AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM
Ibn Ishaq anasema miongoni mwa watu waliokuwa katika kundi lililokuwa likimuudhi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ nyumbani kwake ni Abu Lahab, Al-Hakam bin Abi 'AI-Asi bin Umayya, Uqbah bin Abi Muayti, Adiyy bin Hamra AI- Thaqafy, Ibnu Al-Asdaa Al-Hudhaly - na wote hawa walikuwa ni majirani zake. Hakusilimu katika wao mtu yeyote isipokuwa Al-Hakam bin Abi 'Al-Asi. (1)
Watu hawa walimfanyia Mtume ﷺ vituko vingi, upo wakati walikuwa wakimtupia fuko la uzazi la mbuzi na hali yakuwa anasali na wakati mwingine wakimtupia likiwa katika chungu chake. llifikia hatua Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ akatengeneza sehemu ya kusalia ili ajisitiri wakati anaposali, kutokana na mashambulizi yao. Kila walipomtupia alikuwa akilitoa kwa ujiti na kisha husimama mlangoni kwake na kuuliza:
[Enyi Banu Abdi Manafi! Ni ujirani gani huu?] Kisha hulitupa njiani .. (2)
Uqbah bin Abi Mu'ait ndiye aliyekuwa akiongoza katika uovu na ubaya. Imamul Bukhari amepokea kutoka kwa Abdillah bin Masoud (r.a), kuwa, [Mtume ﷺ alikuwa akisali mbele ya Al-Ka'aba, hali yakuwa Abu Jahli na marafiki zake wamekaa pembezoni, ghafla baadhi yao wakawauliza wenzao ni nani kati yenu atakaye leta fuko la uzazi la ngamia wa Banu fulani
ili aliweka mgongoni kwa Muhammad wakati atakapokuwa amesujudu. Aliyekuwa muovu zaidi katika watu wale (Uqbah bin Abi Muayti) 152 akalileta na akangojea, mpaka wakati Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliposujudu akaliweka juu ya mgongo wake kati ya mabega yake. Hali yakuwa mimi ninaangalia, nikiwa siwezi kumsaidia kwa kitu chochote, laiti ningelikuwa ninao uwezo ningelimsaidia. Wakawa wanacheka wakiegemeana kwa furaha, na hali yakuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesujudu hanyanyui kichwa chake, mpaka alipokuja Fatma na kuliondoa lile fuko mgongoni kwake na kulitupa kando. Hapo ndipo alipokinyanyua kichwa chake, kisha akasema: "Ee, Mola wangu wa Haki, ninawashitaki kwako Makuraishi." Aliyasema maneno haya mara tatu. Jambo hilo lilikuwa gumu sana kwao, kwa sababu alikuwa amewaombea dua mbaya, aliwaapiza - na akasema: "Walikuwa wakiamini kuwa maombi katika mji huo yalikuwa yanakubaliwa, aliwataja kwa majina yao, kwa kusema: Ee Mola wangu wa haki ninamshitaki kwako Abu Jahli, Utbah bin Rabia, Shaibah bin Rabia, Al-Walid bin Utbah, Umayya bin Khalaf, na Uqbah bin Abi Muayti na alimtaja mtu wa saba ambaye sikumhifadhi, Ninaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu (s.w.t) Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, niliwaona wale ambao Mtume (s.a.w) alikuwa amewataja wameanguka ndani ya kisima cha Badri."] (3)
Umayya bin Khalaf alikuwa na mazoea ya kumramba kishogo na kumtia dosari kila alipomwona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ, na kwa ajili yake ilishuka aya:
{وَيْلٌ لِّكُلِّ هُمَزَةٍ لُّمَزَةٍ}
[Adhabu kali itamthubutukia kila mwenye kuramba kishogo, msengenyaji.] [104:1]
Ibni Hisham amesema, Al-Humaza: Ni yule ambaye anamshutumu mtu wazi wazi, na anayavunja macho yake na kukonyeza kwa macho hayo, na AI-Lumaza, ni yule ambaye anawatia aibu watu kwa siri na kuwaudhi. (4)
Ndugu ya Ubay bin Khalaf na Uqbah bin Abi Muayti walikuwa ni watu waliokuwa wakielewana, ipo siku Uqbah aliwahi kukaa mbele ya Mtume ﷺ na kusikiliza mawaidha yake. Khabari hiyo ilipomfikia Ubay alimlaumu sana na akataka amtemee mate usoni, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ, akafanya hivyo.
Ubay bin Khalaf mwenyewe aliwahi kuupukuchua mfupa uliochakaa kisha akaupulizia katika upepo upande aliokuwepo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ.
Al-Akhnasi bin Shuraiq Al-Thaqafy alikuwa ni miongoni. mwa watu waliokuwa wakimuudhi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ na Qur'an imemtaja kwa sifa tisa zinazofahamisha juu ya yale ambayo alikuwa nayo. Kwa Kauli Yake MwenyeziMungu (s.w.t) Aliye Mtukufu:
{وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ}
[Wa,la usimtii kila muapaji sana; aliye dhalili Msengenyaji, aendae akitiafitina. Azuiaye kheri, anayedhulumu viumbe wenziwe, anayemuasi Mwenyezi Mungu (s.w.t). Mwenye roho ngumu; (na) juu ya hayo (hana nafuu hata chembe), kama kitu kilichopachikwa kisipachikike vizuri:] [68: 10-13]
Mara nyingi, Abu Jahli alikuwa akienda kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ na kuisikiliza Qur'an, kisha huondoka akiwa haamini na wala haonyeshi utiifu au adabu yoyote ile. Mbali na hayo alikuwa akimuudhi sana Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ kwa maneno. na alikuwa akiwazuia watu wasifuate njia ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Kisha akitoka, akijivuna na akijifakharisha kwa aliyokuwa akifanya katika mambo ya shari, kana kwamba amefanya jambo la maana sana na la kusifiwa. Kwa hilo ikashuka aya hii:
{فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ}
[Hakusadiki wala hakusali] [75:31] 155
Zaidi ya hayo alitaka kumzuia Mtume ﷺ asifike katika Haram Tukufu. llitokea wakati mmoja Mtume ﷺ alikuwa akisali katika ua wa Nyumba Takatifu. Abu Jahl akawa akimtisha na kumtukana. Mtume ﷺ alimkaripia Abu Jahl, naye akalipiza kwa kudai kuwa alikuwa Mkuu wa Makka. Mwenyezi Mungu ﷻ Aliteremsha aya ifuatayo:
{فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ}
[Basi na awaite wanachma wenzake (wamsaidie).] [96:17] (6)
Tukio hili limesimuliwa kwa maneno mengine kuwa, Mtume ﷺ alimkaba Abu Jahl shingoni akamtikisa kwa nguvu huku akisema:
{أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ ثُمَّ أَوْلَىٰ لَكَ فَأَوْلَىٰ}
Imekunsha kukufika adhabu ya Mwenyezi Mungu)
[Ole wako, ole wako!Kisha Ole wako, ole wako!] [75:34-35].
Adui wa Mwenyezi Mungu akasema, "Hivi Unanitisha Ewe Muhammad, Wallahi, hutoweza wewe wala Mola wako chochote ... "157
Abu Jahl aliendelea na mwenendo wake huo bila kutanabahi kuwa anafanya mambo ya kipumbavu. Alidhamiria kufanya mambo mabaya zaidi dhidi ya Mtume ﷺ, aliapa kummwagia mchanga usoni na kumnyonga shingo yake. Alipokuwa anakwenda kutekeleza azma yake hiyo mara alionekana akirejea huku ameuziba uso wake kwa viganja vyake. Wafuasi wake walitaka kujua lililojiri. Akawaambia, "Nimehisi moto unaowaka ndani ya shimo na mbawa zinaruka." Baadaye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema:
[لَوْ دَنَا مِنِّي لاخْتَطَفَتْهُ الْمَلائِكَةُ عُضْوًا عُضْوًا]
[Angeendelea na azma yake, malaika toangeng'oa mbavu zake moja baada ya nuengine.]
Haya ndiyo baadhi ya madhila yaliyokuwa yakimwandama Mtume ﷺ, mtu maarufu, aliyeheshimiwa na watu wake na aliyeungwa mkono na mtu maarufu, ami yake Abu Talib. Kama hali ndiyo hiyo kwa Mtume ﷺ itakuwaje kwa watu dhaifu ambao hawakuwa na ukoo wa kuwasaidia.
(1) Huyu ni baba yake Khalifa wa Dola ya Umawiyyah, Marwan Bin Al- Hakam
(2) lbn Hisham, Juzuu 1, Uk. 416
(3) Sahihil Bukhari, Kitabu Wudhuu, Juzuu 1, Uk. 37.
(4) Hisham, Juzuu 1, Uk, 356-357.
(5) Fy Dhilalil Qur'an, Juzuu 29, Uk. 212
(6) Ibid. Juzuu 30, Uk. 208.
(7) Ibid. Juzuu 29, Uk. 302.
* Arraheeq Al Makhtuum Uk. 147-153
Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.