndilo neno lake Mwenyezi Mungu:
{أفئن مات أو قتل انقلبتم على أعقابكم}
Je, akifa au akauwawa ndiyo mtageuka mrudi nyuma? [Tafsiri Al-Twabariy 3/458]
Kwa hivyo aya iliteremka juu ya wanafiki walio eneza uvumi kwa kuuliwa Mtume na kutaka Maswhaba Warudi kwenye ushirikina dini ya mababu zao.
Wala aya haijazungumzia kabisa kuhusu Kuritadi Maswahaba baada ya kufa Mtume kama wanavyo dai Mashia.
Pili: Hata aya kama imeteremka juu ya Maswahaba baada ya kufa Mtume itakuwa ni dalili ya wazi kuwatakasa Maswahaba kwani wao ndio walio anda jeshi lakupigana na Murtadina.
Abubakar Swidiq na Maswahaba ndio walio simama imara kupigana na walio ritadi mpaka akawarudisha kwenye dini na wale walio kataa kurudi aliwapiga,na hili laonyesha wazi ubora wa swahaba wa Mtume (S.W.A).hasa Abubakar na Fadhla yake juu ya kuitetea dini hii.
Ndio imepokewa kwa sayyidnya Ali radhi za allah ziwe juu yake katika neno lake Mwenyezi Mungu:
{وسيجزيالله الشاكرين}
"Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanao mshukuru"
[الثابتين على دينهم أبا بكر وأصحابه]
"Wenye na thabati juu ya dini yao, Abubakar na Maswahaba wake" [Tafsiri Al-Twabariy 3/455].
Ndugu Muislamu tazama hawa Mashia namna wanvyogeuza aya za Mwenyzi Mungu bila ya kujali wala kumuogopa Mwenyezi Mungu.
Wamewasingizia maswahaba wa Bwana Mtume Muhamad kuwa waliridadi baada ya kufa kwake ilhali hawa Maswahaba ndio walio simama imara kupigana na walio ritadi mpaka kuwamaliza na Uislamu kuenea ulimwengu Mzima.
Na hawa Maswahaba Allah amewasifu kwenye kitabu chake kitukufu,na wao ndio walio isambaza hii dini mpaka kutufikia sisi, na hili liko wazi kwa kila mwenye akili na fahamu mzuri lakini hawa mashia chuki zao juu ya Maswahaba wamebadilisha mazuri yao kuyafanya mabaya,na kuwabadikia ubaya badala ya uzuri.
ATAKAE KUFA NA ASIMJUE IMAMU WA ZAMA ZAKE BASI ATAKUFA KIFO CHA JAHILIA
Katika shubuhati za mashia katika kuithibitisha itikadi hii ya uimamu ni hadithi hii ambao utaipata katika vitabu vyote vya kishia
[من مات ولم يعرف إمام زمانه مات ميتة جاهلية]
[Atakae kufa na asimjue imamu wa zama zake atakufa kifo cha Jahilia.]
Na kudai kuwa hadihti hii iko katika vitabu vya ahlu Sunna.
Jawabu
Hadithi kwa tamko hilo au kwa swigha hii wanavyodai Mashia Hakuna katika vitabu vya Ahlu Sunnah
Asema Sheikh Al-Albany Mungu amrehemu katika kitabu chake [Al-Silsilatul Ahadithi Dhwaifa wal-Maudhua 1/525]
"Atakae kufa na asimjue imamu wa zama zake atakufa kifo cha jahilia."
Haina asili kwa lafdhi hii.
Na amesema Sheikhul-Isalaam Ibnu Taymia "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu hajasema Mtume hivi,linalo julikana ni Hadithi ilio pokelewa na Imam Muslim kutoka kwa Ibnu Umar amesema nimemsika Mtume ﷺ akisema:
ما روى مسلم أن ابن عمر قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: " من خلع يدا من طاعة لقي الله يوم القيامة ولا حجة له، ومن مات وليس في عنقه بيعة مات ميتة جاهلية
[Atakae vua mkono wa utiifu (kwa kiongozi) atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa hana hoja,na atake kufa na hana katika shingo yake Bay'a atakufa kifo cha jahiliya.]
Kwa hivyo hadithi wanao dai Mashia haikupokewa kinamna hiyo wanavyo dai,bali wamebadilisha temko la Hadithi.
Kisha hata kama hadithi yao ni swahihi haina dalili juu ya itiadi yao ya kudai maimamu kumi na mbili.
Na kudai kwao kuwa hadithi hii iko katika vitabu vya Ahlu sunna ni kutaka kuwadanganya wenye ilimu chache kwa sabubu ya kufana matamshi yake.
Na hadithi inahimiza waislamu wawe watiifu kwa viongozi wao, na wasiwe niwenye kuasi.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.