SOMO LA FIQHI
Makosa na matanabahisho katika kuzuru
1. Kusafiri na kujisumbua kwa safari kwa lengo la kuzuru kaburi na sehemu za turathi zilizoko Madina. Lililowekwa na Sheria ni kufunga safari kuuzuru Msikiti wa Mtume ﷺ, na ziyara ya kaburi yake inaingia ndani.
2. Kuelekea upande wa kaburi Wakati wa kuomba Dua
3. Kumuomba Mtume ﷺ na kutaka haja kwake, badala ya Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na Aliyetukuka, ni miongoni mwa ushirikina mkubwa kabisa.
4. Kujipukusa na kuta za Chumba alichozikwa Mtume ndani yake kwa lengo la kupata baraka ni miongoni mwa mambo ya uzushi yaliyoharamishwa na ni miongoni mwa njia zinazopelekea kwenye ushirikina.
5. Kuinua sauti kwenye kaburi ya Mtume ﷺ na kisimamo kirefu, na kukariri salamu kwa mbali kila anapoingia na kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto juu ya kifua wakati wa kutowa salamu kama vile anavyo fanya akiwa kwenye Swala.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.