JE MUME HULAZIMIKA KUGAWA SIKU IKIWA AMESAFIRI NA MMOJA KATIKA WAKE ZAKE?

 

Swali:
Ikiwa mume yuko na wake wawili na akasafiri na mmoja katika wake zake je akirudi kutoka safari huwa ni lazima akidhi siku zile alizokuwa safarini kwa mke aliebaki?

Jawabu:
Mume anapotaka kusafiri na mmoja katika wake zake kwa haja yake mume humlazimu kupiga kura kati ya wake zake, yule kura itakayo mtokea ndie atasafiri na mume wake, na kwa hali hii huwa mume haimlazimu akirudi kutoka safarini kukidhi siku alizo kuwa safarini kwa mke alio baki. Ama safari ikiwa ni kwa haja ya mkewe ima kwa matibabu au kuwazuru jamaa zake, basi mume atakapo rudi atakidhi siku zile alizokuwa safarini na mke yule aliesafiri nayeye, kwa sababu safari ilikuwa ni kwa haja ya mkewe na uadilifu nikuwa akirudi basi huwa ni akidhi siku kama zile.


Na Allah ndie mjuzi zaidi

comments