SOMO LA FIQHI
Siku ya Kumi na mbili na Usiku wake
Nilazima kualala minaa usiku wa siku ya kumi na mbili, na mchana wake jua litakapo pinduka atatupa vijiwe kwenye jamarati zote kama alivyo fanya siku ya kumi na moja.
Ikiwa atataka kufanya haraka kuondoka siku hii, basi akisha maliza kutupa ataondoka mina kabla ya kutwa jua, ikiwa jua litazama nayeye yuko minaa basi itamlazimu kulala mina na kulazimaka kutupa vijiwe siku ya kumi na tatu, nao nikuzidisha kheri kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَاذْكُرُوا اللَّهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَن تَأَخَّرَ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ لِمَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّكُمْ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ}
[Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika zile siku zinazo hisabiwa. Lakini mwenye kufanya haraka katika siku mbili (akarejea) si dhambi juu yake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kumchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba nyinyi mtakusanywa kwake.] [Al-Baqara: 203]
Na makusudio kwa mwenye kufanya haraka siku mbili katika masiku ya Tashriiq ni siku ya kumi na moja na siku ya kumi na mbili, na mwenye kuchelewa ni akatimiza siku ya kumi natatu.
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.