Menu

SOMO LA FIQHI


somo lafiqhi


Swala za fardhi ambazo Muislamu amefaradhiwa na Mola wake kuziswali kila siku, mchana na usiku ni swala tano.

Kila moja miongoni mwa swala tano hizi ina wakati wake maalum ambao muislamu anawajibikiwa kuiswali ndani ya wakati huo.

1.ALFAJIRI.
2.ADHUHURI.
3. AL-ASIRI.
4.MAGHRIBI.
5.ISHAA.

Na dalili ya uwajibu wa kuswali mara tano kwa siku zimekuja aya kadha zikishiria nyakati hizi miongoni mwa aya hizo ni neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

 

{فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ  وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ}     الروم:18

 

[Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na asubuhi,Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri.]    [Al-Rruum:18]

 

رَوَى لَيْثٌ عَنْ الْحَكَمِ عَنْ أَبِي عِيَاضٍ قَالَ : قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ : " جَمَعَتْ هَذِهِ الآيَةُ مَوَاقِيتَ الصَّلاةِ : { فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ } الْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ { وَحِينَ تُصْبِحُونَ } الْفَجْرَ { وَعَشِيًّا } الْعَصْرَ { وَحِينَ تُظْهِرُونَ } الظُّهْرَ 

 

Amepokea Al-layth kutoka kwa Al-Hakam kutoka kwa Abuu Iyaadh Amesema: Asema Ibnu Abbas: aya hii imekusanya nyakati za Swala zote "Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni" Maghribi na Ishaa "Mtakaseni Mwenyezi Mungu asubuhi," Al-fajiri "Wa'ashian" Alasiri "Wahiina Tudh'hiruun" Adhuhuri. 

Na neno lake Mwenyezi Mungu:

 

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا}    الإسراء:78}

 

[Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima]         [Al-Israai:78]

Jua linapo pinduka ni Swala ya Adhuhuri na Alasiri, "mpaka giza la usiku" ni Swala ya Maghribi na Swala ya Ishaa "na Qur'ani ya Al-fajiri" ni Swala ya Al-fajri, kama ilivyo pokelewa na Ibnu Abbas na wengine katika Salaf Mungu awarehemu.

 

NA KATIKA SUNNA

 

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا ، " أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ مُعَاذًا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِلَى الْيَمَنِ  فَقَالَ : ادْعُهُمْ إِلَى شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ  وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذَلِكَ فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدِ افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ     رواه البخاري ومسلم

 

Imepokelewa na Ibn Abbaas – Allah awaridhie kwamba Mtume  alimtuma Mua'adh – Allah amridhie – kwenda katika nchi ya Yemen (kulingania dini) akamwamiba:

[Walinganie (Waite) kutamka shahada kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na kwamba mimi Muhammad ni Mjumbe wa Allah, ikiwa wao watalitii hilo (watalikubali) basi wafahamishe kwamba Allah amefaradhisha juu yao swala tano mchana na usiku………]      [Bukhaariy na Muslim.]

Kauli yake Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipomwambia yule mkazi wa majangwani ambaye alimuliza swala zilizo faridhi juu yake.

 

فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَعَلَى آلِهِ وَسَلَّمَ : " خَمْسُ صَلَوَاتٍ فِي الْيَوْمِ وَاللَّيْلَةِ " ، قَالَ : هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُنَّ ؟ ، قَالَ : " لا ، إِلا أَنْ تَطَّوَّعَ     رواه البخاري ومسلم

 

Akasema Mtume :  [Swala tano kila mchana na usiku]  Yule mkazi wa majangwani akamuuliza (tena). Je, ninalazimika na swala nyingine zisizo hizo (tano) (Mtume) akamjibu [Hapana ila swala za suna]        [Imepokewa na Bukhaary na Muslim.]

Na neno lake Mtume :

 

فَرَضَ اللَّهُ عَلَى أُمَّتِي لَيْلَةَ الْإِسْرَاءِ خَمْسِينَ صَلَاةً، فَلَمْ أَزَلْ أُرَاجِعُهُ وَأَسْأَلُهُ التَّخْفِيفَ حَتَّى جَعَلَهَا خَمْسًا فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ]      رواه مسلم]

 

[Amefaridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umati wangu Lailati Israai, Swala khamsini, sikuwacha kumrejelea (Mwenyezi Mungu Mtukufu) na kumuomba kupunguziwa mpaka Akazijaalia tano kwa kila siku - mchana na usiku]       [Imepokelewa na Muslim]


LOGOISLAM

Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6487095
TodayToday201
Highest 12-07-2024 : 5072
US
Guests 49

Mkurugenzi na naibu wake

SS10

 

VIKAO VYA OFISI

title_676e572c3975b21002450911735284524
title_676e572c3984618995593421735284524
title_676e572c399295117024941735284524

NISHATI ZA OFISI

title_676e572c3b06411153331631735284524
title_676e572c3b1584312109401735284524
title_676e572c3b23c15740847021735284524 Add content here

HUDUMA MPYA

: 3 + 8 =

IslamChoice- Kiswahili

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com