SOMO LA FIQHI YA KUAMILIANA


somo lafiqhi


Vigawanyo vya uamuzi:
Uamuzi una vigawanyo vifuatavyo:
Mwanzo: Uamuzi wa mkao (majlis):Nayo ni sehemu ambayo Uuzaji inafanyika, hapa muuzaji na mnunuzi wana uamuzi wa kufanya au kutofanya biashara maadamu hawajatengana kati yao; kwa hadithi ya Ibn Omar Mwenyezi Mungu awaele radhi

 

 المُتَبَايِعَانِ كُلُّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا بِالخِيَارِ عَلَى صَاحِبِهِ مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا ]     رواه البخاري ومسلم]

 

[Muuzaji na Mnunuzi kila mmoja kati yao ana uamuzi maadamu hawajatengana][imepokewa na Bukhari (21112) na Muslim (1531).]

Pili: Uamuzi wa masharti (sharti): Nalo ni sharti Linaloekwa na muuzaji au mnunuzi kupewa muda maalum na ukiisha muda huo bila ya malalamishi yoyote basi biashara itawajibika kati yao. Mfano wake mtu anunue gari kisha aseme: Nipe muda kiasi cha mwezi mmoja, kutokana na hayo hana haki ya kurudisha gari maadamu muda haujamalizika na ukimalizika muda huo itamlazimu anunue gari hilo.

Tatu: Uamuzi wa aibu (upungufu): Nao pale mnunuzi anapoona bidhaa iko na aibu (upungufu) na hajafahamishwa na muuzaji awali au muuzaji pia hajui mapungufu hayo, sharti yawe mapungufu hayo yanapunguza thamani ya bidhaa. Hapo mnunuzi ana uamuzi wa kuendelea na biashara na kuchukua malipo yanayotokana na mapungufu hayo (tofauti kati ya bei ya bidhaa na bei ya bidhaa ikiwa na mapungufu) au ana haki ya kurudisha bidhaa hiyo, na inapaswa kwa muuzaji arudishe pesa.

Nne: Uamuzi wa udanganyifu (Tadlis): Nao ni udanganyifu anaofanya Muuzaji juu ya Mnunuzi, na tendo hili limeharamishwa katika Uislamu; kwa neno lake Mtume aliposema

 

مَنْ غَشَّنَا فَلَيْسَ مِنَّا]   رواه مسلم]

 

[Mwenye kufanya udanganyifu si katika sisi].   [Imepokewa na Musalim]

Mfano wake awe muuzaji anamiliki gari na lipo na kasoro nyingi ndani yake, na anakusudia kulipamba ili liwe lenye kuvutia na lionekane halina kasoro yoyote. Mnunuzi anapotambua aibu hizo, atakuwa ana haki ya kurudisha gari hilo kwa muuzaji na kudai pesa zake.


comments