Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


1. Kuhudhurisha nia moyoni.

2. Kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kusema “bismillah”

3. Kuosha vitanga viwili vya mikono (mara tatu)

4. Kupiga mswaki: na mahali pake ni wakati kusukutua.

5. Kusukutua na kupaliza maji puani na kuyatoa.(mara tatu)

6. Kuosha uso (mara tatu) pamoja na kupitisha maji ndani ya ndevu.

Na mpaka wa uso kiurefu ni kuanzia mameleo ya nywele za kichwa mpaka chini ya kidevu, na kiupana ni kuanzia sikio mpaka sikio.

7. Kuosha mkono wa kulia kuanzia ncha za vidole mpaka kifundoni (mara tatu), kisha mkono wa kushoto kama hivyo.

8. Kupangusa kichwa kwa kuupasha maji mkono kisha kupukusa mwanzo wa kichwa mpaka kwenye kishogo chake kisha kuurudisha mwanzo wake mara nyingine (mara moja).

9. Kupangusa katikati mwasikio kwa kidole cha shahada, na inje yake kwa kidole cha gumba (mara moja)

10. Kuosha mguu wa kulia hadi kwenye vifundo (mara tatu) kisha mguu wa kushoto hivyohivyo.

11. Dua baada ya kumaliza kutawadha kwa kusema:

 

أشْهَدُ أنْ لا إله إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيك لَهُ ، وأشْهَدُ أنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ، اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنَ التَوَّابِينَ ، واجْعَلْني مِنَ المُتَطَهِّرِينَ ، سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ وبِحَمْدِكَ ، أشْهَدُ أنْ لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ ، أسْتَغْفِرُكَ وأتُوبُ إِلَيْكَ

 

[Nashuhudia kuwa hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na mjumbe wake, Ewe Mola! Nijaalie mimi ni kati ya wenye kutubia, na unijaalie mimi ni kati ya wenye kujitwahirisha” Kutakasika ni kwako, ewe Mola! na shukrani ni zako. Nashuhudia kuwa hakuna Mola isipokuwa Wewe. na kuomba msamaha na natubia kwako]    [Imepokewa na Nasai.]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6668174
TodayToday862
Highest 06-05-2025 : 6758
US
Guests 13

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_6866bc9dcf9087453055451751563421
title_6866bc9dcf9f414635767091751563421
title_6866bc9dcfad819072834681751563421

NISHATI ZA OFISI

title_6866bc9dd10af17128838691751563421
title_6866bc9dd119a16157273671751563421
title_6866bc9dd127a9152883041751563421 Add content here

HUDUMA MPYA

: 2 + 11 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com