Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suali: Ni nini Maana ya zaka kilugha na kisheria

Jawabu: Zaka kilugha.
Ni kukua kwa kitu na kuzidi.

Na Maana ya Zaka kisheria.
Ni kiwango maalumu cha mali kinachotolewa wakati maalumu ili kupewa watu maalumu.

Suali: Ni upi umuhimu wa kutoa Zaka?

Jawabu: Umuhimu wa zaka
Zaka ni faradhi katika faradhi za Dini ya Kislamu, na ni nguzo ya tatu katika nguzo za Uislamu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ}   النور:56}

 

[Na shikeni Sala, na toeni Zaka, na mt'iini Mtume, ili mpate kurehemewa.]  (Suratu An-Nur: 56),

Na akasema Mtume ﷺ:

 

بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان  رواه البخاري ومسلم 

 

[Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

 

Suala: Ni ipi hukmu kwa anaekataa kutoa Zaka?

Jawabu: Hukmu ya Anayekataa kutoa Zaka, ima awe amekataa kwa kupinga kwamba zaka sio lazima kutoa,  Nakukataa kuwajibishwa kwake. au kukataa kwa ubakhili.hukmu yake ni kama ifuatavyo:

1. Mwenye kukataa kutoa Zaka kwa kupinga.
Anayepinga wajibu wa Zaka basi amekufuru kwa makubaliano ya umma wote – ikiwa mtu huyu anajua vizuri wajibu wa Zaka; kwa sababu atakuwa amemzulia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

2. Anayekataa kutoa Zaka kwa ubakhili.
Atakayekataa kutoa Zaka kwa ubakhili wake basi huchukuliwa kutoka kwake Zakaa kwa nguvu na wala hawi kafiri kwa kufanya hivyo kukataa kutowa Zaka kwa ubakhili.

Na atakuwa ametenda dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa na ni uovu mkubwa sana.

Kwa kauli ya Mtume kuhusu wanaokataa kutoa Zaka:

 

قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَا مِنْ صَاحِبِ ذَهَبٍ وَلَا فِضَّةٍ لَا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا إِلَّا إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ صُفِّحَتْ لَهُ صَفَائِحَ مِنْ نَارٍ فَأُحْمِيَ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَيُكْوَى بِهَا جَنْبُهُ وَجَبِينُهُ وَظَهْرُهُ كُلَّمَا بَرَدَتْ أُعِيدَتْ لَهُ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ حَتَّى يُقْضَى بَيْنَ الْعِبَادِ فَيَرَى سَبِيلَهُ إِمَّا إِلَى الْجَنَّةِ وَإِمَّا إِلَى النَّارِ.

 

[Mtu yeyote aliye na hazina ya dhahabu na fedha na wala haitolei Zaka basi atachomwa nayo katika moto wa Jahannam na itajaaliwa kama vinoo ambavyo atapigwa navyo kwenye migongo na vipaji kila akipata ubaridi (yakipoa makali ya moto) anaregelewa tena (kupigwa navyo), mpaka Allaah Amalize kuhukumu waja wake siku ambayo ni sawa na miaka elfu khamsini. Kisha ndio ataoneshwa njia yake ikiwa ni ya peponi au motoni]

[Imepokewa na Bukhari.]

Na lau atapigana na kukataa kutekeleza amri ya zaka basi mpigeni vita mpaka arudi katika kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, na atoe zaka, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ}     التوبة:5}

"Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu."    [Suratu At-tawbah: 5]

Na kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

 

أمرت أن أقاتل الناس حتى يشهدوا أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، ويقيموا الصلاة ، ويؤتوا الزكاة ، فإذا فعلوا ذلك ، عصموا مني دماءهم وأموالهم ، إلا بحق الإسلام ، وحسابهم على الله تعالى    رواه البخاري ومسلم

 

[Nimeamrishwa niwapige watu vita mpaka washuhudiye ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe Swala, na watoe Zaka, watakapofanya hivyo basi imeharamishwa kwangu damu yao na mali yao isipokuwa kwa haki ya Uislamu, na malipo yao yako kwa Mwenyezi Mungu]     [Imepokewa na Muslim.].

Na Abubakar Radhi za Allah ziwe juu yake alimpiga vita mtu yoyote ambaye alipinga wajibu wa zaka, na akasema:

 

والله لأقاتلن من فرق بين الصلاة والزكاة فإن الزكاة حق المال ، والله لو منعوني عقالا كانوا يؤدونه إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم لقاتلتهم على منعه

 

[Naapa kwa Mungu ya kwamba nitampiga vita yoyote aliyetenganisha kati ya Swala na Zaka, kwa hakika hiyo Zaka ni haki ya mali, Wallaahi kama wakinizuilia hata kwa (kamba ya) kutiwa shemere (anayofungwa mnyama kwenye pua zake) nitapambana nao madamu walikuwa wakiitoa kwa Mtume]     [ Imepokewa na Bukhari.]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487589
TodayToday695
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 65

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e65945cc0713057797111735288212
title_676e65945ccf42268906231735288212
title_676e65945cdd718434597751735288212

NISHATI ZA OFISI

title_676e65946961416616047581735288212
title_676e6594697c35673028041735288212
title_676e6594699e65775449061735288212 Add content here

HUDUMA MPYA

: 1 + 2 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com