SOMO LA FIQHI
1. Kupitisha mpaka katika kusukutuwa na kupandisha maji puani.
Na hii ni kwa ajili ya kuhofia maji yasije yakaingia tumboni mwake, kwa kauli ya Mtume ﷺ:
وبالغ في الاستنشاق إلا أن تكون صائما] رواه أبوداود والترمذي]
[Na fanyeni sana katika kupandisha maji puani isipokuwa wakati mtu amefunga saumu] [Imwpokewa na Abuu Daud na Tirmidhiy.]
2. Kumpiga busu kwa matamanio ya kimapenzi.
Inachukizwa kwa aliyefunga saumu ikiwa anachelea nafsi yake kutokwa na manii au kusisimukwa kwa matamanio ya kimapenzi.
Na ni juu ya aliyefunga kujiepusha na kila ambalo litampelekea kusisimukwa na kuleta harakati za kuibuka matamanio ya kimapenzi, na ikiwa anaamini nafsi yake kwamba haitompelekea katika hisia za matamanio ya kimapenzi basi hakuna kosa kwake kum’busu mkewe au mke kumbusu mumewe; kutoka kwa Bibi A’isha radhi za Allah ziwe juu yake anasema:
كان يقبل وهو صائم، وكان أملككم لإربه] متفق عليه]
[Alikuwa Mtume ﷺ akipiga busu hali yakuwa amefunga na alikuwa ni m’bora zaidi kuliko nyinyi katika kumiliki matamanio ya kimapenzi] [Imwpokewa na Bukharin a Muslim.].
Na kwa ajili hii inachukizwa kubashiriana kimapenzi kwa kijana kinyume na mzee kwa kuwa kijana damu yake ni moto zaidi, kutoka kwa Abu Hureirah anasema:
أن رجلا سأل النبي صلى الله عليه وسلم عن المباشرة للصائم فرخص له، وأتاه آخر فسأله فنهاه، فإذا الذي رخص له شيخ والذي نهاه شاب. رواه أبوداود
[Kwamba kuna mtu mmoja alimuuliza Mtume ﷺ kuhusu kubashiriana mke na mume kwa aliyefunga, Mtume akampa ruhusa ya kufanya hivyo, na akaja mwengine akauliza (swali hilo hilo), Mtume akamkataza, kwani yule aliyempa ruhusa alikuwa ni mzee, na yule aliyemkataza alikuwa ni kijana.] [Imwpokewa na Abuu Daud.]
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.