Menu

SOMO LA FIQHI


 somo lafiqhi


Suala: Ni zipi fadhila za kutawadha

Jabuwabu: Zimepokelewa hadithi kadhaa kutoka kwa Bwana Mtume ﷺ katika kutaja na kuonyesha ubora na fadhila za udhu. Miongoni mwa hadithi hizo ni hizi zifuatazo:

1. Ni sababu ya kupendwa na Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu aliyetukuka Anasema:

 

إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}    البقرة:222}

 

[Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kujitwahirisha]     [Al Baqara: 222].

2. Ni alama ya umma wa Mtume Muhammad kwa kuwa watakuja Siku ya Kiyama wakiwa weupe wa nyuso na viungo vya kutawadha
Amesema Mtume :

 

إِنَّ أُمَّتِي يُدْعَوْنَ يَوْمَ القِيَامَةِ غُرًّا مُحَجَّلِينَ مِنْ آثَارِ الوُضُوءِ، فَمَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمْ أَنْ يُطِيلَ غُرَّتَهُ فَلْيَفْعَلْ]     متفق عليه] 

 

[Hakika ya umma wangu wataitwa Siku ya Qiyama wakiwa weupe nyuso na viungo kutokana na athari ya kutawadha, basi yoyote miongoni mwenu anayeweza kurefusha weupe wake na afanye] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

3. Kunafuta dhambi na makosa
Amesema Mtume ﷺ:

 

مَنْ تَوَضَّأَ ، فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُجَ مِنْ تَحْتِ أَظْفَارِهِ]     رواه مسلم]

 

[Mwenye kutawadha akautengeza udhu wake, basi dhambi zake hutoka mwilini mwake mpaka hutoka chini ya kucha zake]  [Imepokewa na Muslim.].

4.Huinua daraja
Amesema Mtume ﷺ:

 

ألا أدلكم على ما يمحو الله به الخطايا ويرفع به الدرجات ؟ قالوا : بلى يا رسول الله قال : إسباغ الوضوء على المكاره وكثرة الخطا إلى المساجد وانتظار الصلاة بعد الصلاة فذلكم الرباط    رواه مسلم

[Je, nisiwajulishe nyinyi kile ambacho kwacho Mwenyezi Mungu hufuta dhambi na huinua daraja? Wakasema “Ndio, tuonyeshe” akasema: “Ni kueneza maji ya udhu kwenye viungo, na kukithirisha hatua za kwenga misikitini na kungojea Swala baada ya Swala. Hiyo ndiyo jihadi]     [Imepokewa na Muslim.]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487228
TodayToday334
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 70

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e5ab82a64f10914339581735285432
title_676e5ab82a74a19795092731735285432
title_676e5ab82a8473187796501735285432

NISHATI ZA OFISI

title_676e5ab82bff616632213481735285432
title_676e5ab82c0eb18362659641735285432
title_676e5ab82c1de5163565611735285432 Add content here

HUDUMA MPYA

: 6 + 10 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com