FIQHI YA IBAADA
Inahisabiwa ni katika miilango muhimu katika somo hili na ndio Mash'huri zaidi na linalo somwa sana,kwa sababu lina lenga kuweka misingi ya ibaada na kuimarisha pia kufungamanisha ibaada na hukmu zake na kitabu cha Mwenyezi mungu na Sunna za bwana Mtume zilizo takasika.
Inafunza fiqhi ya ibaada; hukmu za ibaada alizo kalifiswa mwanadamu kwa ufafanuzi na uwazi kama ilivyo pokelewa kutoka kwa bwana mtume Muhammad Rehma na amani zimfikie yeye na kama ilivyo pokelwa kwa maswahaba watukufu.
Twahar:
Yanafunzwa katika mlango wa twahara mamabo ya fuatayo: Vigawanyo viwili vya twahar,utwahara wa hisia na utwahara wa kimaana.
Vigawanyo vya Maji na hukmu zake,na sampuli za najisi na njia ya kujitwahirisha,Makombo yalio na najisi na yalio twahara, kwenda chooni na yanao pendeza kufanywa na yanao chukiza, Sunna za kimaumbile na kutawadha na hukmu yake pamoja na kutaja Mashri yake na nguzo zake na sunna zake na mambo yanao vunja udhu, pia yanafunzwa na namna ya kupangusa hofu mbili, kupangusa juu ya bendeji na vitata,kila yanao ambatana katika mlango huo, vile vile pia kufunzwa namna ya kuoga janaba na yanao wajibika na yanao pendezwa katika kuoga. Kufunzwa namna ya kutayam’mam na humku yake pamoja na kuelezea hikma yake na yanao paswa kufanya na mambo yanao haribu kutayam’mam,na kufunzwa yote yanao ambatana na Damu ya Hedhi na Istihadha na damu ya nifasi.
Swala
Ni katika mlango muhimu katika fiqhi ya Ibaada na yanayo funzwa katika mlango huu ni maelezo kuhusu swala na yanao ambatana na hukmu yake na namna ya kuswali, kuelezea cheo cha swala na fadhla zake na ninani anae wajibika kuswali na hukmu ya mwenye kuacha swala. Pia kufunza masharti ya swala pamoja na nguzo zake,Wajibati zake na Sunna zake, mambo yanao chukizwa katika swala na mambo yanayo haribu swala. Vile vile pia kuelezea kuhusu Kuadhini na kukimu hukmu yake na fadhala yake na hikma ya kuwekwa adhana na sunna za kuadhini. Kufunzwa sijda mbili za kusahu na sijda ya kisomo na sijda ya kushukuru na yanao ambatana na hukmu zake. Swala ya jamaa na hukmu yake pamoja na kuelezea hikma yake, kufunza kuhusu Mas'ala ya uimamu na kufuatwa kwake na hukmu yake, Swala za watu wenye nyudhuru na namna ya kuswali, pia kuelezea hukmu ya swala ya ijumaa na hikma yake, mashri yake na fadhla zake, kuhusu swala za Sunna na swala ya kuomba mvua na swala ya kupatwa na jua na mwezi pamoja na kuelezea hukmu na hikma na yote yanao ambatana na sunna hizo.
SAUMU
Saumu katika mlango wa fiqhi ni moja katika milago muhimu katika fiqhi ya ibada. Yanao funzwa katika mlango huu ni kuelezea Saumu katika Uislamu, yanao ambatana kuhusu kufunga katika kuelezea hukmu yake na fadhla yake. Pia kuelezea nguzo za saumu na yanaopendekezwa kwa mwenye kufunga na yanao chukiza, yanoa haribu saumu. Pia kueleza Udhuru wa kuacha kufunga mwezi wa ramadhani na kuelezea namna ya kukidhi saumu na katika yanayo funzwa. Ndio katika mlango huu pia yaelezwa Saumu za sunna kwa ujumla na kuelezea fadhala zake na kuhusu usiku wa cheo (laylatul-qadr)na alama zake na fadhla ya usiku huo, kuelezea ibaada ya itikafu hukmu yake na masharti yake na zama za kukaa itikafu, yanayo faa kufanywa na mambo yanao haribu.
ZAKA
Katika mas'ala muhimu yanao funzwa katika mlango huu : ni kuelezea hukmu ya kutoa zaka na Mashrti yake na hukmu ya mwenye kukataa kutoa zaka, Sampuli za zaka na kuelezea hukmu yake na mashrti yake na namna yakutoa zaka, Watu wanofaa kupewa zaka na wasio faa kupewa.
HIJJA
Na katika mlango huu yanafunzwa kuhusu hukmu za kuenda hija na umrah na nyakti zake. Pia nguzo zake pamoja na wajibati zake na sunna zake. Kueleze Mas'ala ya kuvaa ihram na yanayo pendeza na kuchukiza na yanayo haramishwa, yanao ambatana na ibada ya hajji, aina zake,na kuelezea wakti gani inayonza kutolewa talbiya, wakati inayo malizika, pia kuelezea hukmu za fidia na sampuli zake, kuchinja na hukmu yake na namna ya kugawanywa nyama zake na kuelezea fadhla ya kuzuru mji wa Madina pamoja na msikti wa Mtume (S.A.W.) . Kuelezea hukmu ya kuzuru pamoja na Adabu zake, Makosa ya watu wengi wanaofanya.